JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

Tukiwa Kidato cha Sita katika Sekondari ya Azania mwaka 1993 katika Mabweni ya Azania. Anayeandika ni Ibrahimu Makana. Anayekula kando yangu ni Juma Seifu Hamsini. Nilivaa la michirizi ya pundamilia na mokasini (skuna) au viatu vyeupe chini. Juma alikuwa Mkurugenzi (DED) wa Jiji la Arusha kabla ya kuhamishiwa Tanga hivi karibuni. Sijajua Makana na wengine wako wapi kwa sasa. Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 1 Oktoba 2024
 
Mwamba alikua anajua mpira na mpira ulikua unamjua. R. I. P Gagarino
 

Idd amini akiogelea kwenye swimming pool alipokuwa ziarani Adis ababa Ethiopia katikati ya miaka ya 1970s
 
Hii ilikua mechi na Stella Abidjan 1993 katika fainali ya kombe la Abiola ( siku hizi Shirikisho Barani Afrika) pale shamba la bibi

Simba walikua wamesha chapisha kanga na skafu za ubingwa(Simba Bingwa) na kabda ya mechi pia ilitangazwa njia ambazo msafara wa timu utakapopita na kombe

Jean Boli Zozo akatuharibia shughuli hasa pale dakika ya 70 alipofunga goli la pili kwa shuti kali akiwa ametoka kumlamba chenga za maudhi beki wa kulia wa Simba, Rashid Abdallah. Kipa Mohamed Mwameja wala hakujisumbua kuruka maana alishtukia tu nyavu zikitikisika

Siku hiyo waliokua viongozi wa kitaifa wote walikuwepo uwanjani ikiwemo Rais Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu na Makamu wa Rais John Samwel Malecela na wengine kibao

Kiingilio cha juu siku hiyo uwanjani kilikua shilingi 50,000.0. Kwa mwaka 1993 ilikua ni pesa nyingi sana. Unanunua kiwanja Boko au Bunju
 
Kiingilio cha juu siku hiyo uwanjani kilikua shilingi 50,000.0. Kwa mwaka 1993 ilikua ni pesa nyingi sana. Unanunua kiwanja Boko au Bunju
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…