Afadhali umenitia moyo best....
mimi nimejaribu vitumbua mara kadhaa....
mara wananiambia vile vikaangio havijazoea mata sijui nini. kwa kifupi huwa naishia kuchemsha uji kwenye mafuta.....
nikaamua kujiachia zangu
asante kwa mara nyingine!bagia zilitoka mwaaa!
Mkate unavutia machoni wallahi waonekana mtam dah!
Usivunjike moyo shosti endelea kujaribu tu!mapishi mengine mpaka uyajaribu mara kadhaa ndo yanakubali...na ukikosea aina ya mchele tu au kuchujua huo unga haviwi!
Yeah...mkate wa kumimina pendelea kutumia mchele mkavu maana mengine kama ina mafuta mafuta....inakua haiji vizuri
Aisee! naomba uwe unatoa copy na kwa wife wangu pia..anapenda sana kujifunza mambo mapya
asante kwa pishi la mkate sijawahi onja mkate wa ufuta........ sipendi mkate jamani labda unitengeneze naweze kupenda huu lol
Thanks aloooot madame, will practice the theory!! Mega bless
Wanadai kikaango ukikiunguzia machicha ya nazi kinakuwa sawa,sijui pana ukweli hapo?
farkhina naomba ya mkate wa ufuta na mkate wa tambi.
Yani baada ya kusoma hii post, ghafla nimeskia harufu ya mkate wa ufuta.... LOL.
farkhina apo mbona naona kama jiko la gas? Ina maana twaweza kutumia jiko la gas au? Mana mm nshazoea jiko la seredani.
halafu anaupenda anauita ricebread kwa kilugha 🙂Hahahahaha nimempikia mkwe wangu mwambie aje ale....
Mahitaji
Mchele kikombe 1
Tui la nazi kikombe 3/4- 1
Hamira 1 teaspoon
Hiliki kiasi
Ute wa yai 1
Sukari 3/4 kikombe
Namna ya kutaarisha
1)Roweka mchele usiku 1
2)Saga kwenye blenda mchele,hamira,tui la nazi,hiliki hadi viwe laini..
3)weka sehemu ya joto ili uimuke..
4)washa oven moto kiasi 300-350°..mimina sukari na ute wa yai kwenye mchanganyiko wako then changanya vizuri...
5)weka sufuria jikoni mafuta kidogo yakipata moto mimina mchanganyiko wako
6)baada ya dakika 5-10 mkate ukishaanza kushikana funika kwa ufuniko then weka kwenye oven hadi uwive na kuwa rangi ya brown
7)subiria mkate upoe ndipo uukate vipande vipande
8)mkate wa kuminina tayari kwa kuliwa..