Kuna uzi wowote umeuelezea kuhusu meditation? Natamani kufanya hili jambo.
Kwanza mniwie radhi nitachanganya lugha kiingereza na kiswahili
Pili post yaweza kuwa ndefu tuvumiliane lakini nitajitahidi kuifupisha
Wanaforum tumekuwa na masomo mengi mazuri juu ya meditation hasa toka kwa Pasco Mtambuzi heshima kuu kwao na ndugu yetu Rakims
Ni masomo ambayo kwa kiasi kikubwa yaliwanufaisha wengi lakini bahati mbaya sana tulipitiwa na kudhani kuwa wote wako kwenye ile level moja nasi ya uelewa hivyo masomo mengi yakawa in deep na kiufundi zaidi bila kuelewa kuwa wasomaji wengine walihitaji kwenda nao kuanzia chini kabisa
Meditation bado ni kitu kigeni kwenye familia zetu na kwa kiasi kikubwa inahusishwa na nguvu za giza hasa kutokana na mapokeo yetu kwenye mambo kama hayo, hivyo ni vigumu mno kuwa na meditation huru uwapo nyumbani mtaani au kazini, lakini bado kukiwa na uhitaji mkubwa wa hiki kitu hasa kwa wale ambao tayari wana upeo na uelewa fulani wa meditation
Fuatana nami katika mada hii ambayo kwa njia mojawapo yaweza kukupa nafasi ya kufanya basics za meditation bila bughudha
1.Time management n discipline
Tengeneza utaratibu wa kufanya jambo moja kwa muda ule ule at least mara 5 kwa wiki! Yaani kwa mfano lazima uamke saa 12 kamili asubuhi, moja kamili lazima uwe uko njiani kwenda kazini saba kamili lunch mbili kamili dinner na saa nne kamili unapanda kitandani (huu ni mfano tu)
2.lishe na kinywaji
Hakikisha unakua na kipimo kisichobadilika kwenye chakula kuanzia asubuhi mpaka usiku, maji pekeyake ndio unaweza kunywa mengi bila kipimo maalum
chakula ni kwa ajili ya afya ya mwili na si ladha ya mdomoni hivyo usiongeze kipimo kwa ile ladha upendayo na kupunguza kipimo kwa chakula usichokipenda
3.Jambo moja kwa wakati mmoja chochote ufanyacho na muda hata wa dk tano ukipata jaribu kumakinika na kufanya breathing meditation au counting breath meditation kimya kabisa.
Kama unadrive concentrate kwenye driving kama uko kwenye usafiri wa jumuiya kaa kimya na kuwa mtulivu ukiendelea na meditation yako usihamaki kuhusu foleni nk mwachie dereva hiyo headache
Haya yaweza kuwa rahisi kuyasoma lakini practice ikawa ngumu lakini msingi wa meditation huanzia huku
Weza kuji control kwenye muda Weza kuji control kwenye lishe na Weza kuji control kwenye kufanya jambo moja kwa wakati mmoja baada ya hapo tutapeana hatua inayofuata
Jr[emoji769]