Stuxnet
JF-Expert Member
- Feb 12, 2011
- 18,875
- 29,427
Siyo kwa Tanzania. Huyo bwege mnampa trending za social media tu. Hii nchi haipinduliki.Umefuatilia ya captain Traore?, Ni kama captain Tesha alichofanya, na Traore alikaa msituni, vyombo vya habari na wanasiasa wenye ulaji walimponda na kusema ni muhuni tu aliyetokea jeshini, ila Traore aliendeleza harakati na falsafa zake ili kupata baadhi ya vijana wa kumuunga mkono na mwisho kuteka mji waliojaa maafisa na mkuu wa nchi.
Kwa nchi kama Tanzania au Bukina farso huwez tu ukatoka kimya kimya na kuichukua ikulu, lazima uligawanye kwanza jeshi na wakujue kuwa uyu ni mwenzetu, na lengo lake ni zuri na sio kutoka kimya kimya wanaweza fikiria ni kabaka kaingia ikulu, zikaja kambi zote.
Soma historia ya Tz kuanzia mutiny ya 1964 halafu angalia JKN aliisuka vipi JWTZ.
Sogea tena hadi 1967-70 wakati wa akina Sarakikya angalia JKN alifanya nini wakati vuguvugu la Askari wa kutoka Kaskazini.
Halafu kwenye 1990s kuna kikosi kutoka 30 Div kiliingia msituni Saranda kati ya Tabora na Singida, jiulize kiliiishia wapi!!
Narudia, "Keptein Tesha" ni wa mchongo tu. Ma captain hupindua nchi wala hawauzi sura kwanza kwenye Youtube