simu yangu ya htc ilipasuka kioo, nikatafuta weee, mwisho kuna mtu humu jukwaani akanitajia fundi yupo posta anaitwa sele. nikaenda kufika kaniambua kioo kipo ila bei laki, haipungui wala nini, nikaona pagumu.
mwezi uliopita nikaamua nijaribu ebay nikakuta vioo kibao nikachagua model yangu, nikalipia kwa paypal, kama elfu 36 tu na free shipping.
baada ya wiki 3 nimekipata kioo.
kwa wale wanaohofia kuibiwa au kutapeliwa, mie nimepata bidhaa niliyonunua, nanyi msisite kununua.
kuna majibu bado cjapata.
vipi kuhusu Adress line 1 na Adress line 2?
hyo nimeikuta ktk paypal na cjajua najaza vp.
wanaojua naomba wanipe majibu tafadhali
simu ulienda kuichukua wapi mkuu,airport,bandarini au crdb?
Simu nilienda kuchukua kwenye ofisi za FedEx
ebay mambo yao poa. kwa wale wenye kadi za bank ya CRDB nendeni bank jisajili kwa online purchase. Utasubiria kwa wiki moja hadi mbili au hata siku 3 kadi inakuwa active. Then, jisajili paypal nakwambia utaokoa fedha kwa kununua vitu kwa bei poa.
Du itabid nikuchek unisaidie
Gharama za usafrishaji kwa FedEx walikuchaji bei gani? Ukitoa gharama za manunuz ya cmu
Gharama za usafirishaji zilikua dola 30 tu... nililipa wakati nanunua simu ilipofika sikulipia tena
Yule aliyekuuzia ndo alikujumlishia na hela ya u2maji au ni fedex wenyewe?
Nami kichwa saizi kinagonga maanaa haya yote sikuyajua!!!
Nilikwenda crdb nikajaza fomu ya internet enabling service. Baada ya cku mbili nikapata ujumbe kwa njia ya email kwamba kadi yangu iko tyar kwa manunuzi. Baada ya hapo nikaenda paypal na kuingza details zangu na ikakubali.
Assume This:Lakini bado hujanipa jibu kuhusu address line 1 na 2 ...ww ulitumia ipi....
Mkuuu hiyo ni Education material hamnaga kutozwa Ushuru
Laptop nayo ni education material?
Hivi printer wanachaji ushuru? Nimeona printer zenye free shipping on ebay nawaza kununua
Hii thread inanihamasisha kufungua petition kui-request Paypal kuruhusu Paypal Tanzanian Accounts to be able to receive money
! Wakati fulani nilijaribu kuleta hiyo mada hapa lakini ni kama haikuwa na uungwaji mkono; probably ilitokana na uelewa mdogo wa wadau kuhusu suala zima la Paypal account! We don't have always use Paypal to make payment (Encouraging Importation); I think it's time now to make use of Paypal to receive payment and thus encouraging online exportation! Nadhani kama tunapata uungwaji mkono na serikali na kuondosha vikwazo basi it's possible kabisa! Hatima watu wangeuza vinywago ebay badala ya kusubiria wazungu waje!