JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

1768527945444.jpg
 
1768528476001.jpg
Huyo ni Full back Left wa zamani wa SIGARA, SIMBA SC NA AFC - ARUSHA, Mkongwe Aziz Nyoni Njalambaya, sijui mnamkumbuka?
 
WAHENGA - WACHEZAJI WA ZAMANI WA YANGA, MBUNGA, CHINA, SURE BOY NA EDGAR FONGO.
1768529424357.jpg
 
NAWAKUMBUSHA TU

1. Karudi baba mmoja,
toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja,
na kutetemeka mwili,
Watoto wake wakaja,
ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli iwafae maishani.

2. Akatamka mgonjwa,
ninaumwa kwelikweli,
Hata kama nikichanjwa,
haitoki homa kali,
Roho naona yachinjwa,
kifo kimenikabili,
Semeni niseme nini,
kiwafae maishani.

3. Yakawatoka kinywani,
maneno yenye akili,
Baba yetu wa thamani,
sisi tunataka mali,
Urithi tunatamani,
mali yetu ya halali,
Sema iko wapi mali,
itufae maishani

4. Baba aliye kufani,
akajibu lile swali,
Ninakufa maskini,
baba yenu sina hali,
Neno moja lishikeni,
kama mnataka mali,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

5. Wakazidi kumchimba,
baba mwenye homa kali,
Baba yetu watufumba,
hatujui fumbo hili,
akili zetu nyembamba,
hazijajua methali,
Kama tunataka mali,
tutapataje shambani?

6. Kwanza shirikianeni,
nawapa hiyo kauli,
Fanyeni kazi shambani,
mwisho mtapata mali,
haya sasa buriani,
kifo kimeniwasili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

7. Alipokwisha kutaja,
fumbo hili la akili,
Mauti nayo yakaja,
roho ikaacha mwili,
Na watoto kwa umoja,
wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

8. Fumbo wakatafakari,
watoto wale wawili,
wakakata na shauri,
baada ya siku mbili,
wote wakawa tayari,
pori nene kukabili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

9. Wakazipanda shambani,
mbegu nyingi mbalimbali,
tangu zile za mibuni,
hadi zitupazo wali,
na mvua ikaja chini,
wakaona na dalili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

10. Shamba wakapalilia,
bila kupata ajali,
Mavuno yakawajia,
wakafaidi ugali,
Wote wakashangilia,
wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

11. Wakanunua na ng'ombe,
majike kwa mafahali,
wakapata na vikombe,
mashine na baiskeli,
Hawakuitaka pombe,
sababu pombe si mali,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

12. Wakaongeza mazao,
na nyumba za matofali,
Pale penye shamba lao,
wakaihubiri mali,
Wakakiweka kibao,
wakaandika kauli...

"KAMA MNATAKA MALI
MTAIPATA SHAMBANI".
🚶🚶
1768529584261.jpg
 
Maisha ya Faraghani ya Debbie Rowe, Mke wa Zamani wa Michael Jackson

Debbie Rowe, mke wa zamani wa marehemu Michael Jackson, ameendelea kuishi maisha ya faraghani tangu talaka yao iliyojaa gumzo zaidi ya miaka 20 iliyopita. Muonekano wake wa nadra hadharani Aprili mwaka jana ulimshangaza wengi, miaka tisa baada ya kupambana na saratani ya matiti.

Rowe, mwenye umri wa miaka 67, ni mama wa Paris (27) na Prince (28), watoto wanaodaiwa kuwa wa Michael Jackson. Mtoto wa tatu wa Jackson, Bigi (23), alizaliwa kupitia mama mbadala, huku utambulisho wa mama yake ukiwa haujulikani. Hata hivyo, kwa miaka mingi kumekuwapo na uvumi kuhusu uhalisia wa Michael Jackson kuwa baba wa kibaolojia wa watoto hao.

