Jeshi la Polisi: Watu 130 wakamatwa kwa tuhuma za mipango ya kuchoma shule na kuua viongozi

Jeshi la Polisi: Watu 130 wakamatwa kwa tuhuma za mipango ya kuchoma shule na kuua viongozi

Jeshi la Polisi nchini limetangaza kuwatia mbaroni jumla ya watuhumiwa 130 katika mikoa mbalimbali kwa tuhuma za kupanga na kuhamasisha vitendo vya kihalifu nchini ambapo watuhumiwa hao wanadaiwa kutumia vikao vya ndani na mitandao ya kijamii kuratibu mikakati ya kuvuruga amani na usalama wa taifa kati ya mwezi Juni na Julai mwaka huu.

Akizungumza kuhusu uzito wa njama hizo, Msemaji wa Jeshi la Polisi, DCP David Misime, amefichua mipango ya hatari iliyokuwa imeandaliwa na wahalifu hao akisema kuwa vitendo hivyo vya kihalifu vilikuwa ni pamoja na kupanga, kutamka, kuandaa na kusambaza taarifa za uchochezi, kuhamasisha watu kushiriki katika vitendo vya kihalifu vikiwepo kuua baadhi ya viongozi na wananchi.

"Walikuwa pia wamepanga na kuratibu kuchoma shule mbalimbali, kulipua transforma za umeme ili nchi iwe gizani, kuharibu na kupora mali za umma na za watu binafsi sambamba na kuua askari wa vyombo vya ulinzi na usalama ili kupora silaha”, ameeleza.

Pia soma: Polisi Tanzania wanadai Waandamanaji sasa Wanapanga kuua Viongozi, wameshaanza kuwakamata

Upuuzi mtupu yaani hawa polisi wetu hawajui hata mleta machafuko ni nani ,yaani wao mtu akitoa maoni tofauti tu yasiyoyapenda wanasema alikuwa anapanga maandamano...Non Sense.

Ubalozi wa US ulipolipuliwa mwaka 1998 ,jeshi la polisi lilikamata kijiji kizima na kuwaweka ndani lakini walipokuja wenye FBI/CIA wakawaambia wawaachie wote maana hakuna aliyehusika hata mmoja...hata hao 130 hakuna aliyepanga kuvuruga amani bali wamekamatwa kwa kutoa comment tu facebook au instagram.
 
Watu wamekubali kukaa kimya halafu mnawachokoza kwa nguvu.
 
Hivi unathibitisha vipi kuwa huyu mtu AMEPANGA kufanya jambo fulani? Maana naona kuna chance ya kusingiziwa watu wengi kwenye hili.

Sijaona mahali anasema wamekamata hata Bomu, Viberiti, Panga, Bunduki, Bastola, Rungu, Visu n.k ambavyo vina ashiria May be walikuwa wamepanga kuchoma sheli.

Tanzania bila rushwa, haiwezekani.
AI ndiyo wangeitumia kutenda hayo.
 
Back
Top Bottom