Thomas Sankara alikuwa kiongozi na akiwa na miaka 33 tu, Lakini mwenye maono makubwa na siasa za mrengo wa kushoto, anatambulika sana kama "Che of Africa"-‘Che wa Afrika’ akifananishwa na Ernesto Guevara ambaye alikuwa mwanamapinduzi huko Amerika Kusini. Thomas Isidore Noel Sankara alizaliwa Desemba 21 mwaka 1949 nchini Burkina Faso iliyotambulika Kama Upper Volta kwa wakati huo.”
Wakati wa mafunzo ya kijeshi alikutana na kapteni Blaise Compaoré wakawa marafiki wakubwa. Thomas Sankara alipanda ngazi za kijeshi hadi cheo cha Captain pamoja na rafiki yake Blaise Compaore.
View attachment 1531512
Blaise Compaore kushoto na Thomas Sankara kulia
Mwaka 1981 alikuwa waziri wa mambo ya ndani katika serikali ya kijeshi ya Rais Major Jean Baptiste. na baadaye aliteuliwa kuwa waziri mkuu kwa kipindi cha kuanzia Mwezi Januari 1983 mpaka mwezi Mei alipokamatwa na kutiwa mbaroni na serikali ya Rais Major Jean Baptiste kutokana na msimamo wake juu ya ukombozi kwa watu wote wa Volta na kupendelea Marxist Revolution theories.
Mnamo august 1983, vijana wawili marafiki haswa pia makapteni wa jeshi na wanamapinduzi Thomas Sankara na Blaise Compaore walipindua serikali ya rais wa wakati huo wakisaidiwa na serikali ya Ghaddafi na Sankara kuwa Rais wa TANO wa VOLTA YA JUU au BURKINA FASO kwa sasa.
View attachment 1531515
Kutoka kushoto Blaise Compaore, Thomas Sankara na Jean Babtiste siku Sankara alipotawazwa kuwa rais baada ya mapinduzi august 4,1983.
Vijana hawa wakiwa katika fikra za kimax wakiwa na ndoto nyingi za kuijenga upper volta, walibadili kabisa historia ya taifa hilo, walibadili jina la nchi na kuitwa Burkina Faso(country of honorable citizen), Sankara akawa anatumia baiskeli kutembelea vijijini kuhimiza maendeleo wakiwa na pacha wake Compaore wakiwa kama pete na kidole.
Urafiki wa makapteni hawa wa kijeshi ulikuwa mkubwa kiasi ambacho wakati wanausalama walipomwambia Sankara kuwa Compaore ana mpango wa kumpindua na kumuua yeye aliwajibu kuwa Compaore asingeweza kufanya hivyo, Labda mtu mwingine. Akaongeza kuwa hata kama Compaore angetaka kufanya hayo, hakuna wa kumzuia. Ni wazi kuwa Sankara alikuwa karibu mno na Compaore,kwa kiasi kuwa Compaore alikuwa sehemu ya maisha ya kila siku ya Sankara
kama ilivyoambiwa na wanausalama, Compaore aliongoza mapinduzi yaliyosababisha kifo cha rafiki yake sankara mwaka 1987 October 5, na yeye mwenyewe huku akishuhudia na kushiriki mauaji na mapinduzi ya rafiki yake "kipenzi" Sankara katika mapigano ya usaliti yaliyotokea Mjini Ouagadougou Sankara akiwa katika kikao cha utendaji wa kazi, Akawa ndo rais mpya wa sita wa Bukinafaso.
“While Revolutionaries as individuals can be murdered, you cannot kill Ideas”, Haya yalikuwa ni maneno ya Thomas Sankara aliyoyatamka wiki moja kabla ya kuuawa."
Compaore, Alipata kusema katika shirika la kutetea haki za Binadamu duniani kwamba “kifo cha Thomasi Sankara ni ajali tu kama ajali zingine.
Miaka 27 baadae mwezi june 2014 chama tawala CDP kilitangaza kushinikiza mabadiliko ya katiba kuruhusu Rais Compaore kugombea tena kwa awamu nyingine kwenye uchaguzi wa mwaka 2015.
October 30 bunge likakutana kufanya mabadiliko ya katiba, Jambo hili liliamsha hisia chungu dhidi ya utawala wa Compaore, jambo lilisababisha ghasia kubwa ndani na nje ya majengo la Bunge jijini Ouagadougou
Wakati ghasia hizi zikiendelea zilizojulikana kama (Burkina faso's Black Spring) Rais Compaore akatangaza hali ya tahadhari akaghairisha kikao hicho cha bunge na kuvunja Serikali huku akiahidi kushughulikia malalamiko ya waandamanaji.
Baadae jioni ya siku hiyo hiyo jeshi kupitia kwa General Honore Traore lilitangaza kuundwa kwa serikali ya mpito na kuahidi kurejeshwa kwa utawala wa kiraia na kidemokrasia ndani ya mwaka mmoja.Hii ilionekana kama mapinduzi ya kijeshi dhidi ya utawala wa Rais Compaore.
October 31 mwezi ule ule aliyompindua na kumua rafiki yake "kipenzi" miaka 27 iliyopita Rais Compaore akatangaza kujiuzulu na kutokomea ukimbizini Ivory Coast kwa rafiki yake Rais Alasane Outtara wa Ivory Coast.Hii ilionekana kama kisasi na malipo kwa yale aliyomfanyia rafiki yake miaka 27 iliyopita.
Hii ilihitimisha miaka 27 ya utawala wa Rais na pacha msaliti wa Rais Thomas Sankara.
View attachment 1531511
Kaburi la mwanamapinduzi halisi wa Africa na Burkina faso Captain Thomas Isdore Sankara
Credit:Vyanzo mbalimbali vya habari duniani, jf(mkuu paploman)
Tusameheane kwa makosa yoyote yatakayokuwa yamejitokeza kwenye muhtasari huu wa maisha, nyakati, kifo na baada ya maisha ya Mwanamapinduzi Rais Thomas Isdore Sankara
Makosa hayo yanaweza kutokana na uchache wa Elimu yangu na udhaifu wa kawaida wa kibinaadamu.
Cc. Dr.
Saint Anne