Sasa angalia hapa dar, pamoja na joto loote hili kondakta na dereva wa daladala wanaambiwa wavae suti.Hali ya hewa ya Arusha ni rafiki sana kwa aina zote za nguo. Sasa hili joto la Dar watu wataacha kuwa wachafu? Hata ukitaka nguo nzuri, viatu, makoti Arusha ndio kila kitu, kila ninapoenda Arusha lazima nirudi na mikato
Ndio maaana nimeoa arushaNimetembea Dar, Mwanza, Mbeya, Dodoma, Tanga na Arusha yenyewe ambako kuna yanayoitwa majiji ya nchi yetu, niseme tu watu wa jiji la Arusha wanaongoza kwa unadhifu na usafi wa binadamu na mazingira.
Yani hata ukipanda daladala (wenyewe wanaita hiace/Haisi) za Arusha harufu ya kwenye daladala unayoipata ni ya manukato mazuri, hata makondakta wao ni nadhifu wakiwa na nguo nzuri na safi.
Sehemu nyingi pia za umma za biashara wanajitahidi sana kufanya usafi na kuweka mazingira katika hali nzuri.
Halafu wengi ni wenyeji wa manyara na singida chunguza😁Hao ndio wanazingua na maviatu yao makubwa ya ajabu ajabu kama wehu.