Jifunze njia nzuri ya kufanya manunuzi kwenye mtandao (Ebay, Amazon, Bestbuy)

Jifunze njia nzuri ya kufanya manunuzi kwenye mtandao (Ebay, Amazon, Bestbuy)

hii ni gharama ya kutuma shati la usd 17 imefikia total 85usd...
View attachment 483412
- Ghalama kubwa ni sehemu ya changamoto kwa shipping company za USA.
1. Kwa kuzingatia hizo changamoto
2. Pia kwa kuzingatia uhitaji wa watanzania wengi

Hivyo nimeanzisha huduma kama ya MYUS, COMGATEWAY etl

Huduma hiyo nimeiita SHIP4ME
- Unanunua bidhaa wewe mwenyewe
- Ila shipping address nakupatia yakwangu ya USA au Taifa jingine kama UK, GERMAN etl kwa kutegemea ni site ipi na ya wapi unanunua bidhaa.

(NB: Faida ya kutumia huduma yanguni zaidi ya MYUS au COMGATEWAY ambapo wao wanakupa anwani ya USA tu, ila kwa mimi nakupa anwani ya CHINA, USA, UK, MUMBAI, JAPAN, FRANCE, GERMAN, etl)

- Ambapo ghalama za kusarishia kwangu zinatokana na uzito wa mzigo tu

Tuchukue mfano hai, Kwa sharti moja uzito wake hauzidi 500g ila ni chini ya hapo, Hapo kwangu ungelipia USD 15 kama freight cost.

Hiyo ghalama walio kucharge kwa upande wangu hiyo ni ghalama ya kusafirishia LAPTOP na sio shati.

Kuhusu huduma ya BUY4ME & PAY4ME pitia hii link: www.v.ht/buy4me

Pole sana Mr. MTUI
 
- Ghalama kubwa ni sehemu ya changamoto kwa shipping company za USA.
1. Kwa kuzingatia hizo changamoto
2. Pia kwa kuzingatia uhitaji wa watanzania wengi

Hivyo nimeanzisha huduma kama ya MYUS, COMGATEWAY etl

Huduma hiyo nimeiita SHIP4ME
- Unanunua bidhaa wewe mwenyewe
- Ila shipping address nakupatia yakwangu ya USA au Taifa jingine kama UK, GERMAN etl kwa kutegemea ni site ipi na ya wapi unanunua bidhaa.

(NB: Faida ya kutumia huduma yanguni zaidi ya MYUS au COMGATEWAY ambapo wao wanakupa anwani ya USA tu, ila kwa mimi nakupa anwani ya CHINA, USA, UK, MUMBAI, JAPAN, FRANCE, GERMAN, etl)

- Ambapo ghalama za kusarishia kwangu zinatokana na uzito wa mzigo tu

Tuchukue mfano hai, Kwa sharti moja uzito wake hauzidi 500g ila ni chini ya hapo, Hapo kwangu ungelipia USD 15 kama freight cost.

Hiyo ghalama walio kucharge kwa upande wangu hiyo ni ghalama ya kusafirishia LAPTOP na sio shati.

Kuhusu huduma ya BUY4ME & PAY4ME pitia hii link: www.v.ht/buy4me

Pole sana Mr. MTUI
Asante mkuu ngoja wajuzi waje... Ntapitia hyo website yako nione yaliyomo
 
Mbona kuna bidhaa nyingine wanasema hauzi kwa tz?
 
Habari za jion, naomba kujua jinsi ya kulipia huduma online, especially kama kama service yenyewe iko china,.marekani nk....
Nimejaribu kutumia card zangu za benki ila zinakataa
 
Labda ungetoa maelezo kama umeshawahi kuitumia kadi kununua bidhaa online hapo kabla? Na je kadi yako ni ya benki gani?
 
jalibu kufungua account ya paypal itakuwa rahisi kwa ww kuripia hizo huduma ingia google andika paypal alaf neenda sehemu wameandika creat account alaf utafuata maelekezo hii njai ni rahisi pia ni salama
 
jalibu kufungua account ya paypal itakuwa rahisi kwa ww kuripia hizo huduma ingia google andika paypal alaf neenda sehemu wameandika creat account alaf utafuata maelekezo hii njai ni rahisi pia ni salama
hawezi kwa kadi ya CRDB mpaka wai activate wenyewe..
 
