Jihadhari sana kabla hujamkopesha mtu, Kuna wengine kila anayemkopesha anakufa au anapata ugonjwa mbaya sana

Jihadhari sana kabla hujamkopesha mtu, Kuna wengine kila anayemkopesha anakufa au anapata ugonjwa mbaya sana

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Shika neno hili. Kuna mtu ukimkopesha Hela, kila mara unakuwa mtu wa kupoteza simu na mtu msahaulifu.

Mtu mwingine ukimkopesha Hela Yako, anakupeperusha, unajikuta bila sababu yoyote umehamia mbali na eneo la mdaiwa wako.

Mtu mwingine ukimkopesha Hela, unajikuta unaanza kuandamwa na makesi ya ajabu ajabu unaishia jela.

Mwingine ukimkopesha Hela, unaishia kitandani. Utaumwa mpaka basi.

Mwingine ukimkopesha Hela lazima ufe.

Jihadhari sana.

SIRI YA UTAJIRI NI UBAHILI
 
Imani tu... ingawa kukopesha/kukopeshwa kunahatarisha urafiki au undugu wenu.

Kuna watu kwenye kukopa wapo vzr, kurudisha sasa inakuwa kesi, atanuna, ataleta maneno, atakuchukia, na mbaya zaidi atashirikisha watu kuhusu deni lako wakati kipindi anakopa hao watu hakuwaambia.
 
Unaweza ukarogwa kwa pesa yako mwenyewe, kisa unaidai.
 
Mdaiwa ni mtumwa kwa mkopeshaji wake

Usikopeshe mtu unaejua ni ngumu kumdai mf. Kumkopesha mpenzi/mwenza, rafiki wa karibu, ndugu

Ikiwezekana usikopeshe kabisa mtu binafsi vivyohivyo nawe usikope kwa mtu

Usikope kausha damu, app za ovyo ovyo, benki za masharti yasiyoeleweka

NB: kama umetoa ahadi ujue una madeni "Ahadi ni deni"
 
Mikopo imevunja mahusiano mengi hasa undugu na urafiki. Ni kheri kama una uwezo umpe mtu hata robo ya anachokiomba lakini sio kumkopesha maana wengi huwa wapole kwenye kukopa Ila kwenye kurejesha mtihani
 
Mwanzisha thread kakosea anapofungamanisha mikopo na uchawi au imani potofu. Ninachojua mimi ni kuwa kukopa na kukopesha kunatakiwa kusifanywe na watu binafsi bali taasisi zenye kazi hii. Hasa ngozi nyeusi, siyo waaminifu. Wengi tumeshapoteza fedha kwa sababu tu waliokopa walitugeuka.
 
Nakubali kabisaa

Kuna mtu nilimkopesha, kumbe kile kitu alichoweka dhamana kulikuwa cha urithi na kulikuwa na maagano flani hivi (nilikuja kujua baadae) nilipata misuko suko mikubwa kazini nilikaribia kwenye termination. Mkopo ulilipwa nusu, ili mambo yasiwe mengi nikairudisha ile dhamana (bila kujua story behind).
Jamaa akaenda akaikopea kwa mtu mwingine, duu huyo ndio alipigwa bora hata mimi. Alipoenda kwa wataalam kutafuta suluhu ndio akaelezwa. Akarudisha dhamana faster bila kulipwa hata shilingi.
So haya mambo yapo kabisaaa
 
Back
Top Bottom