JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

IMG-20260821-WA0074.jpg
 
Tukiwa Kidato cha Sita katika Sekondari ya Azania mwaka 1993 katika Mabweni ya Azania. Anayeandika ni Ibrahimu Makana. Anayekula kando yangu ni Juma Seifu Hamsini. Nilivaa la michirizi ya pundamilia na mokasini (skuna) au viatu vyeupe chini. Juma alikuwa Mkurugenzi (DED) wa Jiji la Arusha kabla ya kuhamishiwa Tanga hivi karibuni. Sijajua Makana na wengine wako wapi kwa sasa. Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 1 Oktoba 2024
1793364119836.jpg
 
Hamissi Thobias GAGA-(Gagarino)
Simba na yanga mwaka 1990,mechi ya ligi,huyu mwamba wa kuitwa Hamissi Gaga

Wakti yupo unyamani Simba sc,.ilitokea penati Kwa ubazi wa yanga sc,mchezaji wa yanga alizani refa kapuliza firimbi,.kumbe ni mashabiki nje ya uwanja,mpigaji ni Hamissi Gaga

Wakti ameweka mpira katika duara la kupiggia penati,

Mwamba akarudi nyuma filimbi ilipo pulizwa,,Gaga bila ajizi alienda kupiga penati

Kipa wa yanga Steven Nemesi aliuzwa vizuri tu golini,.lkn kilichotkea mpira ukala nguzo ya chini katika goli, mpira uakrudi uwanjani,

Thoma kipese alikuwa peke yake hajakabwa na mtu,

Akauwahi mpira na kugeuka kwenda langoni Kwa Simba na kutia chuma....

Sitasaahau Ile Assist ya mpira kula nguzo ya ya goli,..R.I.P GAGA ThobiasView attachment 3530308
Mwamba alikua anajua mpira na mpira ulikua unamjua. R. I. P Gagarino
 
FB_IMG_1792495154553.jpg
FB_IMG_1792495158842.jpg
FB_IMG_1792495166971.jpg

Idd amini akiogelea kwenye swimming pool alipokuwa ziarani Adis ababa Ethiopia katikati ya miaka ya 1970s
 
View attachment 3530321 ENZI YA KIDEDEA HIYO (MUCHACHO GROUP) nyakati zimeenda sana, walikuwa wako vizuri sana katika kuishangilia SIMBA SPORTS CLUB, mwanzo, mwisho "Nanukuu" Wimbo wao Maarufu, hakuna hakuna, hakuna lolote hapo Simba inashambuliwa, SIMBA SC ikishambulia utawasikia Tunataka GOLI, tunataka Goli SIMBA, tunataka GOLI tunataka GOLI Simba, Simba iyoo, iyoo, kosa kosa mara Malota imooo halafu kuna ile Kona goliii, Kona goliiii, Kona goliii, enzi ya Kocha Dragan Popadic yalifungwa sana magoli ya Kona, kabla sijamaliza WAHENGA tukumbushane, hiyo ilikuwa mechi dhidi ya Timu gani? kwa mbaaaali naona Jamaa kavaa lubega, Kanga ya Ubingwa, ilikuwa Mechi kubwa hiyo bila shaka, hahaha 😁.
Hii ilikua mechi na Stella Abidjan 1993 katika fainali ya kombe la Abiola ( siku hizi Shirikisho Barani Afrika) pale shamba la bibi

Simba walikua wamesha chapisha kanga na skafu za ubingwa(Simba Bingwa) na kabda ya mechi pia ilitangazwa njia ambazo msafara wa timu utakapopita na kombe

Jean Boli Zozo akatuharibia shughuli hasa pale dakika ya 70 alipofunga goli la pili kwa shuti kali akiwa ametoka kumlamba chenga za maudhi beki wa kulia wa Simba, Rashid Abdallah. Kipa Mohamed Mwameja wala hakujisumbua kuruka maana alishtukia tu nyavu zikitikisika

Siku hiyo waliokua viongozi wa kitaifa wote walikuwepo uwanjani ikiwemo Rais Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu na Makamu wa Rais John Samwel Malecela na wengine kibao

Kiingilio cha juu siku hiyo uwanjani kilikua shilingi 50,000.0. Kwa mwaka 1993 ilikua ni pesa nyingi sana. Unanunua kiwanja Boko au Bunju
 
Back
Top Bottom