Jifunze kuendesha (ku-control) nafsi ili kujikomboa katika vifungo na kuwa msaada kwa wengine

Niliwahi kutana na watu kama wewe ni kazi sana kuwaaminisha kuhusu uwepo wa ulimwengu wa kiroho ...kuna muda utafika lakini utaamini
 
Bora wewe umekuwa mkweli, wengi wanapenda kutoa ushuhuda wa uwongo.
 
Unaelewa kuwa mpaka hapa ushakubali kwamba imani ya kuwapo Mungu inaweza kuwa na madhara?
 
Unafikiri ulimwengu unajiendea tu bila ya mipangilio ya huyo unayesema hayupo? na vipi uumbwaji wako
Je wewe unafikiri huyo muumbaji alitokea tu from no where?

Kuna ulazima upi wa kwamba kila kitu kimeumbwa?

Kama kila kitu lazima kiwe kimeumbwa, Je Mungu huyo aliumbwa na nani?

Kwa nini una exclude Mungu kwenye uumbaji halafu unataka Dunia iwe na muumbaji?

Je huyo Mungu alitokea from nothing?
 
Hili swali alishindwa kulijibu mtakatifu Augustino(Saint Augustine of Hippo), unadhani mr pipa anaweza kulijibu?
 
chimbuko lako wewe ni wapi?
 
Watu wameaminishwa kwamba ukimuomba chochote Mungu lazima akupe

Wameaminishwa kwamba Mungu ni wa upendo tu yaani ni wa mambo mazuri tu bila kutambua kuwa Mungu wa harusi ndiyo huyo huyo Mungu wa misiba
 
Watu wameaminishwa kwamba ukimuomba chochote Mungu lazima akupe

Wameaminishwa kwamba Mungu ni wa upendo tu yaani ni wa mambo mazuri tu bila kutambua kuwa Mungu wa harusi ndiyo huyo huyo Mungu wa misiba
Sasa kwa nini mumpe sifa nzuri nzuri tu huyo Mungu?

Kama huyo Mungu si wa upendo tu, Pia Mungu huyo ni wa Uovu na Ukatili.

Mambo ya kuunda dhana ya "shetani" kwamba ndio chanzo cha uovu ni kujaribu kuficha madhaifu na Uovu wa huyo Mungu wenu.

Huyo Mungu wenu pia ni MUOVU sana.
 
Je unaamini kwamba kuna Nguvu ya asili inayo ongoza binadamu na dunia? Wengine huita Cosmos Energy/Power na wengine huita Consciousness n.k
 
Huo uovu na ukatili ni matokeo ya macho yako yanavyoona

Sisi wengine hatuoni kama ukatili bali ni asili jinsi ilivyo

Ndiyo maana kuna usiku na kuna mchana!

Mbona giza likiingia hupigi kelele kwanini mwanga umetoweka??
 
Unathibitisha vipi elimu uliyonayo wewe kuhusu Mungu ni sahihi sana kuliko ya wengine?

Au unafosi mafikirio yako kuhusu huyo Mungu ndio mafikirio ya kila mtu?
Na wewe unathibitisha vipi uelewa ulionao kuhusu Mungu ndiyo sahihi kuliko wa wengine??
 
Profesa Noah Harari wa chuo kikuu cha Jerusalemu, nae, kwny kitabu chake cha SAPIENS, anasema ''if there is God, then he is evil''
 
Na wewe unathibitisha vipi uelewa ulionao kuhusu Mungu ndiyo sahihi kuliko wa wengine??
Kwa sababu huyo Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.

Hakuna uthibitisho wowote ule wa uwepo wa Mungu zaidi ya blah! blah! na stori za kusadikika tu.

Maandiko yote ya kidini kuanzia Biblia, Quran,Torah, Tip taka na vitabu vingine vyote vya kidini ni Fiction stories sawa na Hekaya za Abunuwasi au riwaya za Alfu Lela ulela.
 
Hakuna Madhara yoyote mkuu

Shida iliyopo ni kuwa watu hawana elimu sahihi kuhusu Mungu
Unaelewa kuwa, ikiwa kweli kuna watu hawana elimu sahihi kuhusu Mungu , huo nao ninushahidi kwamba Mungu hayupo?

Kwa sababu, kama Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote yupo, na ndiye kaumba ulimwengu huu, asingeumba ulimwengu ambao inawezekana kiumbe chake chochote kikakosa elimu sahihi kumhusu yeye Mungu.

Unaelewa hilo?

Au maneno mengi nikuwekee picha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…