Naomba msaada. Nimeshindwa kubadilisha account kwenda premium kwenye MyUS.com, hasa shida inayoonekana ni kulipia fee
 
Naomba msaada. Nimeshindwa kubadilisha account kwenda premium kwenye MyUS.com, hasa shida inayoonekana ni kulipia fee
Nimebadilisha membership nikaletewa majibu haya:

An error has occurred. You may need to update the payment or billing information. Please select the My Account Settings tab above then update your Payment Method. Please contact Customer Service if you require further assistance.
 
An error has occurred. You may need to update the payment or billing information.
Hili hujitokeza iwapo account yako ina fedha kidogo au haina fedha kuweza kulipa kiasi husika.
 
Account ina kiasi cha kutosha kulipa madai wanayodai, lakini bado inakataa
 
Imekuwa ni shida sana kwa watanzania wengi kununua bidhaaa katika masoko haya ya mtandaoni kwani mengi huwa hayakupi fursa ya kutumiwa mzigo wako moja kwa moja Tanzania. Baadhi ya thread zilianzishwa na zimeelezea mengi sana kuhusiana na manunuzi haya ya mtandaoni, ila tulipata ufumbuzi mdogo.

Nimejaribu kupitia pitia forums nyingi nichanganue namna mbadala ya kupata mizigo bila ya kutumia gharama nyingi. hii ni kwa kutumia FOWARDING COMPANIES ambazo kazi yake ni;

1: Kukupatia anuani ya Marekani (au popote iliopo ila nashauri marekani au uingereza UK) au US Shipping Address

2: Kupokea mzigo kwenye soko ulilotumia (eidha amazon,ebay au lolote lile lisilo ship Tanzania)

3: Kukutumia mzigo wewe hapo ulipo kwa wakala kama DHL,FEDEX,UPS,USPS NK baada ya kujua kazi ya fowarding company unahitaji kuwa na vigezo vifuatavyo (kwa wageni wasiofahamu/hawajapitia previous threads:

1: CREDIT CARD (KADI YA BENKI) INAYOFANYA ONLINE PURCHASES;
Hii inapatikana almost bank zote hapa Tanzania (kasoro NMB sina uhakika), ni kadi yeyote ya visa au mastercard unachotakiwa ni kwenda kwenye tawi la benki yako na kuomba fomu ya kuruhusu kadi yako ifanye malipo ya mtandaoni(online purchases) na mara nyingi huchukua maximum 24hours kuactivate.

2: KUJIUNGA NA PAYPAL
Hiii ni kampuni inayolinda malipo yako kwa kutomuonesha muuzaji details (nyaraka) za kadi yako kama number na css ambayo vitampa muuzaji access ya kuchukua pesa zako. Ila kwa paypal utalindwa na kurudishiwa pesa pale panapotokea shida au huduma mbaya.

3: KUJIUNGA NA FOWARDING COMPANY

Hii hatua ni ya wewe kwenda kwenye website (tovuti) za hizi fowarding company na kujiunga (sighnup) nazo/nayo ili zianze kukupatia huduma... nitaelezea chini zaidi kuhusu ipi ni ipi na huduma zao zikoje na faida na hasara za kila moja ili ujichagulie wewe mwenyewe binafsi

4: KUTAMBUA SOKO BORA LENYE HUDUMA NZURI(ONLINE MARKET)
Hapa tunazungumzia website za masoko kama ebay,amazon, bestbuy, apple.com, dell.com, toshiba.com nk.. masoko haya ndipo utakapo nunua bidhaa yako.

PROCESS NZIMA KUANZIA UNANUNUA MPAKA MZIGO UNAKUFIKIA IKOJE?


Hii iko hivi....

1: Ingia katika soko lako ulilolichagua au unalopendelea, hapa nasuggest kutumia sana amazon(ndilo ninaloliamini) amazon ukiingia utakuta bidhaa nyingi ila kuwa makini kuchukua zile bidhaa zilizo na alama ya prime chini...alama hiyo inamaanisha kuwa huo mzigo unauzwa, utapakiwa, na kutumwa na amazon wenyewe, so no utapeli hapo, yani u get what u wanted.

