Jeshi la Polisi: Watanzania Msikubali Kabisa Kukamatwa Na Askari Asiye na Kitambulisho

Ndugu zangu Watanzania,

Embu Someni Habari hii muongeze Ufahamu kidogo.

👉Jeshi la Polisi mkoani Geita limewataka wananchi kutokubali kukamatwa na mtu yeyote anayedai kuwa askari polisi bila kuonyesha kitambulisho na kueleza kituo gani alichotokea.

Kamanda wa Polisi humo, Safia Jongo ametoa kauli hiyo Aprili 8, 2025 wakati wa mafunzo ya ulinzi shirikishi na polisi jamii, yaliyotolewa kwa watendaji wa kata, vijiji, mitaa, wenye viti na maofisa tarafa, yaliyoandaliwa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na mgodi wa dhahabu wa Geita (GGML) kwa lengo la kuimarisha usalama wa wananchi kupitia ushirikiano wa karibu.

Amesema kumekuwa na matukio ya utekaji, yanayodaiwa kufanywa na watu waliovaa sare za polisi, wakiwa kwenye magari yanayodaiwa kuwa ya Serikali, lakini hawatoi uthibitisho wowote kwa wananchi jambo linalotia hofu na kuathiri imani kwa vyombo vya dola.

“Askari wa kweli anapokwenda kukamata mtu lazima ajitambulishe kwa jina, awe na kitambulisho cha kazi na aseme anatoka kituo gani. Kama hana hivyo, huyo si askari ni mtu wa kawaida ambaye anaweza kuwa jambazi au mhalifu,” amesema Safia.View attachment 3297723

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Angeongea IGP ndiyo tungeona wako serious...!
 
Soka ameitwa kituo cha polisi na hadi leo hajawahi kuonekana halafu unauliza ushahidi kutoka kwangu?

Namba ya mwisho kuongea na Soka kwa mujibu wa waliokuwa karibu yake ni ya afande wa kituo cha polisi Chang'ombe.

Kunguni wa mama Abdul akili mliweka rehani?
Hao mashuhuda kwanini wasiweke namba hiyo hadharani na kwenda kutoa ushahidi na maelezo yao kituoni
 
Na afande RPc ujilinde hasa maana kwa kauli hii, wenzako wanakuzyuuuumu
 
Waliomkamata Hayati Mzee Ally Kibao walikuwa na pingu Magari ya Polisi pamoja Bunduki za SMG ambazo hubebwa na Polisi je Marehemu angeazaje kuhoji wakati tekniki zilizotumika ni kama za kukamata Jambazi?
kibao.jpg

RIP Mzee Ally Kibao
 
Hao mashuhuda kwanini wasiweke namba hiyo hadharani na kwenda kutoa ushahidi na maelezo yao kituoni
Namba iliwekwa hadharani kule X polisi walichukua hatua gani?

Aliyemtishia kumuua Ben Saanane namba yake iliwekwa humu humu polisi walichukua hatua gani baada ya miezi miwili mbele Ben Saanane kupotea hadi leo ni miaka 9 hajulikani alipo.

Mzee Kibao alishushwa kwenye gari mchana kweupe na kupotea baadae alipopatikana amekufa huyo mama yenu alisema ni drama.

Huko bungeni Tulia akazima mjadala wa utekaji nakuwekea hapa video utazame.

View: https://youtu.be/8Gn4Bejv9Sc?si=Im5DHrVE5x41SGRv
 
Unaweza kufika kituo cha polisi kusaidia upelelezi
 
Nifike ili iweje?

Huna taarifa hao waliokuwa karibu na Soka walifika kituoni hapo na kupeleka huo ushahidi ikiwemo namba ya huyo polisi walipoona kimya ndio wakatoa taarifa kule X.

Na hadi leo ni zaidi ya miezi 6 serikali ya chura kiziwi iko kimya kuhusu utekaji inasema ni drama?
 
Hivi yule mwenezi wa BAWACHA aliyepigwa mangumi na kuumizwa vibaya . Kama ingetokea ameuwawa unafikiri lawama angetupiwa nani? Unafikiri CHADEMA wangeshindwa kuinyooshea kidole serikali? Unafikiri CHADEMA wasingesema serikali na vyombo vyake vya usalama wanahusika? Je hatua gani zimechukuliwa na CHADEMA juu ya uhuni uliofanyika wa kumuumiza ,kumtesa na kumjeruhi vibaya yule Dada?
 
Hivi yule mwenezi wa BAWACHA aliyepigwa mangumi na kuumizwa vibaya . Kama ingetokea ameuwawa unafikiri lawama angetupiwa nani?
Alipigwa na nani?

Hujajibu swali moja kuhusu utekaji wa Soka ushadandia mada mpya?
Unafikiri CHADEMA wangeshindwa kuinyooshea kidole serikali? Unafikiri CHADEMA wasingesema serikali na vyombo vyake vya usalama wanahusika? Je hatua gani zimechukuliwa na CHADEMA juu ya uhuni uliofanyika wa kumuumiza ,kumtesa na kumjeruhi vibaya yule Dada?
Chadema wameinyooshea serikali vidole mara ngapi?

Na katika hizo mara zote serikali iliponyooshewa kidole ilijibu vipi?
 
Ndugu zangu Watanzania,

Embu Someni Habari hii muongeze Ufahamu kidogo.

👉Jeshi la Polisi mkoani Geita limewataka wananchi kutokubali kukamatwa na mtu yeyote anayedai kuwa askari polisi bila kuonyesha kitambulisho na kueleza kituo gani alichotokea.

Kamanda wa Polisi humo, Safia Jongo ametoa kauli hiyo Aprili 8, 2025 wakati wa mafunzo ya ulinzi shirikishi na polisi jamii, yaliyotolewa kwa watendaji wa kata, vijiji, mitaa, wenye viti na maofisa tarafa, yaliyoandaliwa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na mgodi wa dhahabu wa Geita (GGML) kwa lengo la kuimarisha usalama wa wananchi kupitia ushirikiano wa karibu.

Amesema kumekuwa na matukio ya utekaji, yanayodaiwa kufanywa na watu waliovaa sare za polisi, wakiwa kwenye magari yanayodaiwa kuwa ya Serikali, lakini hawatoi uthibitisho wowote kwa wananchi jambo linalotia hofu na kuathiri imani kwa vyombo vya dola.

“Askari wa kweli anapokwenda kukamata mtu lazima ajitambulishe kwa jina, awe na kitambulisho cha kazi na aseme anatoka kituo gani. Kama hana hivyo, huyo si askari ni mtu wa kawaida ambaye anaweza kuwa jambazi au mhalifu,” amesema Safia.View attachment 3297723

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Kitambulisho sio solution. Majambazi wa Serikali wana kila kitu!
 
Polisi wa nchi gani hao?? Hawafanyi hivi japo tamko litasaidi wananchi kujilinda dhidi ya polisi watekaji
 
Jeshi la polisi, serikali na vyombo vingine vimeshindwa kabisa kapambana na kuwadhibiti hao wanaovaa uniform za polisi na kutumia na magari ya serikali kuteka watu duh kwani kuna jamhuri ndogo ya watekaji kati ya jamhuri ya Muungano tunayoijua?
 
Back
Top Bottom