JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

X Mass ya mwaka 2021 tulienda gereza la Ukonga kumsalimia aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema taifa Mhe. Freeman Mbowe aliyekuwa anakabiliwa na kesi ya UGAIDI. Mwaka 2015 gereza lilelile mwenyekiti wetu wa sasa @TunduALissu anashikilikwa kwa kesi ya UHAINI. Siku moja tutakomesha ukatili huu.
1766643994936.jpg
 
Mwanamuziki Mkongwe, Mwinjuma Muumini akiwajibika ipasavyo stejini na kukonga nyoyo za Mashabiki wake, WAHENGA mnakumbuka nyimbo zipi za Mkongwe Muumin, ambaye bado anakomaa na fani.
1766712082980.jpg
 
Dar es salaam 1961.

Marehemu Indira Ghandi akiwa na nadhani Mama Maria Nyerere.
1766722883398.jpg
 
Zawadi Ya Leo Siku Ya Boxing Day.

TUNAMKUMBUKA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE. JE TUNAMFAHAMU MAMA YAKE
MZAZI?

UNAMJUA BIBI CHRISTINA MGAYA WA NYANG'OMBE?

Hayati Bibi Christina Mgaya wa Nyang'ombe alikuwa mke wa tano(Kati ya wake 22) wa chifu
Nyerere Burito. Hayati Bi. Mgaya ndiye mama mzazi wa baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Chifu Burito alikuwa kiongozi wa kabila la Zanaki wa Butiama wakati wa Ukoloni. Alitawala kuanzia 1912 mpaka mwaka Machi 30, 1942 alipofariki.

Inasemekana Bibi Mgaya wa Nyang'ombe alizaliwa mwaka 1897. Alijaaliwa kupata watoto sita
ambao ni Nyerere (Julius)Kambarage, Nyangete Nyerere, Nyakahu Nyerere, Nyakigi Nyerere,
Kizurira (Joseph)Nyerere na kitindamimba aliyeitwa Kiboko (Josephat) Nyerere.

Hivyo utaona mama huyu alikuwa na kazi kubwa ya malezi kwa watoto, akiwemo Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye alikuja kuwa baba wa Taifa letu. Kwa sifa zake, Inaelezwa Bibi Christina Mgaya alikuwa mtu mwenye busara kubwa na aliyependa kuongea kwa mafumbo yenye kubeba mafunzo Fulani. Hata Mwalimu Nyerere alipokuwa raisi bado bibi huyu aliendelea kushiriki shughuli za shamba na hata sherehe za utamaduni na watu
wengine hapo Butiama kabla ya umauti kumkuta mwaka 1997.

Kulingana na Mzee Peter DM Bwimbo Katika kitabu chake kinachoitwa: ‘MLINZI MKUU WA
MWALIMU NYERERE’ anaeleza kwamba Mwalimu Nyerere alimuheshimu sana mama yake, Bibi
Mgaya Nyang’ombe. Mara zote akiwepo Butiama, aliamka mapema kabla ya kufanya chochote
alienda kumsalimu. Hata kulipotokea jambo ndani ya familia, aliheshimu kauli ya mama yake
bila kujali madaraka yake kama raisi wa nchi.

Inaaminika alifariki akiwa na miaka 105( mwaka 1997) amezikwa karibu kabisa na kaburi la Chifu
Nyerere Burito. Ingawa maandiko mengine yanaeleza kuwa alizaliwa mwaka 1897 hivyo basi
kwa mwaka 1997 angekuwa na miaka 100.

Kiufupi, Bibi Christina Mgaya wa Nyang'ombe ni sehemu muhimu sana katika uandishi wa
historia ya Tanzania. Yeye ni kati ya WANAWAKE waliosahaulika kabisa katika kurasa za historia
yetu lakini ujenzi wa TAIFA hili uliitaji mtu aliyepitia malezi muhimu hasa utotoni. Ambaye
alifunzwa tangu utotoni kupenda watu, kutetea watu na kuamini katika Misingi ya HAKI naUSAWA.

Bila shaka elimu hii hakuipata kwa kumsoma KARX MARX au PLATO, ilianzia kwa mama ambaye
hakupata kabisa elimu rasmi. Ila mwenye ucheshi, mkarimu na upendo wa hali ya juu. Huyu
ndiye mama yake Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
1766769738890.jpg
 
.....Ukimcheki Mtu Kazi Aloyce Tendewa Mbele Ya Mwalimu JKN Nyuma Yake Kuna Mtu Kama Wanafanana Hivi, Wahenga Walisema Duniani Wawili Wawili
1766953618849.jpg
 
Back
Top Bottom