Jibu la Halima Mdee kuhusiana na msimamo wa Lissu juu ya Wabunge 19 (COVID 19)

Jibu la Halima Mdee kuhusiana na msimamo wa Lissu juu ya Wabunge 19 (COVID 19)

Na mimi hapa ndio sikuelewi Fundi Mchundo! Kwa kawaida mstaarabu akivuliwa nguo huchutama!
Nichutame kwa kosa lipi?
Thubutu, Ndugai ilibidi azifiche kwa sababu ama alijua au alishirikishwa katika njama hizo toka awali.
Seriously? Ndugai awe na form zinazoonyesha ushiriki wa Mbowe katika njama hiyo halafu atazificha kwa sababu itajulikana kuwa alihusika katika mpango mzima! Tangu lini Ndugai amejali kuhusu public opinion? And worse, mnadhani Mbowe au mtu wake mwingine ni stupid kiasi ya kusaini form ambazo anajua zinaweza kutumika kumchafua?
Hapana, lengo halikuwa kuivuruga Chadema tu, lengo kubwa lilikuwa kuzipa legitimacy CCM na bunge lake fake. Ndugai hakuwa na namna.
Legitimacy inapatikana kwa uwepo wa wale wabunge na sio form. Walitakiwa wabunge kutoka Chadema ambao watakubali kuapishwa hata bila kuwa na form. Na ndivyo ilivyokuwa. Wakina Halima wameendelea kuwa wabunge bila kuonekana form au mtoto wa form.

Mbona hili linaeleweka hata kwa kipofu...uliyekuwa humtaki awe, amekuwa. Kwa wingi wa wenye imani nae kwa sasa, upende usipende, ndiye mwenyekiti
Asiyekubali kushindwa si mshindani. Mimi naheshimu uamuzi wa waliompigia kura Lissu lakini bado naamini kuwa hafai kuwa Mwenyekiti. Muda ndio utakaoonyesha kama niko sahihi au waliompigia kura walipatia.

Aidha, sisi tulichokataa ni mpango wenu wa kutaka mgombea wenu apewe Uenyekiti kwenye kisahani. Tulisema ashindane badala ya kutaka Mbowe amuachie nafasi. Kashindana na kashinda. Tofauti na mlivyotaka kushindana kwake kumempa yeye na chama chake credibility na legitimacy. Hata Lema amekiri hilo.
Sidhani kama hata unaelewa unachokisema. Kwa taarifa yako, hao Covid-19 walishavuliwa uanachama kwa usaliti wao lakini Msigwa na Slaa walijiondoa Chadema kwa sababu na kujiunga na CCM in protest!
Naelewa sana ninachosema. Hakuna mpinzani wake dhati anaweza kuhamia kwa mtesinwake sababu tu anaona kuwa anaonewa kwa kunyimwa nafasi ambayo anaamini aliandikiwa kuwa yake. Wapinzani wa dhati walihamia vyama vingine au walikaa pembeni. Hao unaowatetea, sio tuu walihamia upande wa waliokuwa wanawatesa bali walijiungq nao katika kukibomoa chama chao cha awali. Hao ni watu wetu wenye sense of entitlement na uhusiano ambao ni transactional.
Mimi mpaka sasa hivi huo usaliti wa wakina Halima hata siuoni. Hawa mnaowachukiq hata siku moja hawajakitukana au kukichafua chama chao cha awali kama ambavyo wengi wamefanya. Hawajasaliti principle za chama chao. Na inawezekana na wao walifanya hivyo baada ya frustration na chama chao lakini tofauti na wakina Msigwa waliendelea kukiheshimu.

Hapana, sikubaliani na wewe. Kama wanaipenda Chadema waombe kwanza msamaha halafu waombe upya uanachama.
Kwani nani amesema wasiombe msamaha? Ninachopinga mimi ni kuweka masharti ya kijinga ya kuwataka kukiri na kuwataja waliohusika katika huo mnaouita usaliti. Naona attitude hiyo ni insulting kwa kuamini kuwa wanawake kama Halima hawawezi kufanya uamuzi bila kushirikisha mwanaume.
Kwani Aidan kosa lake nini? Je kugombea Ubunge kwa tiketi ya Chadema na kushinda ni kosa?
Aidan alikaidi agizo la chama chake kuwa haitakuwa na mbunge bungeni kwa sababu hawqutambui uchaguzi mzima. Ni sababu hiyo hiyo iliyowafanya wasipeleke majina ya wabunge wa viti maalum.
Aidan, ni perseverence ndio pengine imewafanya watu waamue asifukuzwe na hapa mwishoni kumkumbatia.

Kwa taarifa yako niliamua kutojibu chochote utakachoweka humu kwa sababu sikubaliani na lugha unazotumia. Nimeijibu hii kwa sababu tumekuwa pamoja humu ndani kwa muda mrefu.

Aidha, katika muda wote huo haukuwahi kutumia maneno ya shombo hata pale tulipotofautiana. Isingekuwa hivyo ningekuweka katika ignore list yangu. Na nikihisi tu kuwa unachotaka ni kubishana tuu na sio kubadilishana mawezo nitakuweka kwenye hiyo list. Umeanza kunichosha.

