Naughty by nature
JF-Expert Member
- Jan 22, 2023
- 2,123
- 2,359
Mi pia katika ili namuunga mkono jamaaKwa mara ya kwanza naunga mkono Mwabukusu.Hii tabia ya Baadhi ya taarifa kujifanya ziko Juu ya sheria ikome mara Moja.
Kila taasisi itekeleze wajibu wake kwa.mujibu wa sheria ,hakuna raia aloye Juu ya mwingine Kwa kisingizio Cha mwanajeshi sijui Tiss na blaa blaa kama hizo.
Anachokitafuta atakipata[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Watanzania uzuzu wetu umeanzia kuonekana hapa hapa kwenye huu uzi. Yaani kabisa kuna watu wanamdhihaki na kumwona Mwambukusi kama amekosea. Watu kama hao unatarajia kuna siku watakomboka na kuwa huru kifikra???
Mkuu, mkoloni wa kwanza wa Mwafrica ni Mwafrica mwenzie..Watanzania uzuzu wetu umeanzia kuonekana hapa hapa kwenye huu uzi. Yaani kabisa kuna watu wanamdhihaki na kumwona Mwambukusi kama amekosea. Watu kama hao unatarajia kuna siku watakomboka na kuwa huru kifikra???
Hapana! Mwambikusi yupo sahihi,baada ya Bunge na Mahakama chombo peke kimebaki na heshima zake ni jeshi,sasa wasiliingize kwenye siasa ili nalo ligalagale kwenye tope Kama hao wengine. Sheria ipo wazi Nani mwenye Hilo jukumu la kufanya msako,nakuapia hakuna atakae thubutu kwenda kufanya msako baada ya Hilo onyo,maana wanajua kufanya hivyo ni uvunjaji wa Sheria,hayupo nasema hayupo,mtaniambia.Namheshimu sana Mwabukusi na ninamuunga mkono katika baadhi ya mambo kama DPW. Au kupinga badndari zetu kugawiwa bure kwa DPW.
Ila ktk ili nadhani hatofautishe utendaji wa kazi za jeshi na polisi. Pia hatofautishe sheria zetu jinai na taratibu za kijeshi.
Ajiulize, kwanini jeshi lina mahakama yake ya kijeshi. Kwanini mwanajeshi akivunja sheria lazima kwanza taratibu zao za kijeshi zifuate avuliwe uanajeshi ndipo taratibu za kawaida za kijinai zifuatwe.
Anatakiwa ajue taratibu za kijeshi na intelligency za kijeshi. Jeshi halikurupuki kufanya jambo. Si mara ya kwanza jeshi kufanya zoezi kama hili. Nakumbuka miaka ya nyuma mkoa fulani zoezi ili lilifanyika na lilisaidia kuzuia uharifu. Yaani ukichekea watu hati sheria za kijinai unaweza shangaa unajeshi lisilo rasmi nchini. Au watu tayari wanamiliki silaha.
Na zoezi ili ufanywa na Military police. Wanajua taratibu tuache wafanye
Acheni upumbavu baada ya kuvichafua vyombo vyote sasa mnaona na jeshi letu mlichafue si ndio,tuonyeshe Sheria inayotamka jwtz wanaweza kufanya hayo? Kazi za jeshi zinajulikana na polisi zinajulikana,sasa tuambie hizo yunifomu zilizotapakaa hapa Tanzania zipo wapi? Jeshi la polisi limeshindwa kufanya hiyo kazi?Ni vizuri upitie sheria za jeshi ujue military polisi ana wajibu gani na wakati gani anaweza fanya majukumu yake. Na majukumu yake nipamoja na nini. Natumai uwezi niuliza tena hilo swali!
Jeshi (JWTZ) lipo kwa ajili ya raia. Halipo kwa ajili yake binafsi. Lipo kulinda amani ya nchi na mipaka ya nchi. Sasa ikitokea uniform za jeshi zimeenea mtaani unadhani nini kinafuata?
Nimeishi Ethiopia, uniform za polisi ilitokea zikaenea sana kwa raia. kuna muda ilikuwa ngumu kutambuia polisi halali ni yupi kwa kuangalia. Hii ilileta madhara makubwa ktk amani ya nchi.
Walichelewa kuchukua hatua hivyo ilibidi wabadili mavazi ya jeshi la polisi nchi zima. japo madhara yalikuwa tayari yameisha tokea.
Kazi ya polisi ni maswala ya jinai na si vinginevyo.
Ebu nitajie kifungu cha sheria za jinai kinachoeleza kukutwa na mavazi ya jeshi la wananchi. Hapo ndo utajua kuwa unapokutwa na magwanda ya jeshi ufikishwi mahakamani. Bali magandwa ya JWTZ ni mali yao wanachofanya ni kuyachukua na kurejesha kwao.
Kwa maswala ya amani ya nchi ebu tuache siasa na ushabiki. Waacheni jeshi wafanye zoezi la kurejesha magwanda yao. Na uzuri wameomba watu warejeshe wao wenyewe.
