Jifunze njia nzuri ya kufanya manunuzi kwenye mtandao (Ebay, Amazon, Bestbuy)

Jifunze njia nzuri ya kufanya manunuzi kwenye mtandao (Ebay, Amazon, Bestbuy)

  • Nimetumia huduma za kampuni zote mbili
  • Nilianza na myus mwezi March na comgateway mwezi July [ screen shot zinajieleza ]
# Kitu ambacho sikupenda upande wa myus ni kuwa hawana option ya kufanya malipo kwa njia ya Paypal, Makato yao huwa ni automatic toka kwenye kadi yako.
# Kama account yako haina fedha na huna mpango wa kuitumia tena waweza kuwaliza - Nadhani hiki ndicho kimekuvutia zaidi

>> Hilo ni kweli iwapo account yako hana kiasi cha fedha cha kutosha, ila ukiweka tu fedha wanachukuwa chao - Kama lengo ni kupata huduma bila ya kulipia basi kwa point hii myus inakufaa
# Kitu nilichopenda upande wa comgateway.
  • Waweza tumia Paypal kufanya malipo
  • Kwangu mimi - hupendelea kufanya malipo kwa paypal na si kwa kutumia kadi, Huwa naamini niko salama zaidi
  • Mteja uamuzi ni wako ni wakati gani ufanye malipo ili mzigo wako utumwe
  • Cost yao kidogo ni nafuu ukilinganisha na myus.
vs1.png

VS
vs2.png


Ni elimu nzuri kwa kweli
 
Wakuu msaada..EBAY kila nikitaka kufanya malipo( confirm and pay), muda huo nipo kwenye ya pay with paypal( kwa sababu tayari nimeshajiunga) Naambiwa your payment didn't go through..please select a different payment option and try again...hebu mnisaidie kwa hilo wataalamu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[QUO TE="moureen mwakibinga, post: 14390989, member: 231228" Tumia unique air cargo
VP sis tunaoagiza mizgo China njia gani rahisi kwetu kampuni gani inafaa
[/QUOTE]
 
Kama kuna yeyote amewahi kuagiza kitu au vitu kutoka Amazon au Ebay,kama mpo naomba mnipe muongozo kame ifuatavyo je kitu ulichoagiza kilifika salama na je huwa ni mda gani kitu hufika baada ya kuagizwa na iwapo kuna huduma ya kuenyesha usogeaji wa bidhaa ninapokuwa safarini
 
Imekuwa ni shida sana kwa watanzania wengi kununua bidhaaa katika masoko haya ya mtandaoni kwani mengi huwa hayakupi fursa ya kutumiwa mzigo wako moja kwa moja Tanzania. Baadhi ya thread zilianzishwa na zimeelezea mengi sana kuhusiana na manunuzi haya ya mtandaoni, ila tulipata ufumbuzi mdogo.

Nimejaribu kupitia pitia forums nyingi nichanganue namna mbadala ya kupata mizigo bila ya kutumia gharama nyingi. hii ni kwa kutumia FOWARDING COMPANIES ambazo kazi yake ni;

1: Kukupatia anuani ya Marekani (au popote iliopo ila nashauri marekani au uingereza UK) au US Shipping Address

2: Kupokea mzigo kwenye soko ulilotumia (eidha amazon,ebay au lolote lile lisilo ship Tanzania)

3: Kukutumia mzigo wewe hapo ulipo kwa wakala kama DHL,FEDEX,UPS,USPS NK baada ya kujua kazi ya fowarding company unahitaji kuwa na vigezo vifuatavyo (kwa wageni wasiofahamu/hawajapitia previous threads:

1: CREDIT CARD (KADI YA BENKI) INAYOFANYA ONLINE PURCHASES;
Hii inapatikana almost bank zote hapa Tanzania (kasoro NMB sina uhakika), ni kadi yeyote ya visa au mastercard unachotakiwa ni kwenda kwenye tawi la benki yako na kuomba fomu ya kuruhusu kadi yako ifanye malipo ya mtandaoni(online purchases) na mara nyingi huchukua maximum 24hours kuactivate.

2: KUJIUNGA NA PAYPAL
Hiii ni kampuni inayolinda malipo yako kwa kutomuonesha muuzaji details (nyaraka) za kadi yako kama number na css ambayo vitampa muuzaji access ya kuchukua pesa zako. Ila kwa paypal utalindwa na kurudishiwa pesa pale panapotokea shida au huduma mbaya.

