DOKEZO Jihadhari Sana na Kitu kinaitwa Vodabima. Unaweza Kupoteza Pesa Yako. Ni Mfumo wa Kubahatisha

DOKEZO Jihadhari Sana na Kitu kinaitwa Vodabima. Unaweza Kupoteza Pesa Yako. Ni Mfumo wa Kubahatisha

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
7,840
Reaction score
18,115
Sijui ni wangapi wamewahi kukumbana na na matatizo ya vodabima.

Kwa uzoefu wangu, mara tatu imetokea unalipa bima ya gari kupittia vodabima. Unapata ujumbe kuonesha pesa imetoka kulipia bima ya gari fulani kuanzia kipindi fulani mpaka kipindi fulani, hakuna ujumbe mwingine. Kwenye mfumo wa kuangalia bima za magari, haioneshi umelipia, unawasiliana na kampuni yako ya bima, wanasema hawajapokea malipo, unaenda ofisi za vodacom, ni hadithi tu!

Mara jaza fomu upate printout ya kupeleka kampuni ya bima, mara tutakurudishia pesa yako, lakini mwisho wa yote, hakuna kitu! Umepoteza pesa uliyolipia bima, utalipishwa fine za barabarani kuwa gari halina bima, n.k.

Naona mabenki nao wameanza kutoa huduma za bima, kama mawakala. Sijui kama wao watakuwa bora zaidi ya hawa vodabima! Vodacom kwenye masuala ya bima, bado sana. Hawajajipanga.
 
Kuna mtu pia aliwahi kulalamika vodabima ya afya. Alilipa na ndugu yake akaumwa akalazwa alikoma!
 
Sijui ni wangapi wamewahi kukumbana na na matatizo ya vodabima.

Kwa uzoefu wangu, mara tatu imetokea unalipa bima ya gari kupittia vodabima. Unapata ujumbe kuonesha pesa imetoka kulipia bima ya gari fulani kuanzia kipindi fulani mpaka kipindi fulani, hakuna ujumbe mwingine. Kwenye mfumo wa kuangalia bima za magari, haioneshi umelipia, unawasiliana na kampuni yako ya bima, wanasema hawajapokea malipo, unaenda ofisi za vodacom, ni hadithi tu! Mara jaza fomu upate printout ya kupeleka kampuni ya bima, mara tutakurudishia pesa yako, lakini mwisho wa yote, hakuna kitu! Umepoteza pesa uliyolipia bima, utalipishwa fine za barabarani kuwa gari halina bima, n.k.

Naona mabenki nao wameanza kutoa huduma za bima, kama mawakala. Sijui kama wao watakuwa bora zaidi ya hawa vodabima! Vodacom kwenye masuala ya bima, bado sana. Hawajajipanga.

Haya ya Vodabima upande wa Motor-vehicle Insurance; nilipata lawana sana kutoka kwa mtu ambaye alitaka Third Part Cover.

Kwa kuwa nilikuwa na hela kwenye M-PESA nikaona nitoe msaada, Kweli nikalipia ile Insurance maisha yakaendelea.

Siku moja saa 6.30 usiku napokea simu jamaa ananiambia kwani ile BIMA ulilipa miezi mitatu? Nikamwambia nakumbuka kabisa kuwa nilikutumia meseji ya malipo na confirmation. Lakini pia tuliingia kwenye mtandao wa TIRA na kuonyesha kuwa insurance cover ni ya mwaka mzima.

Ikabidi nitoke niende polisi maana jamaa alikuwa na majanga yake, polisi wakacheki BIMA wakakuta gari haina BIMA. Nikatoka na ushahidi wangu na kuelekea polisi.

Bahati nzuri wale Polisi walikuwa na muda wa kukusikiliza hivyo tatizo likaisha nikamwacha jamaa akapambane na VODA.

Sijui aliishia wapi lakini hizi case ni nyingi.
 
Nimekata mwezi uliopita kupitia hao vodabima, nilikata Britam Insurance na kuingia TIRAMIS kufanya verification, bima iko active na hakuna shida yoyote.
 
Voda ni magwiji wa utapeli kuanzia biashara yao ya hisa hadi biashara zingine zinazoibuka na trends.
 
nje ya mada naomba kuuliza hivi naweza kukata bima ya afya na sio mfanyakazi je shirika lipi zuri kwa bima ya afya ? na kuhusu ada zao za bima zipoje ? cc min -me Dr am 4 real PhD
Unaweza.
NHIF uwe na NIDA. Haina ukomo wa umri.

Private ni Strategies, Britam, Jubilee na wengineo. Ukiwa na umri zaidi ya miaka 60 wanakukataa.

NSSF. Hii unajiunga kuwa mwanachama wa hiari. Shida yake unatakiwa kuchaguwa hospitali moja tu ya kutibiwa. Hospitali nyengine hadi upate rufaa.
 
Hapo ni tatizo ni ni weak coordination kati ya mfumo wa malipo na kampuni za bima.
 
Wacha niendelee kuishi kizamani aiseee....

Mimi ada hua naenda kulipia bank dirishani nachukua stakabadhi nascan kisha natia kwenye mail na kutuma shuleni.

Bima ya gari hua naenda kwenye ofisi za bima dirishani nalipia napewa stakabadhi kisha napata ujumbe kwenye sim, then nasepa.

Viatu na nguo hua nafunga safari naenda kununua ninacho kiona sio online tafadhali....

Demu mpya hua simtumii pesa hadi aje location ninuone kwa macho hata kama sijamkula, nampa cash anapita vile...

Kwakweli minaona bora niendelee na huu ukale ili nisije kwazika please...
 
Back
Top Bottom