Ila wale wabishi ndo wao jeshi watawafuata majumbani au kokote waliko kuyarejesha. Shida hiko wapi?
Ondoa HIV na COVID researches kwenye orodha, hizi siyo kazi za majeshiJeshi kuwekeza kwenye Research za HIV, COVID, Nuclear, Balistic Missiles, Ndege Jeshi, Submarines, wao wana hangaika na mitumba za Marehemu Wa Kizungu. Kiwanda chao cha Nyumbu kimeshindwa hata kuzalisha Bajaji za Abiria.
Wanajeshi inatakiwa wakaripoti polisi sare zao zilizopotea au kuibwa.jamaa zangu wa chadema kama mna sare zirudisheni tuh
Inasikitisha sanaWatanzania uzuzu wetu umeanzia kuonekana hapa hapa kwenye huu uzi. Yaani kabisa kuna watu wanamdhihaki na kumwona Mwambukusi kama amekosea. Watu kama hao unatarajia kuna siku watakomboka na kuwa huru kifikra???
Dark continentHivi, kwanini Tanzania na Africa kwa ujumla wenye akili uchukiwa kwa kiwango hiki?.
Hiyo ni kazi ya polisiMnaleta utani kwenye ulinzi wa Taifa, acheni upumbavu tutawafuata majumbani uniform za jeshi ni haramu kutumiwa na raia
Yeye anaongelea sheria wewe unaongelea porojo na stories tu.Namheshimu sana Mwabukusi na ninamuunga mkono katika baadhi ya mambo kama DPW. Au kupinga badndari zetu kugawiwa bure kwa DPW.
Ila ktk ili nadhani hatofautishe utendaji wa kazi za jeshi na polisi. Pia hatofautishe sheria zetu jinai na taratibu za kijeshi.
Ajiulize, kwanini jeshi lina mahakama yake ya kijeshi. Kwanini mwanajeshi akivunja sheria lazima kwanza taratibu zao za kijeshi zifuate avuliwe uanajeshi ndipo taratibu za kawaida za kijinai zifuatwe.
Anatakiwa ajue taratibu za kijeshi na intelligency za kijeshi. Jeshi halikurupuki kufanya jambo. Si mara ya kwanza jeshi kufanya zoezi kama hili. Nakumbuka miaka ya nyuma mkoa fulani zoezi ili lilifanyika na lilisaidia kuzuia uharifu. Yaani ukichekea watu hati sheria za kijinai unaweza shangaa unajeshi lisilo rasmi nchini. Au watu tayari wanamiliki silaha.
Na zoezi ili ufanywa na Military police. Wanajua taratibu tuache wafanye kazi.
Acha porojo, jeshi halitakiwi kuingilia kazi za polisi bila decree ya Rais.Huyo mpuuzi jeshi halifanyi ujinga ukiona hivyo ujue kuna tishio kubwa sana la usalama, na toka matukio ya kibiti Police haiaminiki tena kwenye mambo nyeti, undercover police wasaliti walikuwa wengi sana
PorojoNi vizuri upitie sheria za jeshi ujue military polisi ana wajibu gani na wakati gani anaweza fanya majukumu yake. Na majukumu yake nipamoja na nini. Natumai uwezi niuliza tena hilo swali!
Jeshi (JWTZ) lipo kwa ajili ya raia. Halipo kwa ajili yake binafsi. Lipo kulinda amani ya nchi na mipaka ya nchi. Sasa ikitokea uniform za jeshi zimeenea mtaani unadhani nini kinafuata?
Nimeishi Ethiopia, uniform za polisi ilitokea zikaenea sana kwa raia. kuna muda ilikuwa ngumu kutambuia polisi halali ni yupi kwa kuangalia. Hii ilileta madhara makubwa ktk amani ya nchi.
Walichelewa kuchukua hatua hivyo ilibidi wabadili mavazi ya jeshi la polisi nchi zima. japo madhara yalikuwa tayari yameisha tokea.
Kazi ya polisi ni maswala ya jinai na si vinginevyo.
Ebu nitajie kifungu cha sheria za jinai kinachoeleza kukutwa na mavazi ya jeshi la wananchi. Hapo ndo utajua kuwa unapokutwa na magwanda ya jeshi ufikishwi mahakamani. Bali magandwa ya JWTZ ni mali yao wanachofanya ni kuyachukua na kurejesha kwao.
Kwa maswala ya amani ya nchi ebu tuache siasa na ushabiki. Waacheni jeshi wafanye zoezi la kurejesha magwanda yao. Na uzuri wameomba watu warejeshe wao wenyewe.
Ila wale wabishi ndo wao jeshi watawafuata majumbani au kokote waliko kuyarejesha. Shida hiko wapi?
Akili zako kama za FaizaFoxyWewe ndo hutumii akili kwa sababu hujui majukumu ya jeshi. Mmekariri vita tu. Ha ha ha! Ingekuwa jeshi linasubiri vita kwanini mabalozi wengi duniani ni wanajeshi.