3: KUJIUNGA NA FOWARDING COMPANY
Hii hatua ni ya wewe kwenda kwenye website (tovuti) za hizi fowarding company na kujiunga (sighnup) nazo/nayo ili zianze kukupatia huduma... nitaelezea chini zaidi kuhusu ipi ni ipi na huduma zao zikoje na faida na hasara za kila moja ili ujichagulie wewe mwenyewe binafsi

4: KUTAMBUA SOKO BORA LENYE HUDUMA NZURI(ONLINE MARKET)
Hapa tunazungumzia website za masoko kama ebay,amazon, bestbuy, apple.com, dell.com, toshiba.com nk.. masoko haya ndipo utakapo nunua bidhaa yako.

PROCESS NZIMA KUANZIA UNANUNUA MPAKA MZIGO UNAKUFIKIA IKOJE?

Hii iko hivi....

1: Ingia katika soko lako ulilolichagua au unalopendelea, hapa nasuggest kutumia sana amazon(ndilo ninaloliamini) amazon ukiingia utakuta bidhaa nyingi ila kuwa makini kuchukua zile bidhaa zilizo na alama ya prime chini...alama hiyo inamaanisha kuwa huo mzigo unauzwa, utapakiwa, na kutumwa na amazon wenyewe, so no utapeli hapo, yani u get what u wanted.

2: Nunua na kuagiza kitu kwenda kwenye address ya fowarding company ulioichagua, hivyo mzigo ulioununua utaenda moja kwa moja kwenye company yako, wao wakishaupata watakutumia e-mail uthibitishe au uchague courier wa kukutumia mzigo wako, hapo ndio utachagua either dhl,ups,fedex nk.wao watakutumia na kuchukua kiasi chao cha pesa ya huduma na kukutumia mzigo pamoja na kukupatia tracking number ya kujua mzigo wako ulipo na utaupokea vyema.

FOWARDING COMPANIES ZENYEWE:

1: MYUS.COM link- MyUS.com - #1 International Shipping, Mail and Package Forwarding Service - MyUS.com. Hii ni company niliyoitumia na nina expirience nayo ya mizigo miwili, hawa ni waaminifu wana charge pesa kidogo na huwa hawachukui muda kukutumia mzigo wako. yaani unafika leo hata ukitaka utumwe leo unatumwa, na utafika upesi sana bila ya zengwe lolote.

Ubaya wao: wanatumia sana DHL ambayo kwa mizigo mikubwa ni gharama sana kwa mtanzania wa kawaida, kiasi cha dola kumi kujiunga na huduma zao

Uzuri wao: watakutumia mzigo hata kama utakuwa hauna pesa kwenye account yako, watakujulisha ni duka lipi lina discount ya kutumia huduma zao, watakukumbusha kulipa deni lao, utapewa muda wa miezi miwili kulipa pesa yao,

2: COMGATEWAY
Link: Shop the US Online and Ship Internationally | comGateway - Hawa pia ni fowarding company nzuri sana (thanks tu Mwl.RCT), nimepitia site yao na huona wana policy nzuri sana, cha kwanza ni sales tax-free U.S. online shopping yaani punguzo la kodi ya kufanya manunuzi marekani, hii inapelekea huduma zao kuwa nafuu zaidi,pia wana ushirika na shipping courie DHL na FEDEX hivyo kufanya huduma zao kuwa rahisi zaidi.pia wanakupa habari kuhusu discount za masoko mbalimbali kama myus..

3: BORDERLINX
Link: Buy in the USA, ship to Belgium with Borderlinx - Hawa pia ni wazuri sana na hawana tofauti sana na stackry ... Wanawiana ingawa ni competitors wakubwa hivyo inakupa urahisi wa kuwatumia..Hawa pia hawana registration fee na wanakupa option tofauti tofauti za kutumiwa mzigo wako.

