Jicho la tabu: Marekani wakijiridhisha Putin anapanga kutumia nyuklia, watamuwahi kabla hajafanya hivyo na watamgeuzia kibao katumia

Hakutaka kupiga kama [emoji631] anavyoshambulia mpaka watoto wa shule na mahospitali kama alivyofanya katika sehemu nyingi duniani
Mrusi ameheshimu sana hii vita na isitoshe ni ndugu tu

America wao wakinyanyua makombora wanapiga hata desert popote iwe kambi ya jeshi au walipojihami wananchi ni kupiga tu

Nakumbuka bunker busters alizotumia Iraq huku akisema ni wameficha silaha kali wakati ni mahandaki ya kujificha watu

Ila vita mbaya ni kuisikia kwa jirani tu
Hamfatilii vita harafu mnakuja kuandika humu ushaona huko yake makaburi waliyozikwa Wa ukraine wanayofukua sasa hivi na kuyazika upya wamesema hiyo kazi itachukua miaka kadhaa...pana mass burial za kutosha kama kitu hukijui tulia mkuu..
 
Mkuu, hivi ni kwamba umeamua ku block akili yako kutambua kuwa Russia anapigana na NATO hapo Ukraine ama ni makusudi tuu au akili hauna?naamini HAUNA AKILI ya kufikiri
Sasa kwenye akili huku tutafika mbali mkuu mimi huwa simtoi mtu akili mazee...wewe mwenye akili jitathimini kwanza harafu angalia unaweza kusimama kumwambia mtu mwingine nisiemfahamu hana akili?
 
Hivi wajuzi Kuna bomu linaloweza kutoka marekani Hadi Tanzania.
Tunajua marekani na urusi zipo karibu karibu wanaogopa
 
Ushindi katika vita ya nyuklia hautamuliwa na ubora wa Jeshi wala silaha nchi husika ilizonazo, bali ni nani atamuwahi mwenzake katika kutumia nyuklia kushinda/ kumaliza vita.

Kwa msingi huo, msitegemee Marekani asuburi Russia atumie nyuklia ndio nae ajibu mapigo, bali atamuwahi akishajiridhisha kwa asilimia 100 kuwa Russia anakwenda kutumia nyuklia.

Katika hili, sitarajii Biden atasubiri idhini ya Bunge bali litachukuliwa kama ni jambo la dharau linalohitaji Immediate response kwa usalama wa US na washirika wake.

Vile vile wanaweza hata kumzushia katumia nyuklia katika kutafuta justification ya kumshbulia kama walivyofanya kwa Sadam Hussein walipodai kuwa alikuwa na silaha zilizopigwa marufuku( weapons of mass destruction).

Kwa sasa Biden anachofanya ni kuiandaa dunia kisaikolojia kupokea taarifa za aina hiyo wakati wowote kuanzia sasa.

Time will tell.
Wewe ni mhanga mwingine wa hollywood movies
 
Mkuu, hivi ni kwamba umeamua ku block akili yako kutambua kuwa Russia anapigana na NATO hapo Ukraine ama ni makusudi tuu au akili hauna?naamini HAUNA AKILI ya kufikiri
Mbona Putin alishatahadharisha mapema kabisa yeyote atakayeingilia vita vya Ukraine kwa namna yoyote atajibiwa kwa kipigo kikali.

Kwahiyo kama NATO wapo Ukraine maana yake Putin ana mikwara mbuzi?
 
Marekani+NATO wamekaa Afghanistan kwa miaka 20 na mwishowe wamekimbia kwa aibu na Jamaa waliowapiga US Ni wanavaa kobazi tu na ak-47 na hapo hawajapata kutoka nchi nyingine.

Kwa kweli Nilikuaga nadhani US Ni superpower Ila kwa kitu wataliban waliwafanya niliwadharau sana.

]
Wakati US akiwa hapo Afghanistan kwa kipindi chote si alikuwa ana control kila jitu hadi Rais alikuwa kibaraka wake.

Baada ya kujichotea walichokitageti basi wakaona wajiondokee sasa waendelee kubaki ili wagundue nini?
 
