JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

Dar es salaam 1964

Mkufunzi wa kijeshi toka Israel akitoa mafunzo kwa askari wa miamvuli wa Tanganyika.
1766968073794.jpg
 
Nyakati zimeenda sana na hazirudi nyuma, enzi zile kulikuwa na Michezo ya Radioni, basi miongoni mwa Wahusika Wakuu wa Michezo Ile, alikuwa huyo Mzee JONGO,
1766983712688.jpg
 
Jina lake halisi ni Christina Manongi, jina la uigizaji SINTA, ni Msanii wa zamani wa Kundi la KAOLE SANAA GROUP, naye aling'ara enzi yake
1766983808250.jpg
 
Mwaka 1974, Rais wa Zaire (sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo), Mobutu Sese Seko, alifanya jambo ambalo halijawahi kusahaulika katika historia ya michezo na siasa za Afrika. Aliamua kuandaa pambano kubwa zaidi la ndondi duniani kati ya Muhammad Ali na George Foreman, lililojulikana baadaye kama “Rumble in the Jungle.”

Mobutu alikuwa kiongozi aliyependa sana sifa, nguvu na umaarufu wa kimataifa,alitaka kuonyesha dunia kuwa Afrika inaweza kuandaa tukio la kiwango cha dunia ma kujenga taswira ya Zaire kama taifa lenye nguvu, utulivu na maendeleo na kujitambulisha kama kiongozi mkuu wa Afrika katika enzi ya Vita Baridi

Alitumia fedha nyingi za serikali kuwalipa mabondia wote wawili takribani dola milioni 5 kila mmoja, kiasi kikubwa sana kwa wakati huo.Muhammad Ali alikuwa tayari bondia shujaa wa watu weusi na mpigania haki na George Foreman alikuwa bingwa mtawala, mwenye nguvu na aliyepigiwa upatu kushinda

Mobutu aliwakaribisha Kinshasa kama wafalme na kulikuwa na tamasha la muziki huku wasanii maarufu wa wakati huo James Brown na Miriam Makeba walitumbuiza kaauli mbiu maarufu mitaani kuelekea pambano hilo ilikuwa*Ali, bomaye!”ikimaanisha (Ali, muue!)

Ali alishinda mioyo ya wananchi kwa kuzungumza na watu wa kawaida, kucheza nao, na kujitambulisha kama mwana wa Afrika aliyerudi nyumbani.Tarehe 30 Oktoba 1974, pambano lilipigwa usiku wa manane ili liweze kuonyeshwa moja kwa moja MarekaniForeman alionekana mwenye nguvu zaidi lakini Ali alitumia mbinu yake maarufu ya “rope-a-dope” na raundi ya 8 ya pambano, Muhammad Ali alimwangusha Foreman na kushinda kwa knockout.
1766983999548.jpg
 
1766984112362.jpg
Mzee Said Wangamba, Jina la Kisanii, Mzee Small ni miongoni mwa Wasanii wa mwanzoni katikaTasnia ya Sanaa ya Uigizaji hapa Nchini, enzi zile wakirusha Michezo yao kupitia Chaneli ya CTN.
 
Moshi - Arusha 1975

Kumbe Wachaga toka miaka hiyo huu ndo utamaduni wao wa kwenda Moshi na Arusha kila mwisho wa mwaka kumbe wameanza kitambo huu utamaduni
1767098041077.jpg
1767098007042.jpg
 
1767099461131.jpg
Kundi la SOUKOUS STAR nalo lilifanya vizuri sana katika shughuli zao za Muziki enzi zile, tunalikumbuka vizuri bila shaka.
 
