ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 83,659
- 90,151
Kwa mara ya kwanza katika Historia Jiji la Dodoma limepindua meza na kuwa Kimbilio la Biashara ya makazi yaani real estates.
Dom ndio Jiji linajengwa Kwa kasi makazi ya kuishi na biashara kiasi kwamba bei ya kupanga chumba Cha duka Dom ni kubwa kuliko Dar.
View: https://youtu.be/M4wpaMmLVns?si=3S0eyNuXYkSs-eak
=============
Dodoma, mji mkuu wa kiutawala wa Tanzania, inaendelea kubadilika kwa kasi na kuwa kitovu kikubwa zaidi cha uwekezaji wa majengo ya biashara nchini.
Takwimu mpya za uchumi zinaonyesha kuwa soko la majengo ya biashara jijini Dodoma linaongozwa na ongezeko kubwa la kodi za upangishaji, kiwango cha juu cha matumizi ya majengo yaliyopo, pamoja na upungufu mkubwa wa nafasi za biashara, hali inayobadilisha kwa kiasi kikubwa mazingira ya uwekezaji wa sekta ya majengo katika Afrika Mashariki.
Kwa mujibu wa Ripoti ya Utulivu wa Mfumo wa Fedha ya Desemba 2025 ya Bank of Tanzania, wastani wa kodi ya ofisi jijini Dodoma umefikia kati ya Sh30,000 na Sh35,000 kwa mita ya mraba.
Kiwango hiki kinaifanya Dodoma kuwa soko la gharama kubwa zaidi la ofisi nchini, ikiiweka mbele ya Dar es Salaam, kitovu cha jadi cha biashara, ambako kodi ya ofisi za hadhi ya juu ni kati ya Sh25,000 na Sh30,000 kwa mita ya mraba.
Miji mingine ya kibiashara kama Arusha na Mwanza ina viwango vya kodi kati ya Sh20,000 na Sh25,000 kwa mita ya mraba, huku Mbeya ikiwa na wastani wa Sh10,000 kwa mita ya mraba.
View: https://youtu.be/t7Ox-qgLeOg?si=nhRprVPt2-yJAw9u
My Take
Dom imesanufiwa kuwa Jiji la Biashara na makao Makuu ya Nchi kama Nairobi,Lilongwe au Johannesburg.
Ndani ya miaka 25 kutoka Sasa yaani 2050 Dar itakuwa kama Mombasa na Dodoma kuwa kama Addis Ababa.
Serikali ilipo ndipo Kuna pesa.Tumeona Nguvu ya Serikali Sasa ni wakati wa kujenga Miji mikuu Kila Kanda Ili kuwa vitovu vya Uchumi kwenye Kanda husika na Hilo Serikali inaweza ikiamua.
Mwanza -Kanda ya Ziwa
Kigoma- Kanda ya Magharibi
Mbeya-Kanda ya Nyanda za Juu Kusini
-Mtwara -Kanda ya Kusini
-Dar & Pwani -Kanda ya Mashariki
-Arusha-Kanda ya Kaskazini
-Dom-Kanda ya Kati na Mji Mkuu.
Kumekucha Dom 👇👇
View: https://www.instagram.com/p/DZcu6x2DH3I/?igsh=MmFxeHkwMnR4eDZm