Ushindi katika vita ya nyuklia hautamuliwa na ubora wa Jeshi wala silaha nchi husika ilizonazo, bali ni nani atamuwahi mwenzake katika kutumia nyuklia kushinda/ kumaliza vita.

Kwa msingi huo, msitegemee Marekani asuburi Russia atumie nyuklia ndio nae ajibu mapigo, bali atamuwahi akishajiridhisha kwa asilimia 100 kuwa Russia anakwenda kutumia nyuklia.

Katika hili, sitarajii Biden atasubiri idhini ya Bunge bali litachukuliwa kama ni jambo la dharau linalohitaji Immediate response kwa usalama wa US na washirika wake.

Vile vile wanaweza hata kumzushia katumia nyuklia katika kutafuta justification ya kumshbulia kama walivyofanya kwa Sadam Hussein walipodai kuwa alikuwa na silaha zilizopigwa marufuku( weapons of mass destruction).

Kwa sasa Biden anachofanya ni kuiandaa dunia kisaikolojia kupokea taarifa za aina hiyo wakati wowote kuanzia sasa.

Time will tell.
Du! Ficha ujinga wako yaani taifa moja lijjpe uhalali wa kutumia nyuklia kwa dhana tu ya kwamba kuna taifa linataka ku kutumia nyuklia. Inasikitisha sana kuona kuna mijitu bado inaamini marekani ndio kila kitu
 
Mkuu, unafahamu kitu kinaitwa "dead hand"?

Vita ya nyuklia haina kuwahiana. Hao wakubwa walilijua hilo siku nyingi sana. Wakatengeneza systems zinazoweza kufanya retaliation hata kama watu wote wamekufa.

Yani ukipiga bomu ukaua watu wote Urusi, wala hautabaki salama. Walishatengeneza system ambayo inaweza kutambua shambulizi limetokea wapi, na yenyewe ikajibu kwa mashambulizi mazito zaidi.

Putin alisema "You won't even get the time to repent". Yani ukiishambulia Urusi kwa nyuklia, hautapata hata muda wa kusali sala ya toba. Itakushukia mvua ya makombora mpaka shetani abaki anashangaa "mbona ghafla sana jamani".

Hata hao marekani pia wanayo system yao. Hiyo habari ya kuwahiana labda itokee kwa Uganda na Rwanda. Sio hao mabeberu!
Hayo mabomu hadi kufika Marekani sana sana washington kuna muda unakuwepo...
Ila Urusi ndiye ana tabu maana kwake mabomu yako karibu tu hapo Turkiye
 
Mkuu, unafahamu kitu kinaitwa "dead hand"?

Vita ya nyuklia haina kuwahiana. Hao wakubwa walilijua hilo siku nyingi sana. Wakatengeneza systems zinazoweza kufanya retaliation hata kama watu wote wamekufa.

Yani ukipiga bomu ukaua watu wote Urusi, wala hautabaki salama. Walishatengeneza system ambayo inaweza kutambua shambulizi limetokea wapi, na yenyewe ikajibu kwa mashambulizi mazito zaidi.

Putin alisema "You won't even get the time to repent". Yani ukiishambulia Urusi kwa nyuklia, hautapata hata muda wa kusali sala ya toba. Itakushukia mvua ya makombora mpaka shetani abaki anashangaa "mbona ghafla sana jamani".

Hata hao marekani pia wanayo system yao. Hiyo habari ya kuwahiana labda itokee kwa Uganda na Rwanda. Sio hao mabeberu!

