JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

Pale Entebbe aliwahi kushikilia mateka wa Israel bahati nzuri walikuja baadaye kuokolewa kwa nguvu na waisrael wenyewe; halafu bibi mmoja muIsrael alibaki Ialikuwa yupo Hospitali; dd Amini akamuua taratibu kwa kuwa anakta vipnade vya mionofu kwenye mwili wake
 
Kwenye tukio hlli kwa sasa mimim naweza kusema kuwa Viruses wanaoedelea kuisumbua Nchi hii hadi muda huu, alianza nao Mwalimu wakati wa kipindi chake ila hakuweza kuwajua na hadi sasa bado wapo wanaendelea ku-operate

Kwa utafiti wangu wa juujuu, viruses hawa wanahusika pia na matukio mengine yafuatayo”

MOSI

Mgogoro wa uhusiano kati ya Mwalimu na Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya pili. Wawili hawa walichonganishwa makusudi ili Mwalimu amchukie Waziri Mstaafu, ili baadaye Waziri Mstaafu huyo asije akawa Rais wa Nchi

PILI:


Mgogoro kati ya Rais wa awamu ya pili na Mwalimu; hawa nao vile vile walichonganishwa makusudi

TATU:

Viongozi wote mahiri waliowahi kujiuzulu wakati wa awamu ya nne kwa madai ya kukumbwa kashfa. Hawa walikuwa wanachonganishwa na mamlaka zao za uteuzi ili wasije wakaja kugombea Urais huko mbele ya safari; na orodha ni ndefu

Uhakika ni kwamba lazima yupo mtu potential ambaye hafahamiki na ambaye possibly Mwalimu aliwahi kuwa naye kwenye Serikali yake, ambaye huwa anaendesha mtandao huu
 
Mnamo February 12, 1985 Gazeti la Daily News linaripoti kuwa, Mwanamama Elizabeth Olotu anaandika historia kwa kuwa mwanamke wa kwanza kurusha ndege nchini Tanzania.

Pichani, Meneja wa Air Tanzania Corporation (ATC) wa wakati huo, Bakari Mwapachu akimbandika Cheo Afisa wa kwanza (F.O) Bi, Elizabeth Olotu baada ya kurusha ndege ya DHC-6 maarufu Twin Otter kutoka Dar es salaam kwenda Mafia na kurudi akiwa na Rubani kiongozi, Capt. Aziz Abdulla (kulia).

Bakari Mwapachu, aliyepanda kama abiria kwenye ndege hiyo alikuwa na haya ya kusema;

"Betty ametua ardhini kwa namna bora ambayo sijapata kuishuhudia kabla"

Picha:
Maktaba
 
#MAKINIKIA: HEKAYA FUPI YA TRENI YA GARI MOSHI MAARUFU INAYOENDESHWA KWA MVUKE

Injini ya mvuke ndiyo chimbuko la mapinduzi ya usafiri duniani. Kwa kupasha maji moto kwa makaa ya mawe na kuyageuza mvuke, pistoni zilisukumwa na kugeuzwa mwendo wa magurudumu.

Maboresho ya mhandisi James Watt wa Uingereza karne ya 18 yaliifanya injini hii kuwa moyo wa viwanda na reli. Kuanzia 1954, East African Railways lilileta zaidi ya vichwa 40 vya injini hizi, Tanzania ikiwa sehemu ya historia hiyo.

Maarufu zaidi ni kichwa SUK 2927XX, kilichotengenezwa Glasgow mwaka 1955. Kikiwa na uwezo wa kubeba mizigo na abiria zaidi ya tani 750, kilihudumia kwa miongo mitatu mstari wa Tanga–Moshi. Lakini kufa kwa EAR mwaka 1977 na ujio wa dizeli kulikifuta katika ramani.

Mwaka 1998, Mwingereza Mike Dean alikifufua kwa ushirikiano na TRC. Aliibadilisha kutumika mafuta mazito badala ya makaa na kukiweka katika safari za kitalii Dar es Salaam–Soga.

Wageni kutoka Uingereza, Brazil na kwingine walifurahia si safari tu, bali pia burudani za ngoma za asili zilizoandaliwa kuwakaribisha. Safari hizo ziliendelea hadi 2007.

Leo, SUK inabaki kuwa kumbukizi muhimu. Wataalamu wanaamini bado inaweza kufufuliwa tena kama kivutio cha urithi na utalii wa reli Tanzania.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…