MWAMBA HUYO _____ ABEL BALTAZAL. M,BABE WA MUZIKI WA DANSI TANZANIA 🇹🇿. Ni Mcharazaji GUITAR 🎸 Mahili sana Baadhi ya Mashabiki Walimpa Jina, BWANA MIPANGO. Hii ilitokana na Juhudi zake, Alitumia Mbinu Kusuka Mipango, Kuwachukua Baadhi ya WANAMUZIKI kwenda Kwenye BAND Nyingine, ' ABEL BALTAZAL Alipotoka BAND ya KILOSA JAZZ, Mwaka (1969) Akajiunga na N U T A JAZZ akiwa Mcharazaji GUITAR 🎸 la Solo. Alipokea KIJITI Kutoka kwa WILLFRED BONIFAS Ambae aliipa Kisogo BAND NUTA JAZZ na alienda Kujiunga na BAND YA WESTEN JAZZ. '. Hapo ABEL BALTAZAL, Alionyesha Umahiri wake Ktk Kucharaza Guitar, Walirekodi Nyimbo nyingi sana Ktk Awamu Tofauti tofauti. Baadhi ya Nyimbo kama vile (1) NUTA MTOTO WA TANU. (2) MIAKA 10 YA UHURU. (3) IKIWA KAMA HUNITAKI. (4) L E O N A S E M A. (5) MSONDO WA NUTA. (6) PUNGUZA CHENGA Na nyingnezo Nyingi. '. ABEL BALTAZAL. Alifanya kazi na Wanamuziki Wengi CAPTAIN JOHN SAIMON. MAALIM GULUMO, JUMA AKIDA KIZA HOSEIN, HAMISI SAMA AHMED OMAR, ABDALA OMAR DULA MABRUKI MOHAMED ONDONDO. MNENGE RAMADHAN, JUMA TOWN, JOSEPH LUSUNGU, Baadae mwaka (1973. Walijiunga BITCHUKA kutoka Band ya Arusha, na SAID MABELA yeye Alikuja akiwa kama MPULIZAJI wa TRUMPERT, lakini Aliwashangaza alipocharaza Guitar 🎸 la Hatari, Ktk Wimbo: DADA HERUNA. Baada ya hapo, Hawa WABABE Wawili Walipishana Guitar 🎸 la Solo Ktk Nyimbo Tofauti. ' ____ABEL BALTAZAL __ (1977) walipoingia tu Kuwa JUWATA JAZZ BAND, Walirekodi Albamu yenye Nyimbo: KAKA SELEMAN Nk. Ndipo yeye AKAJIENGUA, Akaondoka _. Akaenda Kufanya MIPANGO Kuwakusanya Wanamuziki ili kwenda kuanzisha BAND MPYA. ABEL BALTAZAL Alipewa Kazi Na Rafiki Anaitwa ZAKALIA NDAMAMEE, Alete Wanamuziki. Ndipo ABEL, Akaenda Ushirika, TANZANIA STARS,,,,,,,, Aliwachukuwa Wanamuziki (4) JOSEPH MULENGA,,,,, ABDALLA GAMA,,,,,, HALUNA LUWALI Na GEORGE KESSY. '. Baada ya Hapo, ABEL BALTAZAL Alienda DAR JAZZ, Akafanya MIPANGO yake, Akam ng'oa KING MICHAEL ENOCK,, Ambae Ndie Alikuwa mpiga Solo Guitar 🎸 Tegemezi Takribani kwa Miaka (17) '. Alijiunga DAR ES SALAM JAZZ (1960) Lakini (1977) Alikubali Ombi la ABEL BALTAZAL, Wakaondoka wakaenda kwa ZAKARIA NDAMAMEE na Wakaanzisha BAND mpya DAR INTERNATIONAL, Mkusanyiko wa Wanamuziki kutoka BAND tofauti, Baadhi Walitoka SAFARI TRIPPERS, Palikuwa na KASSIM MPONDA,,,,,,,,MARIJANI RAJABU,,,,,,,,BENI PETII,,,,,,,,,,,, ALLY RAJABU MSHANGAMA,,,,,,, _ JOSEPH BERNARD,,,,,,, hicho kikosi kutoka SAFARI TRIPPERS. Na COSMAS CHIDUMULE Yeye nae aliungana na Wenzake alitokea Kwenye BAND ya URAFIKI JAZZ. - Wanamuziki Waliendelea Kuongezeka Baadae ilipofika March 1978 Walirekodi ALBAMU ambayo yenye Nyimbo (6) NYERERE,,,,,,, RUFAA YA KIFO,,,, _MWANA RUDI UOWE,,,,,,, MAGRETH,,,,,,,, SIKITIKO,,,,,,, BETI,,,,,,,, Huu Wimbo BETI ABEL BALTAZAL Amechalaza Solo Guitar 🎸 ila hizo nyingine Solo Guitar Limechalazwa Na KASSIM MPONDA. Waimbaji: MARIJAN RAJABU,,,,,, COSMAS,,,, _BELESA KAKELE,,,,,,ALLY RAJABU MSHANGAMA. _ Sec, Solo OMAR MAKUKA. _Bess Guitar JOSEPH MULENGA,