Amandla...
 
Aaah sasa kwanini hakuaga kama alikua msafi? Yaani alikimbia mara tu uchaguzi unaanza!!

Wala hakuna mpango wa kuwashughulikia ila kuna mpango wa "enquiry" kivipi wake za Mwalimu, Kigaila, na Mrema walienda bungeni!!

Sasa unakimbiaje kama unaongea ukweli.

Kigaila is a disappointment
Dalili za kangaroo court zinaonekana mapema. Bora amejiondokea maana mngedai anavuruga enquiry. Sasa hivi mko huru kufanya mnachotaka lakini bado mnamtafuta.

Sio kila mtu ana uvumilivu wa Mbowe. Kamaliza kazi aliyopangiwa na hakuna sababu ya kuwa mnafik. Kama vile mke wa Obama alivyokataa kuhudhuria shughuli za uapisho wa Trump. It was her prerogative kama ilivyo kwa Kigaila. Mmeshinda, mmeteua mwingine kuchukua nafasi yake, endeleeni kutimiza ahadi mlizowapa wanachama wa Chadema na watanzania kwa ujumla. Muacheni Kigaila aendelee na maisha yake in peace. Kumsakama kunaonyesha jinsi mlivyo petty.

Una haki ya kuwa disappointed nae. Lakini hauna haki ya kutaka wengine wote wawe disappointed nae.

Amandla...
 
Acha uongo, kwamba wanawake wapokee wabunge 19 alafu oktoba nani atapata fursa ya kuingia bungeni? If anything hao wakifukuzwa ina maana viti zaidi ya 20 vitakua free kwa BAWACHA.
You don't make sense! Halima atalazimishaje wajumbe wa Bawacha wapitishe jina lake kuwa mgombea wa viti maalum halafu aiko convince Kamati Kuu ya Lissu kupeleka jina lake kwa Tume Huru ya Uchaguzi. Huyu huyu Halima unayesema kuwa Bawacha hawamtaki na uongozi wote wa sasa wa CDM hawamtaki! Hauoni hiw ridiculous that argument is?

Kweli stupid is as stupid does. Kwaheri. Unanipotezea tu muda.

Amandla..
 
Lissu hajawakataa! Lissu alichosema waje waseme nani alisaini fomu zao walizoteuliwa kwenda bungeni!
Wakijieleza nadhani wanaweza kuruhusiwa kuja kundini!
Usikute hao ni moja ya wahusika. Wanataka mambo yaishe kimya kimya
 
Tundu Lissu ajenge chama kama alivyahaidi.

Aache Uharakati na kufukuzana na chupi. Musamaha ikufike Bulaya.

Nitamkote memba mwenzi yetu hapa
"Lissu should start to show his "STATEMANSHIP" end kwot

My take
Wanawake wa CHADEMA wameshalalamika kuwa kuna mfumo dume chamani, Lissu anakimbizana na kujibishana nao, watakosa bloc maalum Uchaguzi ya 2025. Ok
Kwani kujenga chama ni kufanyaje? Kutoa kauli ya chama juu ya maswali anayoulizwa ni kufanya nini? Chama kusimamia nidhamu kwa wanachama ni kufanya nini?
Au wenzetu mnategemea atakusanya matofali na kuanza kujenga?
 
lisu anashida gani na hawa kina mama ache ujinga jamii inamwona debe tupu
 
You don't make sense! Halima atalazimishaje wajumbe wa Bawacha wapitishe jina lake kuwa mgombea wa viti maalum halafu aiko convince Kamati Kuu ya Lissu kupeleka jina lake kwa Tume Huru ya Uchaguzi. Huyu huyu Halima unayesema kuwa Bawacha hawamtaki na uongozi wote wa sasa wa CDM hawamtaki! Hauoni hiw ridiculous that argument is?

Kweli stupid is as stupid does. Kwaheri. Unanipotezea tu muda.

Amandla..
You're not only stupid but insanely senile!! Hoja ni kwamba hakuna BAWACHA anamtaka Mdee na wenzie maana kuwarudisha ni kumaanisha watajizibia nafasi 20 za ubunge viti maalum hiyo oktoba. Kwahiyo sio tu Lissu, au baraza kuu na hao BAWACHA wanaohitaji hao wasaliti.
 
You're not only stupid but insanely senile!! Hoja ni kwamba hakuna BAWACHA anamtaka Mdee na wenzie maana kuwarudisha ni kumaanisha watajizibia nafasi 20 za ubunge viti maalum hiyo oktoba. Kwahiyo sio tu Lissu, au baraza kuu na hao BAWACHA wanaohitaji hao wasaliti.
Hizo nafasi zimeandikwa Halima Mdee? Watazihodhi vipi kama watawekewa masharti ya kuwa watarudi kama wanachama wa kawaida na hawataruhusiwa kugombea au kushika nafasi ya uongozi kwa muda fulani?
Kweli stupid is as stupid does. Na nyie ndio washauri wa Lissu?

