Nichutame kwa kosa lipi?
Seriously? Ndugai awe na form zinazoonyesha ushiriki wa Mbowe katika njama hiyo halafu atazificha kwa sababu itajulikana kuwa alihusika katika mpango mzima! Tangu lini Ndugai amejali kuhusu public opinion? And worse, mnadhani Mbowe au mtu wake mwingine ni stupid kiasi ya kusaini form ambazo anajua zinaweza kutumika kumchafua?
Legitimacy inapatikana kwa uwepo wa wale wabunge na sio form. Walitakiwa wabunge kutoka Chadema ambao watakubali kuapishwa hata bila kuwa na form. Na ndivyo ilivyokuwa. Wakina Halima wameendelea kuwa wabunge bila kuonekana form au mtoto wa form.
Asiyekubali kushindwa si mshindani. Mimi naheshimu uamuzi wa waliompigia kura Lissu lakini bado naamini kuwa hafai kuwa Mwenyekiti. Muda ndio utakaoonyesha kama niko sahihi au waliompigia kura walipatia.
Aidha, sisi tulichokataa ni mpango wenu wa kutaka mgombea wenu apewe Uenyekiti kwenye kisahani. Tulisema ashindane badala ya kutaka Mbowe amuachie nafasi. Kashindana na kashinda. Tofauti na mlivyotaka kushindana kwake kumempa yeye na chama chake credibility na legitimacy. Hata Lema amekiri hilo.
Naelewa sana ninachosema. Hakuna mpinzani wake dhati anaweza kuhamia kwa mtesinwake sababu tu anaona kuwa anaonewa kwa kunyimwa nafasi ambayo anaamini aliandikiwa kuwa yake. Wapinzani wa dhati walihamia vyama vingine au walikaa pembeni. Hao unaowatetea, sio tuu walihamia upande wa waliokuwa wanawatesa bali walijiungq nao katika kukibomoa chama chao cha awali. Hao ni watu wetu wenye sense of entitlement na uhusiano ambao ni transactional.
Mimi mpaka sasa hivi huo usaliti wa wakina Halima hata siuoni. Hawa mnaowachukiq hata siku moja hawajakitukana au kukichafua chama chao cha awali kama ambavyo wengi wamefanya. Hawajasaliti principle za chama chao. Na inawezekana na wao walifanya hivyo baada ya frustration na chama chao lakini tofauti na wakina Msigwa waliendelea kukiheshimu.
Kwani nani amesema wasiombe msamaha? Ninachopinga mimi ni kuweka masharti ya kijinga ya kuwataka kukiri na kuwataja waliohusika katika huo mnaouita usaliti. Naona attitude hiyo ni insulting kwa kuamini kuwa wanawake kama Halima hawawezi kufanya uamuzi bila kushirikisha mwanaume.
Aidan alikaidi agizo la chama chake kuwa haitakuwa na mbunge bungeni kwa sababu hawqutambui uchaguzi mzima. Ni sababu hiyo hiyo iliyowafanya wasipeleke majina ya wabunge wa viti maalum.
Aidan, ni perseverence ndio pengine imewafanya watu waamue asifukuzwe na hapa mwishoni kumkumbatia.
Kwa taarifa yako niliamua kutojibu chochote utakachoweka humu kwa sababu sikubaliani na lugha unazotumia. Nimeijibu hii kwa sababu tumekuwa pamoja humu ndani kwa muda mrefu.
Aidha, katika muda wote huo haukuwahi kutumia maneno ya shombo hata pale tulipotofautiana. Isingekuwa hivyo ningekuweka katika ignore list yangu. Na nikihisi tu kuwa unachotaka ni kubishana tuu na sio kubadilishana mawezo nitakuweka kwenye hiyo list. Umeanza kunichosha.
Amandla...