Rythim: ABDALLA GAMA,,,,,,,,,,BENI PETII 'DRAMS: SAID MOHAMED. Trumpert : MACHAKU SALUM,,,,,,, IBRAHIM MWINCHANDE. Saxphone : KING MICHAEL ENOCK 🎷. JOSEPH BERNARD,,,,,,,,,,, Tumba : HALUNA LUWALI. Kinanda: GEORGE KESSY. '. _ Baadae Ulitokea Mtafaruku, Hapo ndipo MARIJANI RAJABU Alijiengua Akaachana na MUSIC akarudi Nyumbani kupumzika. _ lakini kama Kawaida yake ABEL BALTAZA Alifanya MIPANGO Akaondoka na GROUP la Wanamuziki (10) Akawapeleka kwenda Kuanzisha . BAND YA MLIMANI PARK. . ABEL BALTAZAL Alienda JUWATA JAZZ: Akampa Dili MAALIM GULUMO kwamba Amfuate ili Waende MILIMANI PARK, Wakafanye Kazi Pamoja . MAALIM GULUMO Alikubali, Kisha Akafuatwa HAMISI JUMA, ( Maalim Kinyasi ) Kutoka Biashara jazz, . Na Tukumbuke Hapo T-CHIMANGA ASOSSA Alikuwepo, . Na yeye Ndie Mtunzi wa Wimbo, GAMA NISAMEHE: Lakini kabla Hawajarecord T-CHIMANGA ASOSSA Alipata Dharula, Akarudi Nyumbani kwao CONGO 🇨🇩. '. ABEL BALTAZAL na Wanamuziki wenzake Akaenda Kurecod Albamu ilikuwa na Nyimbo (6). MAUDHI,,,,,,,,,, NYERERE,,,,,,,,,,, KASSIM No: 1 Hizo Nyimbo (3) Zote Solo Guita 🎸 Amechalaza. ABEL BALTAZAL. ''. Bess: JOSEPH MULENGA. 'Rythim : ABDALLA GAMA. Drums: HABIBU JEFF MGALUSI. Trumpert: MACHAKU SALUM,,,,,,,,, IBRAHIM MWINCHANDE. Saxphone🎷 KING MICHAEL ENOCK. 'Tumba: HALUNA LUWALI. Kinanda : GEORGE KESSY. Waimbaji: (3) MAALIM GULUMO,,,,,, COSMAS CHIDUMULE, HAMISI JUMA, (Maalim Kinyasi). '. Wimbo. SELINA,,,,,,,,, WEEKEND,,,,,,,,BARUA No :1 Hapo JOSEPH MULENGA Amechalaza Solo Guita 🎸 ABEL BALTAZAL Amecharaza BESS Guitar '. Mwaka (1979) Walikuja Wanamuziki wa (4 " BITCHUKA,,,,,,,,,,,,,,,, MWANYIRO,,,,,,,JUMA TOWN,,,,,,,,,,, ABDALLA OMAR DULA, . (1982) 1983 Waliingia Wanamuziki Wengi sana, Kuanzia Waimbaji mpaka Wapiga Guitar 🎸. Kuna Baadhi ya Nyimbo kama WIVU, TANGAZIA MATAIFA Hapo Solo Guitar Amecharaza ABEL BALTAZAL. '. Lakini Baadae (1984) Baadhi ya Wanamuziki wa (4) Walijiengua Walienda BIMA LEE JOSEPH MULENGA. ABDALA GAMA. SELEMAN MWANYIRO. SHABANI DEDE. Lakini tukumbuke kuwa. ABEL BALTAZAL nae Alienda BIMA LEE lakini haikuchukuwa muda Akarudi. '. Hapo sasa Alifanya MIPANGO Aliwachukuwa Baadhi ya Wanamuziki kutoka Mlimani park wana SIKINDE. . Wakaenda SAFARI SOUND kuanzisha MTINDO WA NDEKULE. . Akiwemo MAALIM GULUMO. HASSAN REHANI BITCHUKA. KASSIM RASHIDI KIZUNGA. CHARZ JOHN NGOSHA. ALLY MAKUNGURU. IBRAHIM MWINCHANDE. '. (1985). Walirekodi Nyimbo nyingi ikiwemo CHATU MKALI. HOMA IMENIZIDIA. Hapo Solo Guitar 🎸 ABEL BALTAZAL. '. Lakini hakuishia hapo, japokuwa BAND ilizidi kufanya kufanya vizuri, na baadhi ya Wanamuziki waliongezeka kwa Nyakati tofauti tofauti Baadae BENOVILLA Alikuja na mtindo POWER ILANDA. '. Walirekodi baadhi ya Nyimbo, Zikiwemo. MVUVI KINDA. KULALA SEBULENI. Baadhi ya wanamuziki Akiwemo. TOTO TUNDU. MUSEMBA WA MINYUGU. HASSAN KUNYATA SHIBANDA SONY. Na wengineo wengi. '. Tukumbuke kuwa Baadae ABEL BALTAZAL Alichukua Baadhi ya Wanamuziki Akaondoka nao Kwenye BAND YA MAGEREZA Hapo ndipo wakaanzisha MTINDO. ___________M K O T E N G O M A_ '. Je! Wewe Unakumbuka Wimbo Gani Guitar 🎸 la ABEL BALTAZAL ❓❓
FB_IMG_1767405412382.jpg
 
Lupelo Investments enzi zake, DAR, IRINGA- NJOMBE Miaka ya 1990s. Kampuni hii inakumbukwa sana kwa rekodi yake nzuri.
1767724658603.jpg
 
Huyu
1768128612441.jpg
ni TUMBA AYILA aka EMORO bila shaka tunamkumbuka vizuri, alikuwa dancer wa Bendi ya Empire Bakuba iliyokuwa chini ya Uongozi wa Pepe Kalle, MWENYEZI MUNGU aendelee kumpa Pumziko la Milele.
 
Back
Top Bottom