JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

1768572350892.jpg
 
A coal miner in his home, a company house in Pursglove, West Virginia, 1938.
1768582261772.jpg
 
1768610900690.jpg
Huyo ni AIME BUANGA, Ni Member wa zamani wa WENGE MUSICA BCBG (BON CHIC BON GENERATION).
 
1769307883541.jpg
Huyo kule CONGO (DRC) walikuwa wakimwita Michael Jackson wa CONGO, Beevans Ghato, kwa sasa yuko zake MAREKANI akiimba nyimbo za kusifu na kuabudu, pia alifanya vizuri katika Ulimwengu wa Muziki wa Kidunia, Je! unakumbuka nyimbo zipi za BEEVANS GHATO?
 

#MAKINIKIA: HEKAYA FUPI YA TRENI YA GARI MOSHI MAARUFU INAYOENDESHWA KWA MVUKE

Injini ya mvuke ndiyo chimbuko la mapinduzi ya usafiri duniani. Kwa kupasha maji moto kwa makaa ya mawe na kuyageuza mvuke, pistoni zilisukumwa na kugeuzwa mwendo wa magurudumu.

Maboresho ya mhandisi James Watt wa Uingereza karne ya 18 yaliifanya injini hii kuwa moyo wa viwanda na reli. Kuanzia 1954, East African Railways lilileta zaidi ya vichwa 40 vya injini hizi, Tanzania ikiwa sehemu ya historia hiyo.

Maarufu zaidi ni kichwa SUK 2927XX, kilichotengenezwa Glasgow mwaka 1955. Kikiwa na uwezo wa kubeba mizigo na abiria zaidi ya tani 750, kilihudumia kwa miongo mitatu mstari wa Tanga–Moshi. Lakini kufa kwa EAR mwaka 1977 na ujio wa dizeli kulikifuta katika ramani.

Mwaka 1998, Mwingereza Mike Dean alikifufua kwa ushirikiano na TRC. Aliibadilisha kutumika mafuta mazito badala ya makaa na kukiweka katika safari za kitalii Dar es Salaam–Soga.

Wageni kutoka Uingereza, Brazil na kwingine walifurahia si safari tu, bali pia burudani za ngoma za asili zilizoandaliwa kuwakaribisha. Safari hizo ziliendelea hadi 2007.

Leo, SUK inabaki kuwa kumbukizi muhimu. Wataalamu wanaamini bado inaweza kufufuliwa tena kama kivutio cha urithi na utalii wa reli Tanzania.

Hatuna utamaduni wa vitu vya kale visivyohusiana na viongozi wa CCM, Mv Liemba imetushinda japo ina historia ya kusisimua.
 
Back
Top Bottom