Jeshi letu lijifunze kutokana na vita ya Ukraine na sasa huko Israel/Hamas

Jeshi letu lijifunze kutokana na vita ya Ukraine na sasa huko Israel/Hamas

Tuanze kubadili mindset.

Hii nchi siyo ya viongozi bali ya raia. Tukiweza kuwaelimisha vijana wetu majeshini kuhusu hilo tutakuwa na wepesi kupiga hatua gatuzi za maendelek
Viongozi ndiyo wanafanya raia wawe siyo wazalendo...
Vita vyote unavyoviona huko nchi zingine,wanaopigana siyo wanajeshi tu mpaka raia nao wanavaa magwanda wanaenda frontline
Sasa kuna nchi moja wao wanajiona
Kama wana hakimiliki wao ndiyo wanafanya kila kitu

Ova
 
TUombe vita visitokee, hali ya jeshi letu tunaikuza, huo uzalendo wa karatasi na uongo sina, tunahitaji mafunzo zaidi na zana za kisasa, tuko nyuma mnoo
Wewe ni Mtanzania? Kama kweli nasikia una undugu na Omani kwa mjibu wa yule Prof Kabudi alietuahidi Noah kila mtanzania
 
Mkuu mimi natengeneza sana hizi drone,sijui kwanini jwtz haitoi sapoti nifanye kazi nao.
Naweza kutuma drone dar nikiwa mwanza na haikosei nilipoituma.

Niko tanzania hii hii,wakinihitaji napatikana.

Sio kwamba sina kazi,nina ajira rasmi kabisa ya serikali.

Wakinihitaji naweza kuhamia hata kwao.
Tulikataza viroba wakahamia kwenye Cuca za kwenye vichupa..Sasa ona madhara yake!

Kama siyo vicuca basi Johnson Johnson imeanza kufanyakazi!
 
Tulikataza viroba wakahamia kwenye Cuca za kwenye vichupa..Sasa ona madhara yake!

Kama siyo vicuca basi Johnson Johnson imeanza kufanyakazi!
Sasa kwa kejeli hizi unadhani watu itatusaidia?

Kitu usichokijua heri kutulia tu,ukiona ile ni technolojia kubwa wengine hayo tunafanya toka std 7 huko.

Hii ndiyo shid ya jamii forum,bora ungeuliza hata baadhi ya kazi zangu sio kejeli.
Haina shida,subiri 2024 utaona kitu hewani toleo jipya kabisa.
 
Kuna siku walikuwa wanafanya mazoezi huko kusini yaana silaha zetu ni vichekesho za kizamani mno zimejaa kutu yaani kiufupi leo hii tukijichanganya hata kwa uganda tutapoteana.
 
Dah!

Mkuu ina maana tuna hali mbaya?

Kwanini tusitumie watafiti wetu waliopo hapahapa nchini?

Mimi mwenyewe kwenye kutengeneza drone naweza sana,tena full automated.

Mwaka kesho nitarusha moja,wakinihitaji niko tayari kufanya kazi nao.
Hapa tunazungumzia drone za kijeshi, sio drones za kupiga picha
 
Ni kweli! Nadhani Jeshi letu liko vizuri tu, maana kama linashika namba 6 duniani kwa ubora, ni swala la kuwekeza tu katika Technology ya zana za kivita.
Lakini hata hivyo bajeti ni changamoto, na sijui Serikali inatenga kiasi gani kila mwaka katika bajeti kwa ajili ya Wizara ya Ulinzi!
Tatizo jeshi limetekwa na wanasiasa ndio maana hata wewe unasingizia tatizo bajeti wakati uhuni wa kisiasa ukiendelea Kwa vikesi uchwara mabilioni ya kulipa fidia yapo Tena Kwa haraka lakini kuweleza kwenye teknolijia bajeti hakuna hii nchi ngumu sanaa
 
Huko sahihi mkuu! Kwenye ghala nahisi kuna bastora na mapanga tu😂
20230919_141508.jpg
 
Tatizo jeshi limetekwa na wanasiasa ndio maana hata wewe unasingizia tatizo bajeti wakati uhuni wa kisiasa ukiendelea Kwa vikesi uchwara mabilioni ya kulipa fidia yapo Tena Kwa haraka lakini kuweleza kwenye teknolijia bajeti hakuna hii nchi ngumu sanaa
Juzi kati hapa pande za msata walikuwa wanafanya drills zao
Zile...
Aise walininginiza chupa za juice maji mo energy kama ndy target
Kifupi tu wasipende kuonesha mazoezi yao maana watu wanawachora tu
Hatujui lakini,labda kama wana silaha za kisasa wanaZificha hawataki kuzionesha hadharani

Ova
 
Nijuavyo Silaha sio ushindi katika vita...
Bali Ni mbinu madhubuti Descpline ya askari.
Maana ukikosa hivyo hata uwe na makombora yapi hushindi vita
 
Viongozi ndiyo wanafanya raia wawe siyo wazalendo...
Vita vyote unavyoviona huko nchi zingine,wanaopigana siyo wanajeshi tu mpaka raia nao wanavaa magwanda wanaenda frontline
Sasa kuna nchi moja wao wanajiona
Kama wana hakimiliki wao ndiyo wanafanya kila kitu

Ova
Na majeshi yetu yanajisahau.

Hayataki kutambua kwamba maslahi ya nchi yanahusu raia wote. Wao wamewekeza kwa viongozi kwa sababu wanapewa rushwa za teuzi hata baada ya kustaafu.


The real enamy wa nchi ni greedy politicians. Wamejaa tele
 
Kati ya taasisi nyeti ninazoziheshimu na kuzienzi ni jeshi letu la JWTZ, limeonyesha ukomavu wake kwa miaka mingi sana hasa wakati wa vita ya ukombozi.

Ilipoingia 1978, November/December hadi 1979, jeshi lilipitia "baptism of fire" wakati wa Vita ya Kagera.

Kimsingi baada ya vita ile ikadhihirika kuwa Defence Policy iko safi na inafanya kazi katika mazingira ya wakati ule.

Najua leo jeshi liko complex kuliko wakati huo na lina vyuo vyake ambavyo ni Think Tanks, kama National Defence College pale Kunduchi.

Sasa leo kuna vita hivi vya Ukraine na vile vile Israel na Hamas. Mbinu zilizojitokeza na kuwa very effective katika kushambulia adui, ni matumzi ya Drones na Missiles.

Huko Ukraine drones zimekuwa a weapon of choice katika ku target sehemu za adui kwa pande zote.

Hamas juzi kwa vifaa ambavyo waweza kufikiri ni vya mchezo mchezo tu, katumia drones ambazo zimechakaza vibaya miuondombinu ya kijeshi ya Israel iliyokuwa mstari wa mbele.

Kwamba wameuawa wanajeshi zaidi ya 300 wa Israel katika mashambulio, hilo na jambo kubwa sana.

Maoni yangu ni; Jeshi letu vile vile litazame upya Defence Policy yake ili matumizi ya vifaa hivi viweze kujumuishwa katika ulinzi wa nchi yetu.

Nawaza tu!
sawa umetumwa ujue sio ?
 
TUombe vita visitokee, hali ya jeshi letu tunaikuza, huo uzalendo wa karatasi na uongo sina, tunahitaji mafunzo zaidi na zana za kisasa, tuko nyuma mnoo
Nakubaliana nawe 100%. Ukiwaona Ijumaa wanapokimbia mchakamchaka utashangaa kama unaowaona kweli ni askari wanaoweza kupigana vita.

Their only area of competence is at harassing innocent civilians.
 
Back
Top Bottom