Debbie Rowe amewahi kusema kuwa alipandikizwa mimba kwa njia ya kitaalamu kwa kutumia mbegu za Michael Jackson. Licha ya hilo, Paris Jackson amekiri kumchukulia mama yake kama rafiki zaidi, akisema alikulia chini ya malezi ya baba yake baada ya talaka ya wazazi wake.
1768529917158.jpg
 
1768530085116.jpg
ENZI YA KIDEDEA HIYO (MUCHACHO GROUP) nyakati zimeenda sana, walikuwa wako vizuri sana katika kuishangilia SIMBA SPORTS CLUB, mwanzo, mwisho "Nanukuu" Wimbo wao Maarufu, hakuna hakuna, hakuna lolote hapo Simba inashambuliwa, SIMBA SC ikishambulia utawasikia Tunataka GOLI, tunataka Goli SIMBA, tunataka GOLI tunataka GOLI Simba, Simba iyoo, iyoo, kosa kosa mara Malota imooo halafu kuna ile Kona goliii, Kona goliiii, Kona goliii, enzi ya Kocha Dragan Popadic yalifungwa sana magoli ya Kona, kabla sijamaliza WAHENGA tukumbushane, hiyo ilikuwa mechi dhidi ya Timu gani? kwa mbaaaali naona Jamaa kavaa lubega, Kanga ya Ubingwa, ilikuwa Mechi kubwa hiyo bila shaka, hahaha 😁.
 
huyo ni OLIVER N'GOMA, alizaliwa Tarehe 23 March 1959 katika Mji wa Mayumba, kusini - Magharibi mwa GABON na kufariki DUNIA June 7 2010, katika Hospitali ya OMAR BONGO Mjini, Libreville, baada ya Figo kushindwa kufanya kazi. Oliver N'goma alikuwa akipiga Muziki wake kwa kutumia Mitindo ya Zouk na Soukouss, Oliver N'goma kama walivyo Wanamuziki wengi wengi naye ni Versatile Musician, Alikuwa anaimba, Anadansi, Mtunzi na pia ni Mpiga gitaa mzuri tu, Nyimbo zilizomtambulisha zaidi kwenye Tasnia ya Muziki ni Bane, Icole, Adia, Lusa na nyinginezo.
1768531157905.jpg
1768531154121.jpg
 
Huyu ni Mwanamuziki Mkongwe BOZI BOZIANA alifanya vizuri katika kazi ya Muziki wa Kikongo
1768531685472.jpg
 
UKWELI KUHUSU NOTI YA SHILINGI 1000 'BUKU'
Mwaka 1990 Wakati Noti Hii Ya Shilingi 1000 Inatoka Kwa Mara Ya Kwanza Na Kuanza Kutumika Mtaani, Ilikuwa Na Msisimko Sana Kwenye Muonekano Wake .

Kwanza Kabisa Ilikuwa Ni Noti Ya Kwanza 'Kubwa' Kwa Umbile Lake Ambapo Mpaka Leo Tanzania Haijachapisha Tena Noti Kubwa Zaidi Ki Umbo Kuizidi Noti Hii Ya Shilingi 1000.

Lakini Pili, Kutokana Na Rangi Zake Wengi Waliifananisha Na Noti Ya Dola Ya Kimarekani Kwa Muonekano Wake. Kwa Sababu Hiyo Watu Waliamua Kuipa Jina La Utani Na Kuiita Buck.

KWA NINI BUCK?

Buck Ni Moja Ya Majina Ya Utani Yanayotumika Kwenye Noti Ya Dola Nchini Marekani, Hivyo Kutokana Na Noti Hii Ya Shilingi 1000 Kufanana Na Dola Ya Marekani Kimuonekano, Hivyo Tukaamua Kuiita Noti Hii Buck Tukiifananisha Na Dola Ya Marekani.

Sasa Wakati Jina Hilo Likishika Kasi Ya Matumizi Mtaani, Mara Ghafla Jina La Buck Likabadilika Na Kuwa 'BUKU', Yaani Maana Yake Ni Kwamba Badala Ya Kulitamka Jina Hilo Kwa English Buck, Sisi Tukaaanza Kuliita Kwa Kiswahili Chetu 'Buku'.

Hiyo Ndiyo Sababu Mpaka Leo Shilingi 1000 Inaitwa Buku, Hii Ni Moja Kati Ya Noti Bora Kabisa Kuwahi Kuchapishwa Tanzania Hasa Kwenye Ubora Na Muonekano, Tutaikumbuka Daima!

1768551064525.jpg
 
Back
Top Bottom