Kwa nini maofisa wengi balozini ni wanajeshi. Si wangekaa kambini kusubiri vita kama unavyomaanisha.
Kwanini kamati za usalama za nchi nyingi hata hapa Tanzania kamati za usalama zinajumuisha wanajeshi, anzia wilayani, mkoa hadi Taifa. Unajua vikao vya ulinzi na usalama vinajadili maswala gani?
Ati serikali! Unajua hiyo serikali inavyoendeshwa? Unajua mambo yote unayoyaona kuanzia kijinini kwenu, wilayani, mkoani hadi Taifa jeshi wanahusikaje?
Kwa taarifa yako humu duniani serikali zote zinategemea jeshi. Si maswala tu ya vita hata na mengineyo.
Kagame, na ethiopia wanaongoza kwa kuwa na wanajeshi wengi nje hawako kivita wapo kwa kazi maalum. Marekani, Uingereza, Ufaransa, na nchi zinginezo wanajeshi ndo maintellijensia wa uchumi. Jeshi linakazi zaidi ya vita.
Tafakari ndugu yangu. Unajua mambo unayoyaona nje ni tofauti na inavyokuwa ndani.
Mfano tu wakati Rais Magufuli amefariki kulitokea matafaruku nani ashike nchi, kuna baadhi ya viongozi waliosema Makamu wakati huo Samia hawezi. Ili liko wazi. Mama Samia alilisema na Mkuu wa Majeshi wakati huo aligusia kidogo.
Ni Mkuu wa majeshi ndo alie toa msimamo kuwa katiba ifuate wote wakaufyata! Kwanini Mkuu wa jeshi aliingia katika kikao cha serikali si angekuwa kambini kwa msemo wako.
Narudia jeshi si vita tu!
Nazidi kumuheshimu na kummelewa Bw. Mwakabusi...WAKILI MWABUKUSI ANATAKA MKUU WA MAJESHI AZUIE UVUNJIFU WA KATIBA.
"Nchi inaongozwa kwa mujibu wa sheria na katiba. Kazi ya kukamata wa halifu ni ya Jeshi la Polisi. Jeshi la wananchi halina mamlaka kisheria na kikatiba kuingia kufanya msako mitaani kwa kisingizio cha kutafuta sare zao. Jukumu lao ni kulinda mipaka ya nchi. Cha ajabu hawajatuambia walizipeleka lini huko mitaani au zilichukuliwa na nani au waliibiwa lini? This is more than a comic [Huu ni usanii]!
Mwanajeshi hana mamlaka ya kupekua mtu katika makazi yake au maungo ya raia. Hii ni kazi ya Polisi wetu. Isipokuwa pale kunapokuwa na hali ya hatari au tishio dhahiri la mapinduzi.
Sheria inaruhusu kukataa ukamataji haramu na iwapo jeshi litaingia kwa namna hii ni haki ya wananchi kukataa ukamataji au upekuzi haramu usiofuata sheria ikiwemo kumshtaki Mwanasheria mkuu na Mkuu wa Majeshi ili kulinda sheria na Katiba ya Nchi na kudai fidia ya usumbufu.
Kama jeshi limeibiwa sare zake likaripoti Polisi. Polisi wafanye uchunguzi na wakibaini kosa Polisi ndiyo wenye utaalamu wa kupeleleza uhalifu wa wizi. Jeshi au wanajeshi hawako juu ya sheria [hivyo] wapunguze mihemko.
Kumekuwa na ujasiri wa uvunjaji katiba na sheria na kuwatisha wananchi katika taifa letu katika uongozi huu wa sasa na kwa hili hatutakubali na tutalitolea tamko rasmi kupinga vurugu hizi katika utumishi wa umma.
Mkuu wa Majeshi awajibike haraka kuzuia ukora huu wanaotaka au kupanga kuufanya!
Najisikia aibu sana kuishi na kushuhudia viroja hivi. Mungu bariki Watanganyika! Mungu ibariki Tanzania! Mungu waadhibu na kuwakemea madhalimu wote.
Boniface Kajunjumele Mwabukusi!
Tunasikitisha tulivyo na uelewa mdogo, aidha wa haki zetu au KATIBA!Kuna kitu naanza kuhisi
Ukifikiri kwa makini lile tamko la JWTZ kuhusu sare za jeshi naliona kama lina mlengo mwingine tofauti na ambavyo limewasilishwa.
Kwanini kusalimisha sare kuambatane na msako wa nyumba kwa nyumba kukagua watu ambao hawajakabidhi sare?
Vipi kama hao wanajeshi wana agenda yao nyingine?
Kupitia sakata la bandari na jinsi upinzani walivyo chachamaa kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na ubovu wa mkataba.
Huku wakihamasisha wananchi waukatae pamoja na kuongeza nguvu ya kudai katiba mpya, na mwitikio wa wananchi umekuwa mkubwa.
Vipi kama ujio wa wanajeshi mtaani hauna lengo la kukusanya sare bali kuwatisha raia ambao hivi karibuni wamekuwa wakihamasishwa kufanya maandamano ya kupinga mkataba?