Jezi mpya za Simba kwa msimu wa 2021/22 zavuja

Jezi mpya za Simba kwa msimu wa 2021/22 zavuja

Tambala zinauzwa mitaani buku 6 na vunjabei halafu anawaletea leo eti mpya.
Mistari kama ya ikweta huoni aibu?[emoji23][emoji23]

Uto hizi siyo jezi za Vibwengo,yani mmeumia hadi basi,jezi kalii rangi zimetulia,siyo yale marangi utadhani CCM wako kwa mkutano wa Kampeni au mashamba ya alizeti Singida na wale vibwengo kama series ya “The Walking Dead”[emoji3][emoji3]
 
Kweli jezi za Simba zimevuja​

Today at 9:58 AM
Sasa wewe unaweka picha saa nne hii wakati watu wameshaanza kununua tangu saa mbili asubuhi, bado unangángánia kwamba zimevuja! Ni kwamba zinauzwa, sio kuvuja tena. hiyo ya kuvuja ilitakiwa uiseme kabla ya mauzo, na kama uliisema basi kwa sasa haina nguvu tena maana watu wamezivaa muda tu
 
Yes ni utani wa jadi,ila mi sijaona tatizo la jezi ya watani wetu Mikia........
 
Lawama kapewa Yanga.
Screenshot_20210903-124111_Instagram.jpg

Naona msimu huu mmekuwa malalamiko fc.Simba kila siku mnakazi ya kumtafuta mchawi mmeanza na Manara, leo mnamtafuta mchawi aliyevujisha jezi, mkaamua zigo mumbebeshe Yanga. Ila ndani ya Simba kuna akina Kassim Dewji, wanagonga copy watakavyo na hawaguswi.
 
Wanajamvi nimeshtushwa sana kuuona uzi wa simba mitandaoni kabala ya tarehe husika ambayo ilikuwa ni tarehe4 na si leo tarehe3 huu mchezo mchafu unatuharibia soka letu.
Ni kawaida sana hiyo
Kumbuka wanaotengeneza jezi siyo Simba SC, ni watu wengine huko China
Hata kwenye smartphones tunaona kabla Apple hawajazinfua iPhone 13 picha zime leak
 
Wanajamvi nimeshtushwa sana kuuona uzi wa simba mitandaoni kabala ya tarehe husika ambayo ilikuwa ni tarehe4 na si leo tarehe3 huu mchezo mchafu unatuharibia soka letu.
Rejea tangazo la leo. Jezi zipo madukani, kununua ni ruksa! Habari ya kuvuja ilikuwa kabla mzigo haujafunguliwa madukani, baada ya kuanza kuuzwa madukani, suala la kuvuja linakuwa limekufa automatically! Kitavujaje kitu kinachouzwa dukani! Ishakuwa old story, kanunue kama ni mdau!
 
Hiyo jezi ya Simba ilikuwa lazima ivuje tu. Haiwezekani eti wazindue kesho jioni Dar halafu muda huo huo ipatikane Tanzania nzima. Isingewezekana kuisafirisha maelfu ya kilomita mikoani bila kutokea wajanja wachache wafanye yao hapa katikati.

Ushauri wa bure kwa Vunjabei na Simba kama kweli wanataka jezi zisivuje siku zijazo basi uzinduzi ufanyike Dar na mikoani kote zipatikane baada ya masaa 24/48. Kutaka jezi zipatikane mikoani siku hiyo hiyo zinapozinduliwa Dar kibongo bongo haiwezekani kwani janja janja wengi.
 
Ukiona hivyo ujue Mkataba wa Fred ukiisha yeye ndio atakuwa anatengeneza jezi,anawaandaa kisaikolojia.
Huyu jamaa ndio maana hawezi fanya kazi na watu makini ni miyayusho sana
Bora yeye anayeuza hizo “ low quality” lakini ni Boss wa kampuni yake mwenyewe na wewe unaesubiri Salary Slip mwisho wa mwezi ndiyo uende kununua “vitu za standards” una nini cha maana kumzidi Fred[emoji3][emoji3][emoji3]
Dah mkuu wote hatuwezi kuwa wafanyabiasha wote hatuwezi kuwa matajiri jibu fact yake ni kweli anauza low quality ila anasoko lake alilolilenga mbona jibu jepesi tu
 
Dah mkuu wote hatuwezi kuwa wafanyabiasha wote hatuwezi kuwa matajiri jibu fact yake ni kweli anauza low quality ila anasoko lake alilolilenga mbona jibu jepesi tu

Hapa point yangu ni yeye kuheshimu kazi za wengine,siyo kuleta madharau,hiyo Low quality yeye kaijuaje? Maana anaongea utadhani yeye ananunua kwa designers moja kwa moja Paris,NW au Italy.Kumbe na yeye tunabanana hapa hapa kwenye maduka yetu yanayouza kama siyo China basi Nguo kutoka Turkey.Au ndiyo wale wakiingia kununua nguo Mr Price wanajiona wanavaa nguo ya standards ya juu.[emoji3][emoji3].
 
Akili za utopolo bana.
Kwani hizi jezi alizihifadh wapi zisivuje? Tena siku moja kabla ya kuzindua? Ina maana yeye tu duniani mwenye alikua anajua ziliko na ana funguo zake? Hana wasaidizi??

By the way Jezi ina tundu la kuingizia kichwa na mikono, itaachaje kuvuja kwenye hayo matundu?
 
Rejea tangazo la leo. Jezi zipo madukani, kununua ni ruksa! Habari ya kuvuja ilikuwa kabla mzigo haujafunguliwa madukani, baada ya kuanza kuuzwa madukani, suala la kuvuja linakuwa limekufa automatically! Kitavujaje kitu kinachouzwa dukani! Ishakuwa old story, kanunue kama ni mdau!
Naziona maduka ya manzese hapa watu wanasagula2

2911615_Screenshot_20210903-120848_Facebook.jpg
 
Back
Top Bottom