Mahitaji
Mchele kikombe 1
Tui la nazi kikombe 3/4- 1
Hamira 1 teaspoon
Hiliki kiasi
Ute wa yai 1
Sukari 3/4 kikombe
Namna ya kutaarisha
1)Roweka mchele usiku 1
2)Saga kwenye blenda mchele,hamira,tui la nazi,hiliki hadi viwe laini..
3)weka sehemu ya joto ili uimuke..
4)washa oven moto kiasi 300-350°..mimina sukari na ute wa yai kwenye mchanganyiko wako then changanya vizuri...
5)weka sufuria jikoni mafuta kidogo yakipata moto mimina mchanganyiko wako
6)baada ya dakika 5-10 mkate ukishaanza kushikana funika kwa ufuniko then weka kwenye oven hadi uwive na kuwa rangi ya brown
7)subiria mkate upoe ndipo uukate vipande vipande
8)mkate wa kuminina tayari kwa kuliwa..