Jeshi la wananchi laonywa lisivunje katiba ya nchi kwa kufanya majukumu yasiyo yake kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi

Jeshi la wananchi laonywa lisivunje katiba ya nchi kwa kufanya majukumu yasiyo yake kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi

Kuna wakati wananchi tunaonekana kudhalilika juu Serikali ya awamu hii, hatukubali huu udhalimu.
 
Military police wa JWTZ ni kwa ajili ya raia

Military police wa JWTZ ni kwa ajili ya raia?
Ni vizuri upitie sheria za jeshi ujue military polisi ana wajibu gani na wakati gani anaweza fanya majukumu yake. Na majukumu yake nipamoja na nini. Natumai uwezi niuliza tena hilo swali!

Jeshi (JWTZ) lipo kwa ajili ya raia. Halipo kwa ajili yake binafsi. Lipo kulinda amani ya nchi na mipaka ya nchi. Sasa ikitokea uniform za jeshi zimeenea mtaani unadhani nini kinafuata?

Nimeishi Ethiopia, uniform za polisi ilitokea zikaenea sana kwa raia. kuna muda ilikuwa ngumu kutambuia polisi halali ni yupi kwa kuangalia. Hii ilileta madhara makubwa ktk amani ya nchi.

Walichelewa kuchukua hatua hivyo ilibidi wabadili mavazi ya jeshi la polisi nchi zima. japo madhara yalikuwa tayari yameisha tokea.

Kazi ya polisi ni maswala ya jinai na si vinginevyo.

Ebu nitajie kifungu cha sheria za jinai kinachoeleza kukutwa na mavazi ya jeshi la wananchi. Hapo ndo utajua kuwa unapokutwa na magwanda ya jeshi ufikishwi mahakamani. Bali magandwa ya JWTZ ni mali yao wanachofanya ni kuyachukua na kurejesha kwao.

Kwa maswala ya amani ya nchi ebu tuache siasa na ushabiki. Waacheni jeshi wafanye zoezi la kurejesha magwanda yao. Na uzuri wameomba watu warejeshe wao wenyewe.

Ila wale wabishi ndo wao jeshi watawafuata majumbani au kokote waliko kuyarejesha. Shida hiko wapi?
 
WAKILI MWABUKUSI ANATAKA MKUU WA MAJESHI AZUIE UVUNJIFU WA KATIBA.

"Nchi inaongozwa kwa mujibu wa sheria na katiba. Kazi ya kukamata wa halifu ni ya Jeshi la Polisi. Jeshi la wananchi halina mamlaka kisheria na kikatiba kuingia kufanya msako mitaani kwa kisingizio cha kutafuta sare zao. Jukumu lao ni kulinda mipaka ya nchi. Cha ajabu hawajatuambia walizipeleka lini huko mitaani au zilichukuliwa na nani au waliibiwa lini? This is more than a comic [Huu ni usanii]!

Mwanajeshi hana mamlaka ya kupekua mtu katika makazi yake au maungo ya raia. Hii ni kazi ya Polisi wetu. Isipokuwa pale kunapokuwa na hali ya hatari au tishio dhahiri la mapinduzi.

Sheria inaruhusu kukataa ukamataji haramu na iwapo jeshi litaingia kwa namna hii ni haki ya wananchi kukataa ukamataji au upekuzi haramu usiofuata sheria ikiwemo kumshtaki Mwanasheria mkuu na Mkuu wa Majeshi ili kulinda sheria na Katiba ya Nchi na kudai fidia ya usumbufu.

Kama jeshi limeibiwa sare zake likaripoti Polisi. Polisi wafanye uchunguzi na wakibaini kosa Polisi ndiyo wenye utaalamu wa kupeleleza uhalifu wa wizi. Jeshi au wanajeshi hawako juu ya sheria [hivyo] wapunguze mihemko.

Kumekuwa na ujasiri wa uvunjaji katiba na sheria na kuwatisha wananchi katika taifa letu katika uongozi huu wa sasa na kwa hili hatutakubali na tutalitolea tamko rasmi kupinga vurugu hizi katika utumishi wa umma.

Mkuu wa Majeshi awajibike haraka kuzuia ukora huu wanaotaka au kupanga kuufanya!

Najisikia aibu sana kuishi na kushuhudia viroja hivi. Mungu bariki Watanganyika! Mungu ibariki Tanzania! Mungu waadhibu na kuwakemea madhalimu wote.

