Jifunze kilimo cha nyanya

Naomba kuuliza mbegu ya kisasa yenye unafuu wa bei tofauti na Assila,
Wengi mnaangalia utofauti wa bei wa assila na mbegu zengine za kisasa

Hamuangalii tofauti ya uzaaji, ubora na uimara wa matunda ya assila na mbegu zengine, hamuangalii ipi inafanya vzr sokoni, bei hamuangalii bei maana assila na hizo mbegu zengine haziuzwi bei moja
Assila inapendwa hadi wauza nyanya magengeni, zinakaa muda mrefu bila kuharibika na zina umbo kubwa inasababisha kupata boksi nyingi wakati wa kuchuma
 
Mkuu hizi mbegu Sio zile nyanya yenye ngozi laini ambazo wafanyabiashara wanaziogopa? Hiyo Jarrah punje ngapi itatosha eka 3?

Jarrah eka moja ni punje elf 8 sababu zinapandwa mstari mmoja tu kwa umbali wa 1.5 mstari ( tuta) hadi mstari (tuta).
Ngozi yake ni ngumu sana na inahifadhika kwa mwezi mzima chini bila kuweka kwenye friji ( iwe sehemu cool and warm with room temperature). Mche mmoja ni kg 10 hivyo eka moja huwa ni kuanzia crate elf 1 kama itapata matunzo yote stahili

Upate to crate mia tano tosha sana
 
Mkuu naona mambo ni moto,,nlipotea kdg ila naleta maswal yngu soon
 
Duh!! Mkuu mm nimechanganya nyanya na pilipili hoho kwenye field moja,, Inaweza leta shida yoyote??
 
Duh!! Mkuu mm nimechanganya nyanya na pilipili hoho kwenye field moja,, Inaweza leta shida yoyote??

Zao la famili moja means wadudu lazima wawe wengi itakulazimu kupiga sana dawa. Kukiwa na ugonjwa yote yanashambuliwa sababu ni same family. Ila kama kila kitu kitaenda sawa moja wapo litakupa hela nzuri
 
Mkuu ni wapi zinapatikana hzo kwa punje nijaribishe ht mbegu 500
 
Zinapandwa kwa "Mstari mmoja tu" ki vp mkuu??
 
Zao la famili moja means wadudu lazima wawe wengi itakulazimu kupiga sana dawa. Kukiwa na ugonjwa yote yanashambuliwa sababu ni same family. Ila kama kila kitu kitaenda sawa moja wapo litakupa hela nzuri
Ok, pia hizi hoho sijawah kuzpiga dawa yoyote toka nizipande mana sijawah ona dalili yyte mbaya japo na natarajia kuzihamishia shamban j3 na kuna chache ambazo nishaziamishi

Je kuna dawa yyte ntatakiwa nipige? mbolea ya kupandia nliweka samad kiganja ki1 na dap gram 10.

Pia hii miche naona km sio ya kijani sana yan ukijani wake unaelekea kwenye unjano flani hivi, ni tatizo au ndo zilivyo?


Mbegu ni Califonia wonder
 

Shambani zitakaa sawa ukijani utarudi,kwenye kitalu mmea hauwezi kukua kwa kadri unavyohitajika. Fanya drenching ya ridomil gold gm1 kwa ltr 1 ya maji itakusaidia kukinga na fungus
 
Na zile nyanya leo zina siku ya 20 toka zipandwe na toka ziingia shamban nimeweka can mara 1, nmepiga booster mara 1 na pia nimepga abanil ambayo nlichanganya na linkmill mara 1

Naomba unijuze kuhusu mbolea km ntahitaji kuweka tena na pia km kuna dawa yoyote nitahitaji kupiga tena

Ahsante
 

Ikikua inafungwa inakua hivi hivyo njia inabaki kwa ajili ya huduma,ukiweka mistari miwili hii njia inapotea unapata matatizo ya mzungukk mdogo wa hewa hivyo magonjwa mengi
 
Aah sawa,,sema huu ulimaj wa mferej ndo siujui mkuu,, mi najua wa kupga shmo moja moja

Sio mbaya hata huo wq shimo moja moja siunanyoosha mstari??
Kama unanyosha hivyo umbali wa mstar mmoja wa mashimo na mwingine ni sm150 na umbali wa shimo na shimo ni sm50
 
Wakulima salama? Mimi ni mkulima mtarajiwa wa nyanya, naomba ushauri wenu na uzoefu, nahitaji kulima nyanya kwny greenhouse, natarajia kuotesha kwny kitalu week mbili zijazo, sasa naomba msaada wa aina nzuri ya mbegu kwa ajili ya kilimo kwny greenhouse, lakini je nikiotesha nyanya kwny kitalu hadi kuvuna kwa mwezi huo wa pili je siwezi kukutana na mavuno ya msimu wa mvua? Hali na bei ya soko itakuwaje? Naomba uzoefu wenu wadau ! Ahsante sana !!

Sent from my HTC Desire 828 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…