Jeshi la wananchi laonywa lisivunje katiba ya nchi kwa kufanya majukumu yasiyo yake kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi

Watanzania uzuzu wetu umeanzia kuonekana hapa hapa kwenye huu uzi. Yaani kabisa kuna watu wanamdhihaki na kumwona Mwambukusi kama amekosea. Watu kama hao unatarajia kuna siku watakomboka na kuwa huru kifikra???
[emoji2956][emoji2956]
 
Mwambulukusi Hoyeeee. Itisha mkutano na mdudu na slaa kama kawaida yenu, na yule askofu wenu. Mlianzishe na wanajeshi. Hili ndiyo dili. Tutawaunga mkono sisi wote.

Tena mwanzishe na maandamano yao haraka sana.
 
Punguza ujinga huko Ethiopia ulikwenda kichunga ng'ombe na huna unachojua! Hata JKT hujaenda utajua vipi kazi za military police!
 
Huyo mpuuzi jeshi halifanyi ujinga ukiona hivyo ujue kuna tishio kubwa sana la usalama, na toka matukio ya kibiti Police haiaminiki tena kwenye mambo nyeti, undercover police wasaliti walikuwa wengi sana
Ya Kibiti yalishadhibitiwa vyema na jeshi letu adhimu....ile ilikuwa ni kazi yao sahihi na kutukuka....

Hili la sare ni kazi ya PT....ni kazi yao kiraia....unaongea kihisia sana kinyume na UHALISIA [emoji1787][emoji1787]
 
Naunga mkono HOJA yako [emoji120][emoji120]
 
Jeshi linapaswa kuzagaa mtaani pale ambapo wanaona kuna external threat au wenyewe wameamua kuchukua nchi. Sasa kweli unakatiza mitaa ya mbagala kusaka sare za jeshi?
Fact...

Aibu kubwa hiyo....

PT wanatosha kuifanya hiyo kazi...kuruhusu hilo ni kulidharau PT.....

JWTZ iheshimu katiba....
 
Wakili MWABUKUSI yuko sahihi....

PT wanatosha kuhangaika na hizo sare.....

PENDEKEZO

Wizara zinashirikiana....hebu Wizara ya ulinzi ikae mezani na wizara ya mambo ya ndani "iwezeshane fungu" ili PT wetu waweze kuifanya hiyo kazi ya "kusanya sare za JWTZ"....

Kwani ni lazima kila siku tufanye yaleyale tuliyoyazoea?!! [emoji15][emoji15][emoji1787][emoji1787]

Dunia inabadilika na UBUNIFU unahitajika katika mambo mengi....

#SiempreJMT[emoji120]

#Karibuni Komoni[emoji120]
 
Kwani wote sini wapo kitengo jmn 🤣 hizi kelele zinatoka wap
 
Acha kuendelea kujidhalilisha! Mwanajeshi kupewa kazi nyingine inawezekana kuwa demotion au kimkakati na pia kustaafishwa kwa lazima lakini hahusiki na raia!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…