Jeshi la wananchi laonywa lisivunje katiba ya nchi kwa kufanya majukumu yasiyo yake kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi

Jeshi la wananchi laonywa lisivunje katiba ya nchi kwa kufanya majukumu yasiyo yake kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi

Sheria zetu zinasema je?
Kama tumejiwekea sheria kufuata mnapata taabu ya nini
kifungu gani kinamtaka lieutenant aingie kwa mtogole kusaka magwanda ya jeshi?
 
jamaa zangu wa chadema kama mna sare zirudisheni tuh
Hakuna sare ama kesi hapo.

Ukiona nguo inayofanana na nguo ya jeshi usiseme ni "nguo ya jeshi" bali sema "nguo zinazofanana na nguo za...".

Je kitu kufanana ndiyo kuwa ni kitu halisi?

Je mtu anaweza kutiwa hatiani kwa kosa la kufanana, kufananishwa ama kutumia bidhaa zinazofanana na bidhaa zenye "marufuku"?

Tangia day1 yule mwanajeshi alipotoa tangazo hilo kwa waandishi wa habari, tuliosikiliza tuliona ni la vioja!

Tulisema wazi kuwa majeshi ya Tz hayana haki miliki ya nguo wanazovaa, bali huagiza kwa kutumia wazabuni kwa gharama wanazokubaliana.

Na mzabuni huagiza kokote, ndani ama nje ya nchi kwa bei anayoiona itamletea faida.

Pia nguo zinazofanana na za jeshi ni karibu rangi zote za vitambaa vya suti madukani vinashonwa sare za jeshi.

Na tulisema pia maswali muhimu aliyoulizwa afisa huyo hakuweza kuyajibu kwa ufasaha, aliyakwepa au alijiuma uma.

Nilimsikia mwandishi mmoja akiuliza kuhusu wasanii wanaovaa mavazi majukwaani yenye kufanana na "kombati", swali hilo alishindwa kulijibu nadhani hakulitegemea kuulizwa, maana majibu aliyotoa si ya kisheria!

Tuliuliza pia kama kutakuwa na gharama za fidia watakazopewa wafanya biashara wa nguo watakaosalimisha hiyo mitumba na majora ya nguo zenye rangi zinazofanana na rangi wanazotumia wanajeshi.

Wapi walipoandaa centre ama base "afficial"
kusalimishia mabelo hayo?

Suala hili linagusa mpaka uchumi wa nchi likichukuliwa seriously!

Kwa jicho la tatu, tuliona ni tamko la kisiasa kwa sababu lilianza kutolewa pindi Mbowe alipoonekana akihutubia kwenye mkutano kuupiga madongo "mkataba wa bandari", huku nyuma yake kukiwa na mpambe kavaa nguo zinazofanana na za jeshi.

Sasa wanajeshi wameanza fitina na figisu za kisiasa?

Kwa kauli hii jeshi limejidhalilisha sana kwa sababu zifuatazo kama alivyosema wakili:

Hawana mandet ya kufanya wanayotaka kuyafanya bali ni Polisi.

Pia rangi zote za nguo wanazovaa hawana haki miliki zake, iwe za baka baka, ama rangi moja, bali wana haki ya kuvaa nguo hizo kwa kununua kama walivyo na haki raia.

Kama wanahaki hiyo wasimame hadharani waoneshe hakimiliki hiyo ya kumiliki rangi hizo kisheria ili kila raia ama wafanya biashara waelewe namna ya kuepuka kutumia ama kununua rangi ambazo zina hakimiliki ya taasisi za majeshi ya Taifa ama Polisi, Magereza, Zimamoto, Uhamiaji na Migambo.
 
Namheshimu sana Mwabukusi na ninamuunga mkono katika baadhi ya mambo kama DPW. Au kupinga badndari zetu kugawiwa bure kwa DPW.
Ila ktk ili nadhani hatofautishe utendaji wa kazi za jeshi na polisi. Pia hatofautishe sheria zetu jinai na taratibu za kijeshi.

Ajiulize, kwanini jeshi lina mahakama yake ya kijeshi. Kwanini mwanajeshi akivunja sheria lazima kwanza taratibu zao za kijeshi zifuate avuliwe uanajeshi ndipo taratibu za kawaida za kijinai zifuatwe.