Boniface Kajunjumele Mwabukusi!
Kule gabon Guinea na Nijer wanasheria wana kazi gani kwa sasa?
 
Watanzania tuache kuchekea ujinga. Jwshi linapaswa kufanya mambo serious na sio kuanza kusumbua raia. Jeshi linapaswa kuwa sehemu ya raia kukimbilia pale ambapo vyombo vingine vyote vimeshindwa
Umeongea ukweli... Jeshi kuingia mtaani labda ni mapinduzi au kusaka waasi. Hiki wanachokifanya ni kutafuta kiki
 
Namheshimu sana Mwabukusi na ninamuunga mkono katika baadhi ya mambo kama DPW. Au kupinga badndari zetu kugawiwa bure kwa DPW.
Ila ktk ili nadhani hatofautishe utendaji wa kazi za jeshi na polisi. Pia hatofautishe sheria zetu jinai na taratibu za kijeshi.

Ajiulize, kwanini jeshi lina mahakama yake ya kijeshi. Kwanini mwanajeshi akivunja sheria lazima kwanza taratibu zao za kijeshi zifuate avuliwe uanajeshi ndipo taratibu za kawaida za kijinai zifuatwe.

Anatakiwa ajue taratibu za kijeshi na intelligency za kijeshi. Jeshi halikurupuki kufanya jambo. Si mara ya kwanza jeshi kufanya zoezi kama hili. Nakumbuka miaka ya nyuma mkoa fulani zoezi ili lilifanyika na lilisaidia kuzuia uharifu. Yaani ukichekea watu hati sheria za kijinai unaweza shangaa unajeshi lisilo rasmi nchini. Au watu tayari wanamiliki silaha.

Na zoezi ili ufanywa na Military police. Wanajua taratibu tuache wafanye kazi.
Ulicholeta hapa ni uzuzu. Kumiliki sare za jeshi ni kosa hakuna anayepinga. Lakini mamlaka yenye wajibu wa kukamata na kufikisha mahakamani hawa wahalifu ni jeshi la polisi. Military police hawapaswi na hawaruhusiwi kisheria kushughulika na raia katika hali ya kawaida. Kukiwa na hali ya hatari wanajeshi wanaweza kuitwa kusaidiana na polisi kudumisha/kurejesha amani na usalama. Anachokumbusha Mwabukusi ni kila mamlaka itekeleze wajibu wake kwa kufuata sheria. Vinginevyo hakungekuwa na haja ya kuwa na sheria. Ni aibu kwa "jeshi la sita" kwa ubora kuanza kuhangaika na vibaka walioiba sare za jeshi, au raia wema wasio na ufahamu, waliovaa mitumba inayofanana na sare za majeshi yetu.
Afrika wajinga wengi sana. Huyo atakuumiza akili.
Kusaka sare za jeshi, ni kazi ya polisi na siyo jeshi.
Ukiwa na bunduki kwanini wanakufuata polisi na siyo jeshi la wananchi?
Jwtz imekosa kazi.
Iwe bunduki au silaha yoyote ya jeshi, wanaopaswa kukufuatilia ni jeshi la polisi, labda kama hawana ujuzi na hiyo silaha ndipo jeshi (JWTZ) litahusishwa
 
Unataka tuamini kwamba huko mahakama hazipo kabisa ebu fafanua.
Ndugu General([emoji294][emoji294][emoji294][emoji294])
aliyechukua madaraka amefuta katiba + porojo zote za mahakama
 
Anachokitafuta atakipata[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Tunahitaji wananchi wote wawe na uelewa, wajue majukumu ya kila taasisi na yao pia kisheria, waweze kutambua haki zao ili waweze kupambana katika dunia yya ushindani.
Umasikini wa nchi una uhusiano mkubwa sana na kujielewa kwa jamii na raia kwa ujumla.
Hoja za Mwabukusi ni za msingi sana katika kujenga uzalendo kwa sababu hakuna mzalendo wa kweli ambaye ni muoga kwa sababu ya ujinga au kutojielewa.
Raia wengi wa nchi tajiri wana uelewa na siyo waoga ambapo katika nchi masikini ni kinyume chake.
Kuwa na raia wasio waoga, wenye uelewa na majasiri ni manufaa kwa nchi na kinyume chake ni hasara kwa nchi na dunia kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom