Ninataka kununua laptop ebay, inaweza kunifikia kweli kwa hapa tz? Vipi kuhusu mambo ya kodi kwa hawa tra?
Duh, mkuu sijawahi agiza PC ila nadhani kama utaweza kuwatumia intermediaries kama ComGateway na MyUS unaweza ipata ndani ya wiki au chini ya hapo. Shida ni gharama za huduma zao. Coz kuna kipindi niliwauliza cost ya services zao (ComGateway) wakaniambia Standard Shipping ya wiki moja kwa mzigo unaoanzia kilogram 1 ni almost 120k za bongo na kama unataka fasta zaidi ni 75$ (sikumbuki hizo digits vizuri mkuu coz ilikuwa ni ka miezi 3 iliopita). Hawa wanaweza ongeza guarantee ya wewe kuupata kwani wanasimamia show nzima wao na hao couriers wanaowatumia wao mpaka mzigo ukufikie na pia mzigo unakuwa na Tracking Number.
Sa kwa kawaida, hii ya kununua tu na kusubiria ufike posta wakushtue ukauchukue, hapo ndo sina uhakika napo. Ila kwa uhakika wa kupata mzigo wako haya yanaweza ongeza guarantee ya wewe kupata mzigo wako:-
i) Request Tracking Number kutoka kwa Muuzaji.
Mara nyingi items utakazolipia Shipping costs/charges, seller anakutumia pamoja na Tracking Number ikiwa pamoja na jina la Carrier (ni kampuni gani itabeba item yako). In case hajakutumia, unaweza request afanye hivyo, japo lazma itaku'cost kama 5$ hivi ya nyongeza. Na hii ufanye kabla hujalipia bidhaa kupitia "contact seller". Mizigo yenye tracking number dizain flan ngumu kukana uwepo wake kwani movements zake zinaweza kuwa tracked all over the globe.
ii) Kuwa na 'mtu wako' pale posta. Si unajua tena bongo yetu. Katika trip zako za kwenda kuchukua mzigo wako, tengeneza urafiki (au pata contacts za) na mmoja wa wanaohusika na International Parcels. Then, huyo atakuwa anakushtua pale mizigo ikifika. Siku moja moja hata 5k ya chai si mbaya.
iii) Kuwa mfuatiliaji kweli na serious.
Sasa kuhusu TRA, naskiaga kwa parcel kubwa kubwa za kwenye box kama kuanzia kg 1 (sina uhakika katika hili, wengine mtanisaidia) wanatoza asilimia 16 (16%) ya gharama ya mzigo. Kwa PC naskia hawana kodi zaidi ya cable yake tu (napo sina uhakika). Mkuu ntaulizia kiundani kwenye hili kwa uhakika zaidi.
Pale nilopokosea, wakuu mnisaidie kurekebisha.