Anatakiwa ajue taratibu za kijeshi na intelligency za kijeshi. Jeshi halikurupuki kufanya jambo. Si mara ya kwanza jeshi kufanya zoezi kama hili. Nakumbuka miaka ya nyuma mkoa fulani zoezi ili lilifanyika na lilisaidia kuzuia uharifu. Yaani ukichekea watu hati sheria za kijinai unaweza shangaa unajeshi lisilo rasmi nchini. Au watu tayari wanamiliki silaha.

Na zoezi ili ufanywa na Military police. Wanajua taratibu tuache wafanye kazi.
UMEULIZWA JESHI LINA HAKI YA KUPEKUA RAIA MITAANI AU KUKAMATA?
 
Huyo mpuuzi jeshi halifanyi ujinga ukiona hivyo ujue kuna tishio kubwa sana la usalama, na toka matukio ya kibiti Police haiaminiki tena kwenye mambo nyeti, undercover police wasaliti walikuwa wengi sana
Umeambiwa taratibu za kisheria, wewe unaleta porojo
 
Kuna kitu naanza kuhisi

Ukifikiri kwa makini lile tamko la JWTZ kuhusu sare za jeshi naliona kama lina mlengo mwingine tofauti na ambavyo limewasilishwa.

Kwanini kusalimisha sare kuambatane na msako wa nyumba kwa nyumba kukagua watu ambao hawajakabidhi sare?

Vipi kama hao wanajeshi wana agenda yao nyingine?

Kupitia sakata la bandari na jinsi upinzani walivyo chachamaa kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na ubovu wa mkataba.

Huku wakihamasisha wananchi waukatae pamoja na kuongeza nguvu ya kudai katiba mpya, na mwitikio wa wananchi umekuwa mkubwa.

Vipi kama ujio wa wanajeshi mtaani hauna lengo la kukusanya sare bali kuwatisha raia ambao hivi karibuni wamekuwa wakihamasishwa kufanya maandamano ya kupinga mkataba?
Yes umenisanua kitu aiseeh
 
Ni vizuri upitie sheria za jeshi ujue military polisi ana wajibu gani na wakati gani anaweza fanya majukumu yake. Na majukumu yake nipamoja na nini. Natumai uwezi niuliza tena hilo swali!

Jeshi (JWTZ) lipo kwa ajili ya raia. Halipo kwa ajili yake binafsi. Lipo kulinda amani ya nchi na mipaka ya nchi. Sasa ikitokea uniform za jeshi zimeenea mtaani unadhani nini kinafuata?

Nimeishi Ethiopia, uniform za polisi ilitokea zikaenea sana kwa raia. kuna muda ilikuwa ngumu kutambuia polisi halali ni yupi kwa kuangalia. Hii ilileta madhara makubwa ktk amani ya nchi.

Walichelewa kuchukua hatua hivyo ilibidi wabadili mavazi ya jeshi la polisi nchi zima. japo madhara yalikuwa tayari yameisha tokea.

Kazi ya polisi ni maswala ya jinai na si vinginevyo.

Ebu nitajie kifungu cha sheria za jinai kinachoeleza kukutwa na mavazi ya jeshi la wananchi. Hapo ndo utajua kuwa unapokutwa na magwanda ya jeshi ufikishwi mahakamani. Bali magandwa ya JWTZ ni mali yao wanachofanya ni kuyachukua na kurejesha kwao.

Kwa maswala ya amani ya nchi ebu tuache siasa na ushabiki. Waacheni jeshi wafanye zoezi la kurejesha magwanda yao. Na uzuri wameomba watu warejeshe wao wenyewe.

Ila wale wabishi ndo wao jeshi watawafuata majumbani au kokote waliko kuyarejesha. Shida hiko wapi?
Umeandika kilichomo kichwani kwako , hujajibu hoja
 
Mnaleta utani kwenye ulinzi wa Taifa, acheni upumbavu tutawafuata majumbani uniform za jeshi ni haramu kutumiwa na raia
Hakuna anepinga kua Uniform za Jeshi ni haramu kutumiwa na Raia. Ila kufuata hizo uniform kwa Raia bila kufuata sharia ni haramu pia.

Kila mtu afuate sharia za nchi hii katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku.

Hongera sana Mwabukisi
 
Back
Top Bottom