JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

Utadhani mtakatifu fulani. Anyway, nadhani hapa alishatubu yale mambo yake.
Idi Amini na Nyerere wote walikuwa wanasiasa.
Na kwenye siasa kuna kitu kinaitwa PROPAGANDA!.
Waswahili wanasema "ukitaka kumuua mbwa mpe jina baya!"
Mimi siamini kwamba Idi Amini alikuwa na madhambi mengi kumshinda julius Nyerere.
Kila mmoja alikuwa na mazuri yake na mabaya yake!.
Kuna mengi mabaya tunayoambiwa kuwa Idi Amini alifanya lakini ukiwauliza wazee wa kiganda walioishi wakati wa utawala wa Idi Amini wanakuuliza wewe hizo habari umezitoa wapi, mbona wao hawakuwahi kumuona Amini akifanya mambo hayo?!
 
Leo mnamo Aprili 8, 1946, Shirika la ndege Ethiopian Air Lines ilifanya safari yake ya kwanza kwenda #Cairo kupitia #Asmara katika ndege yake aina ta #Douglas C-47 #Skytrain.

Shirika la Ndege lilipitia heka heka za sekta ya anga na changamoto za kipekee kwa Afrika hafi kuwa shirika kubwa zaidi la Usafiri wa Anga barani Afrika, lenye faida na lililoshinda tuzo kadhaa.

Hivi sasa Shirika hilo lina;
Ndege - 131
Vituo/Destinations - 147
Njia/Routes - 234
Miruko kila siku - 416
Makao Makuu - Addis AbabaView attachment 2587167
Shirika langu la kwanza kupanda ndege yake mwaka 2015 from Dar to Addis then Addis to Cairo.
 
Hapa kuna walakini.
Mji wa Singida hadi leo 2025 nyumba za gorofa hazijafika 10., Miaka 10 iliyopita Singida hapakuwa na jengo la ghorofa zaidi ya TRA na CRDB nadhani.
Sasa kusema miaka ya 1960 Singida kulikuwa na nyumba ya gorofa kwangu haiingii akilini.
Itakuwa mji mwingine huo!
 
Mathias alisafiri tarehe 26 Septemba 1983 kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza na basi la KAMATA na kulipa nauli shilingi 200 (angalia jina la tiketi). Mimi nilisafiri Agosti 1985 kutoka Kyela, Mbeya kwenda Dar es Salaam na basi la KAMATA na kulipa nauli shiligi 43. Hii ilikuwa ni nusu nauli, nauli kamili ilikuwa ni shilingi 86. Safari yetu kutoka Kyela ilianza saa 4 asubuhi, tulifika Dar es Salaam kesho yake saa 11 jioni. Mimi sikuhifadhi tiketi yangu, lakini niliyoiweka hapa nimeipata kwa Joel Wilson Msella.

Ili kupata shilingi 43 kwa ajili ya nauli yangu ilinibidi niuze maziwa mwezi mzima. Kila siku nilikuwa ninapeleka lita moja ya maziwa kwa mama mmoja aliyeitwa Ijeje aliyekuwa anaishi karibu na Misheni ya Roman Catholic. Nilifanya zoezi hilo mwezi mzima na mwisho wa mwezi nikalipwa pesa. Utaratibu ule ulikuwa unaitwa 'kipande'. Ilikuwa kila siku tunapeleka maziwa lakini tunachukua pesa mwisho wa mwezi.

Enzi zile ilikuwa mtoto akitaka pesa ilimlazimu kuifanyia kazi. Ilikuwa ama tuuze maziwa, au tuuze korosho. Maziwa na korosho vilikuwa ni ndani ya uwezo wetu lakini mpunga ni lazima kikaliwe kikao cha baba na mama ndio uuzwe. Kuuza maziwa kilikuwa kikao kati ya baba na mtoto ingawa mama ilikuwa lazima ajue. Lakini korosho ilikuwa ni nguvu yako kuokota.

Je, umewahi kusafiri na KAMATA, KWACHA au Railways miaka hiyo? Je, unajua kuwa serikali ndiyo iliyokuwa na makampuni ya usafiri? Je, unajua kuwa utaratibu wa watu binafsi kuanza kumiliki mabasi ulianza mwaka 1990 baada ya serikali kuacha kumiliki makampuni ya usafiri?
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?


Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 7 Mei 2023View attachment 2614329
Kule kwetu Ngara kabla ya mwaka 1990 ilikuwa tayari kuna waarabu wanamiliki mabasi ya abiria.
Kati ya makampuni ninayoyakumbuka kusafirisha abiria toka Ngara kwenda Mwanza kati ya mwaka 1985 na 1990 ni El Shargy na El Jabry ambazo zote kampuni hizi mbili zilikuwa zikimilikiwa na waarabu wenye asili ya Oman.
Ukisema watu binafsi wameanza kumiliki mabasi 1985 baada ya Mzee Rukhsa kuingia madarakani nitaelewa ila mwaka 1990 ilikuwa tayari kampuni binafsi za mabasi zipo barabarani.
 
Hapa kuna walakini.
Mji wa Singida hadi leo 2025 nyumba za gorofa hazijafika 10., Miaka 10 iliyopita Singida hapakuwa na jengo la ghorofa zaidi ya TRA na CRDB nadhani.
Sasa kusema miaka ya 1960 Singida kulikuwa na nyumba ya gorofa kwangu haiingii akilini.
Itakuwa mji mwingine huo!
OK asante nitafuatilia
 
Dah!Kwa hiyo hapo miguuni walivaa kobazi pia!?[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kobazi?! Miaka ya 1990 mwanzoni tumesoma na wanafunzi wanakuja shuleni hawana hata lapa la kuvaa mguuni yaani wanatembea peku kwenye shule ya msingi ya kata ,wewe unaulizia kobazi zama za mjerumani?! Miaka hiyo ukipata kobazi si utaitwa mtoto wa kishua ?!
 
IMG-20250704-WA0008.jpg
 
Kama kuna mtu anajua kisa hiki atuambie huyo mtu anayemsalimia mzee Mgabe ni nani na kwanini Mzee Mgabe alikataa kumpa mkono?!
IMG-20250704-WA0007.jpg
 
Pichani ni muonekano wa sasa wa muigizaji maarufu wa Namibia Leonora Jacobs aliyeigiza kwenye filamu maarufu ulimwenguni "Gods Must be Crazy" ya mwaka 1980

Wengi tulidhani ni wa kiume kumbe ni pisi😋
1752616413693.jpg
 
Back
Top Bottom