2: Nunua na kuagiza kitu kwenda kwenye address ya fowarding company ulioichagua, hivyo mzigo ulioununua utaenda moja kwa moja kwenye company yako, wao wakishaupata watakutumia e-mail uthibitishe au uchague courier wa kukutumia mzigo wako, hapo ndio utachagua either dhl,ups,fedex nk.wao watakutumia na kuchukua kiasi chao cha pesa ya huduma na kukutumia mzigo pamoja na kukupatia tracking number ya kujua mzigo wako ulipo na utaupokea vyema.

FOWARDING COMPANIES ZENYEWE:

1: MYUS.COM link- MyUS.com - #1 International Shipping, Mail and Package Forwarding Service - MyUS.com. Hii ni company niliyoitumia na nina expirience nayo ya mizigo miwili, hawa ni waaminifu wana charge pesa kidogo na huwa hawachukui muda kukutumia mzigo wako. yaani unafika leo hata ukitaka utumwe leo unatumwa, na utafika upesi sana bila ya zengwe lolote.

Ubaya wao: wanatumia sana DHL ambayo kwa mizigo mikubwa ni gharama sana kwa mtanzania wa kawaida, kiasi cha dola kumi kujiunga na huduma zao

Uzuri wao:
watakutumia mzigo hata kama utakuwa hauna pesa kwenye account yako, watakujulisha ni duka lipi lina discount ya kutumia huduma zao, watakukumbusha kulipa deni lao, utapewa muda wa miezi miwili kulipa pesa yao,

2: COMGATEWAY
Link: Shop US Stores and Ship Internationally | comGateway - Hawa pia ni fowarding company nzuri sana (thanks tu Mwl.RCT), nimepitia site yao na huona wana policy nzuri sana, cha kwanza ni sales tax-free U.S. online shopping yaani punguzo la kodi ya kufanya manunuzi marekani, hii inapelekea huduma zao kuwa nafuu zaidi,pia wana ushirika na shipping courie DHL na FEDEX hivyo kufanya huduma zao kuwa rahisi zaidi.pia wanakupa habari kuhusu discount za masoko mbalimbali kama myus..

3: BORDERLINX
Link: Buy in the USA, ship to Belgium with Borderlinx - Hawa pia ni wazuri sana na hawana tofauti sana na stackry ... Wanawiana ingawa ni competitors wakubwa hivyo inakupa urahisi wa kuwatumia..Hawa pia hawana registration fee na wanakupa option tofauti tofauti za kutumiwa mzigo wako.

4: SHIPITO
Link: USA Address & Mail Forwarding – Shipito.com | English - Hii pia ni kampuni kongwe ya fowarding na wao gharama zao ni nafuu sana ingawa wanapokea malalamiko mengi sana kutoka kwa wateja wao ukiangalia kwenye forums nyingi.ila kiujumla ni wazuri kwasababu malalamiko ni madogo kulinganisha na ufanisi na pia wanajua na ni wazoefu sana na kazi yao

5: STACKRY
Link: Stackry - US shopping, global shipping - Hii nayo haina tofauti na myus isipokuwa hawa wao hawana kiasi cha kulipia kujiunga nao na wao pia wanakupa option nyingi za kutumia mizigo yako na mabo yao pia ni mazuri kulinganisha na comment wanazopokea kutoka kwa wateja wao. waungwana ni hayo tu niliyo nayo, kazi kwenu ni kufanya utafiti na pia kuangalia na kuchunguza mabo kabla ya kuchukua uamuzi.

STACKRY na BORDERLINX walikuwa recommended sana na wanasifiwa mno angalia hii link -http://tech-vise.com/10-parcel-forwarding-services-for-international-shoppers/ pitia hizo websites na ujionee mwenyewe chagua moja na utazame kama wanakufaa.

HUU NI MTAZAMO WANGU BINAFSI WAKUU , Please evaluate kindly.

Nilikuwa nataka kuonyesha steps ila naona thread haitoshi maana nimeagiza mzigo na nimechukua hatua zote ili mpate kuona ila I think there are limits..

Help Mwl.RCT
Im impressed...keep on doing good stuffs
 
Back
Top Bottom