Vyema sana. Unajua
 
Broo nyuklia sio AK 47.
Eti atumie Russia dhidi ya Ukraine Marekani waijibu Russia dhidi ya shambulio. Hili sahau. Tuliokuwemo katika miaka ya Vita baridi tunajua na kukumbuka Kwamba Tension ( sintofahamu) ya kijeshi iliopo Ukraine haifiki hata Robo ya tukio la Cuban missiles Crisis.
Kulikua na urushianaji maneno was kutisha.
Ukiachana na Hilo Kuna Vietnam alipokimbizwa Marekani na wavietnam wakisaidiwa na Warusi ( Soviet) kwa kila kitu .
Pia Kuna hii wasovieti ( Russian) walipokimbizwa vibaya Afghanistan baada ya Vita ya miaka takriban 9. Hapa Wamarekani walikuwa dhidi ya Wasovieti wakiwasaidia was Afghanistan.
Kwahiyo basi si rahisi Kwamba endapo itatokea Russia pekee ndo itaangamia. West yote hasa NATO ya ulaya itaangamia . Yatapigwa makombora Russia yote lakini kumbuka Kuna submarine ziko active mda wote zitafanya exchange ya makombora. Atabaki Nani?

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
Ndio maana tunakwambia Soviet tactics no more weigh

Ndio maana silaha za kipindi Cha Soviet no more weigh kwa sasa, Urussi Yuko too mechanical hata Kama ana nyuklia at hand!
Mfano mrussi alijua kwa vifaru atashinda vita...ni njia ya kisovieti kbs
Bado nasema Russia pamoja na ukubwa wake na ukuu wake hawako makini
 
Hata Mrusi aliiaminisha dunia kuwa ana Jeshi bora na silaha bora kabisa duniani lakini leo anaumbuka. Hivyo, usiamimini sana katika huo ufanisi unaoelezwa maana sometimes ni exaggeration tu.
SMO ndogo tu kachukua 15 ya nchi kama Ukraine ambayo ni ya pili barani ulaya. Tuache mahaba inaharibu reputation zetu mkuu
 
Kunielewa inatakiwa uwe makini sana mkuu sio unasoma tuu na kujibu...Ukraine ndio Nchi inayoaminiwa na UN kwenye mission zake za kijeshi kama huko DRC na kwingineko wanajua sana vita ya guerilla hao jamaa wakiwa na siraha ni hatari kuliko unavyodhania...kwao pana vita wengine wapo DRC na bado Urusi anasumbuka huko...
Ndio upo mirembe
 
Ndio upo mirembe
Mkuu sisi wa Kilwa huwa hatutukani tumelelewa maisha ya kuheshimu watu hata usiowajua badili avatar yako ndio uendelee kutukana mimi huwa sihangaiki na matusi hiyo stage nilipita siwezi kuirudia tena mazee...Ustaarabu haauzwi dukani au hakuna Elimu ya ustarabu...
 
Putin alisema "You won't even get the time to repent". Yani ukiishambulia Urusi kwa nyuklia, hautapata hata muda wa kusali sala ya toba. Itakushukia mvua ya makombora mpaka shetani abaki anashangaa "mbona ghafla sana jamani".
!

Hii mikwara ya "Putin alisema ...." tumeshaizoea.Putin alisema atakaeisaidia Ukraine kwa silaha atakiona cha moto.Putin alisema Wanajeshi wa Ukraine wamuondoe Zelensiky na wao wajisalimishe mara moja.Putin alisema atapiga Finland na Sweden wakithubutu kutaka kujiunga na NATO.Putin alisema hiki Putin alisema kile and the list goes.
 
Kwenye hii ishu usimuamini au usihadaike sana na Muongeaji ukampuuza anayekaa kimya.

Binafsi sitishiki kivile na Putin. Najua anaweza kuharibu ila naye ataharibiwa na hakuna atakachofaidi maana anachokitafuta hatokifikia tena.
 
Hata Mrusi aliiaminisha dunia kuwa ana Jeshi bora na silaha bora kabisa duniani lakini leo anaumbuka. Hivyo, usiamimini sana katika huo ufanisi unaoelezwa maana sometimes ni exaggeration tu.

Kila siku nawakumbusheni kuhusu vita ya VietNam - swali ni,je,WavietCong walikuwa na uwezo gani kijeshi, kiuchumi kuishinda Merikani, sasa ilikuwaje kuwaje wakaishinda a Super Power, hilo hamliasemi masaa yote kuisema na kuwakebehi Warusi na Putin - hamkumbuki yaliyo wahi kuwakumba jeshi la Wamerikani miaka ya nyuma.
 
Back
Top Bottom