4: SHIPITO
Link: USA Address & Mail Forwarding Shipito.com | English - Hii pia ni kampuni kongwe ya fowarding na wao gharama zao ni nafuu sana ingawa wanapokea malalamiko mengi sana kutoka kwa wateja wao ukiangalia kwenye forums nyingi.ila kiujumla ni wazuri kwasababu malalamiko ni madogo kulinganisha na ufanisi na pia wanajua na ni wazoefu sana na kazi yao

5: STACKRY
Link: Stackry - US shopping, global shipping - Hii nayo haina tofauti na myus isipokuwa hawa wao hawana kiasi cha kulipia kujiunga nao na wao pia wanakupa option nyingi za kutumia mizigo yako na mabo yao pia ni mazuri kulinganisha na comment wanazopokea kutoka kwa wateja wao. waungwana ni hayo tu niliyo nayo, kazi kwenu ni kufanya utafiti na pia kuangalia na kuchunguza mabo kabla ya kuchukua uamuzi.

STACKRY na BORDERLINX walikuwa recommended sana na wanasifiwa mno angalia hii link -http://tech-vise.com/10-parcel-forwarding-services-for-international-shoppers/ pitia hizo websites na ujionee mwenyewe chagua moja na utazame kama wanakufaa.

HUU NI MTAZAMO WANGU BINAFSI WAKUU , Please evaluate kindly.

Nilikuwa nataka kuonyesha steps ila naona thread haitoshi maana nimeagiza mzigo na nimechukua hatua zote ili mpate kuona ila I think there are limits..

Help Mwl.RCT
nimekutana na forwarding company inaitwa reship, spesheli kwa USA, Canada and UK. Ubora wake hii ipoje?
 
Msaada nataka kununua vitu kwa bei ya jumla alibaba vipi kuhusu uaminifu wa supplier
 
Msaada nataka kununua vitu kwa bei ya jumla alibaba vipi kuhusu uaminifu wa supplier

Alibaba wana kitu inaitwa “Alibaba trade assurance” ambayo kazi yake kuu ni kulinda pesa yako , ubora wa bidhaa , na muda mlokubaliana wa mzigo kukufikia wewe
cha kuzingatia wasiliana nae na mfanye makubaliano humo humo alibaba sio kwenye e-mail au whatsapp namna ya kufanya malipo nenda help center watakuelekeza vizuri kuhusu alibaba trade assurance ili uwe salama zaidi usilipe nje ya humo alibaba
 
Babarazack,
Seller huchagua njia za kuwatumia parcels wateja wake, wapo wanaotoa option kwa njia zote na kumpa uhuru buyer kuchagua njia ipi nafuu na ya haraka kwake, ila wapo baadhi ambao huwa wameweka njia moja tu with no options mfano; unakuta seller amechagua only DHL/FedEx hizi ni very expensive, bidhaa inauzwa 11.99$ lakini shipping fee 120$ by DHL/FedEx took 5-7 days shipments to arrived. So itakubidi kuachana na seller huyo na kutafuta mwenye nafuu unless kama unapesa ya kupoteza!
 
Wakuu kwanaemjua shiping agent yeyote india to tanzania Naomba mawasiliano yake nahitaji kuagiza bidhaa amazoni.in na flipkart lakini jamaa hawaship bongo.
 
nelson15,
Kwanza sikushauri kufanya manunuzi huko yaani Amazon.in or Flipkart hizi Indian-based shopping platforms, ila kwa upande wa Amazon.in unaweza tumia EasybuyAfrica.com hawa wananunua on your behalf, unachotakiwa kufanya ingia kwenye page husika (sio flipkart) copy URL then ingia easybuyafrica.com nenda sehemu ya search then paste ile URL bidhaa itatokea utaichagua kama rangi etc. Pia kuna kipengele cha kukokotoa amount ya pesa mpaka mzigo kufika+ their fees. Shortcomings za kuwa tumia hawa their too expensive, unless ingia Amazon.com maana huku bidhaa zilizopo Amazon US/UK/India zinapatikana!
NB:
Hawa EasybuyAfrica wapo partnership na Vodacom so hakuna ubabaishaji zaidi ya gharama tu, wapo karibia every Vodashop. Ukiona unahitaji maelezo ingia EasybuyAfrica.com utapata maelezo!
 
Alibaba wana kitu inaitwa “Alibaba trade assurance” ambayo kazi yake kuu ni kulinda pesa yako , ubora wa bidhaa , na muda mlokubaliana wa mzigo kukufikia wewe
cha kuzingatia wasiliana nae na mfanye makubaliano humo humo alibaba sio kwenye e-mail au whatsapp namna ya kufanya malipo nenda help center watakuelekeza vizuri kuhusu alibaba trade assurance ili uwe salama zaidi usilipe nje ya humo alibaba
Asante sana
 
Back
Top Bottom