Jeshi la Polisi: Watanzania Msikubali Kabisa Kukamatwa Na Askari Asiye na Kitambulisho

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
40,476
Reaction score
26,173
Ndugu zangu Watanzania,

Embu Someni Habari hii muongeze Ufahamu kidogo.

👉Jeshi la Polisi mkoani Geita limewataka wananchi kutokubali kukamatwa na mtu yeyote anayedai kuwa askari polisi bila kuonyesha kitambulisho na kueleza kituo gani alichotokea.

Kamanda wa Polisi humo, Safia Jongo ametoa kauli hiyo Aprili 8, 2025 wakati wa mafunzo ya ulinzi shirikishi na polisi jamii, yaliyotolewa kwa watendaji wa kata, vijiji, mitaa, wenye viti na maofisa tarafa, yaliyoandaliwa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na mgodi wa dhahabu wa Geita (GGML) kwa lengo la kuimarisha usalama wa wananchi kupitia ushirikiano wa karibu.

Amesema kumekuwa na matukio ya utekaji, yanayodaiwa kufanywa na watu waliovaa sare za polisi, wakiwa kwenye magari yanayodaiwa kuwa ya Serikali, lakini hawatoi uthibitisho wowote kwa wananchi jambo linalotia hofu na kuathiri imani kwa vyombo vya dola.

“Askari wa kweli anapokwenda kukamata mtu lazima ajitambulishe kwa jina, awe na kitambulisho cha kazi na aseme anatoka kituo gani. Kama hana hivyo, huyo si askari ni mtu wa kawaida ambaye anaweza kuwa jambazi au mhalifu,” amesema Safia.
Screenshot_20250409-132651_1.jpg

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Soka yuko wapi kunguni wa mama??

Mara ya mwisho alipigiwa simu akachukue pikipiki yake kituo cha polisi Chang'ombe na hakuwahi kuonekana hadi leo.

Huyo mama unayesema amewafikia mamilioni mbona hajaifikia familia ya Soka na kuwapatia suluhu?
 
Ndugu zangu Watanzania,

Embu Someni Habari hii muongeze Ufahamu kidogo.

👉Jeshi la Polisi mkoani Geita limewataka wananchi kutokubali kukamatwa na mtu yeyote anayedai kuwa askari polisi bila kuonyesha kitambulisho na kueleza kituo gani alichotokea.

Kamanda wa Polisi humo, Safia Jongo ametoa kauli hiyo Aprili 8, 2025 wakati wa mafunzo ya ulinzi shirikishi na polisi jamii, yaliyotolewa kwa watendaji wa kata, vijiji, mitaa, wenye viti na maofisa tarafa, yaliyoandaliwa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na mgodi wa dhahabu wa Geita (GGML) kwa lengo la kuimarisha usalama wa wananchi kupitia ushirikiano wa karibu.

Amesema kumekuwa na matukio ya utekaji, yanayodaiwa kufanywa na watu waliovaa sare za polisi, wakiwa kwenye magari yanayodaiwa kuwa ya Serikali, lakini hawatoi uthibitisho wowote kwa wananchi jambo linalotia hofu na kuathiri imani kwa vyombo vya dola.

“Askari wa kweli anapokwenda kukamata mtu lazima ajitambulishe kwa jina, awe na kitambulisho cha kazi na aseme anatoka kituo gani. Kama hana hivyo, huyo si askari ni mtu wa kawaida ambaye anaweza kuwa jambazi au mhalifu,” amesema Safia.View attachment 3297723

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Asante, sasa tutawaua sana
 
Soka yuko wapi kunguni wa mama??

Mara ya mwisho alipigiwa simu akachukue pikipiki yake kituo cha polisi Chang'ombe na hakuwahi kuonekana hadi leo.

Huyo mama unayesema amewafikia mamilioni mbona hajaifikia familia ya Soka na kuwapatia suluhu?
Embu fika kwanza kwenye hicho kituo cha polisi unachokisema ili ukawaambie hayo maelezo yako.
 
Hiyo ni taarifa ya kuwaelimisha watanzania wasiojua jambo hilo.
Mwashambwa bwana, kwani hao wakamataji wanajituma wenyewe au wanatumwa na kupewa maelekezo kutoka juu.
Mbona mnatufanya mabwege sana!
Usicheze na mfumo na siokwamba hawaijui sheria wanaijua A to Z but ..............
 
Pumbavu wakati wanakulazimisha kukukamata pasi na kuonesha kitambulisho?
😄😄Usijali maana polisi wetu ni waungwana sana na watajitambulisha wakija kukukamata. Watakuwa wanapiga hadi na stori na wewe hadi utafurahi Mwenyewe hata kama ulikuwa na mawazo utajikuta umepata amani
 
Mwashambwa bwana, kwani hao wakamataji wanajituma wenyewe au wanatumwa na kupewa maelekezo kutoka juu.
Mbona mnatufanya mabwege sana!
Usicheze na mfumo na siokwamba hawaijui sheria wanaijua A to Z but ..............
Wala usiogope.hata ukiwa umechelewa magari usiku waweza kuomba rift kwenye gari la polisi na ukasaidiwa kusogezwa mbele
.
 
Wewe unajielewa kweli?

Unajua kusoma kwa ufahamu?

Soma nilichoandika tena ndio ujibu.
Wewe si una ushahidi wa maneno yako? Sasa unaogopa nini ndugu yangu mtanzania uliyejaa msongo wa mawazo kufika kituo cha polisi. Halafu CHADEMA hamuaminiki maana majuzi tu hapa mlimpiga mangumi na mateke yule mwenezi wa BAWACHA. Angekufa mngesingizia kauwawa na watu wasio julikana.
 
Kuna mtu litamkuta jambo wakati wa kudai kitambulisho
Wala msiogope kuomba kitambulisho kwa askari wetu. Maana askari wetu ni weledi sana na wenye kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya jeshi la polisi
 
Wewe si una ushahidi wa maneno yako? Sasa unaogopa nini ndugu yangu mtanzania uliyejaa msongo wa mawazo kufika kituo cha polisi. Halafu CHADEMA hamuaminiki maana majuzi tu hapa mlimpiga mangumi na mateke yule mwenezi wa BAWACHA. Angekufa mngesingizia kauwawa na watu wasio julikana.
Soka ameitwa kituo cha polisi na hadi leo hajawahi kuonekana halafu unauliza ushahidi kutoka kwangu?

Namba ya mwisho kuongea na Soka kwa mujibu wa waliokuwa karibu yake ni ya afande wa kituo cha polisi Chang'ombe.

Kunguni wa mama Abdul akili mliweka rehani?
 
Back
Top Bottom