Kwaheri na karibu kwenye ignore list.

Amandla...
 
Watazihodhi vipi kama watawekewa masharti ya kuwa watarudi kama wanachama wa kawaida na hawataruhusiwa kugombea au kushika nafasi ya uongozi kwa muda fulani?
Kanuni gani ya chadema inazuia hii? Kama 2020 hawakuomba unadhani mwaka huu watasubiri ridhaa ili waende bungeni?
 
Sio point. CCM wanashiriki kwa sababu ni takwa la kikatiba. Na wanahitaji legitimacy kuwa wanakubalika na raia wa Tanzania. Hili la wakina Halima ni tofauti. Panapo fanana ni kuwa bila ya wakina Halima Bunge lingekosa legitimacy. Kuna Kamati ambazo zinatakiwa ziongozwe na upinzani. Bila ya wakina Halima zingekosa wenyeviti. Na ili kupata mbunge wa viti maalum chama kinatakiwa kupata kiwango fulani cha kura za wabunge. Vyama vilivyokuwa na sifa hiyo ni CCM na CDM tu.

Amandla....
Mkuu hata yeye alizisaini kwa kujua kuwa ni takwa la sheria kuwa wabunge lazima wawe na udhamini wa chama kupitiwa fomu zilizosainiwa na katibu au mwenyekiti. Asingeweza kusema waende tu wakapokelewe sababu ni CCM mwenzao
 
Mkuu hata yeye alizisaini kwa kujua kuwa ni takwa la sheria kuwa wabunge lazima wawe na udhamini wa chama kupitiwa fomu zilizosainiwa na katibu au mwenyekiti. Asingeweza kusema waende tu wakapokelewe sababu ni CCM mwenzao
Tangu lini Ndugai alizuiwa kufanya analotaka kwa vile Katiba au taratibu zinamkataza? Angekuwa na hizo fomu asingefanya haraka kuwaapishia gereji.

Mbowe alishiriki katika kuanzisha hiki chama. Ameathirika sana kibiashara. Amekaa mahabusu mara chungu mzima. Amefungwa. Watu wake wa karibu wamepotea, wengine wamefungwa na wengine wameuawa. Leo unaniambia alifanyiwa yote hayo akiwa mole wa chama tawala? Mnasikitisha sana.

Amandla...
 
Team Lisu mna matatizo sana, sasa unadhani wajumbe wanatoka wapi chadema? Hamtafika popote na matusi, mpaka mtairudisha chadema mikono salama.
Amka toka ndotoni utajinyea, zoeeni kuongozwa na msiyempenda
Mwalimu hakutukanwa kama Kigaila. Kigaila karibu washikane mashati na Lema Arusha. Kigaila alisingiziwa kuwa anawanyima vitambulisho wajumbe wa Lissu. Kigaila ameambiwa mara kibao kuwa haaminiki kwa sababu ya mke wake. Ilikuwa wazi kabisa kuwa Lissu asingeendelea nae. Na watafanya kila juhudi kumpaka matope. Lakini mlitaka asimame kinafik na kuwaaga? Mwalimu protegee wake amemrithi.

Sasa unakiri kuwa kulikuwa na ajenda ya kuwashughulikia. Wanachofanya wakina Lissu ni ku alienate watu wenye uwezo mkubwa na commitment kwa chama kwa sababu ya petty grievances. Ita backfire tu. To paraphrase them " mkimaliza kuwashughulikia wakina Kigaila na Mwalimu mtaanza kushughulikiana wenyewe". Na ndio, kulikuwa na mpango wa kumshughulikia Mrema lakini kuna mtu akawa na pupa. Sio vizuri wanavyofanya. Wanaendeleza yale waliyomfanyia Mbowe kwa watu wanao amini ni watu wake badala ya kujaribu kushirikiana nao. Halafu wanazungumzia kutibu majeraha!

Amandla...
Rubish
 
Tangu lini Ndugai alizuiwa kufanya analotaka kwa vile Katiba au taratibu zinamkataza? Angekuwa na hizo fomu asingefanya haraka kuwaapishia gereji.

Mbowe alishiriki katika kuanzisha hiki chama. Ameathirika sana kibiashara. Amekaa mahabusu mara chungu mzima. Amefungwa. Watu wake wa karibu wamepotea, wengine wamefungwa na wengine wameuawa. Leo unaniambia alifanyiwa yote hayo akiwa mole wa chama tawala? Mnasikitisha sana.

Amandla...
Hata CCM na hao Covid 19 walikuwa wanashangaa kwa nini, rufaa ya kina Mdee haisikilizwi badala yake Mbowe na wanachadema wanalalamika kuhusu spika kuendelea kuwatambua.

Wenyewe chadema hawataki kusikiliza rufaa ila wanalalamika kuhusu spika.

Kuhusu Mbowe kuhusika na hao Covid 19 kuwepo bungeni, Mdee alishasema kitambo sana, "muulizeni mwenyekiti"
 
Back
Top Bottom