Jiji la Dodoma Laipiku Dar na Kuwa Kimbilio la Biashara ya Kupangisha Nyumba za Kuishi na Biashara (Frame)

Jiji la Dodoma Laipiku Dar na Kuwa Kimbilio la Biashara ya Kupangisha Nyumba za Kuishi na Biashara (Frame)

Dodoma inakuwa kwa kasi, ila hapo pa Dar kuwa kama mombasa na Dom kuwa kama Addis Ababa ni ndoto, ingawa sipapendi Dar na nilisha hamisha makazi ila Dom kuipuku Dar bado na labda siku Dodoma ikiota bahari yake ya dodoma
Nimeamia mwenyewe dodoma kutoka Ziwa
 
Kwa mara ya kwanza katika Historia Jiji la Dodoma limepindua meza na kuwa Kimbilio la Biashara ya makazi yaani real estates.

Dom ndio Jiji linajengwa Kwa kasi makazi ya kuishi na biashara kiasi kwamba bei ya kupanga chumba Cha duka Dom ni kubwa kuliko Dar.
=============
Dodoma, mji mkuu wa kiutawala wa Tanzania, inaendelea kubadilika kwa kasi na kuwa kitovu kikubwa zaidi cha uwekezaji wa majengo ya biashara nchini.

Takwimu mpya za uchumi zinaonyesha kuwa soko la majengo ya biashara jijini Dodoma linaongozwa na ongezeko kubwa la kodi za upangishaji, kiwango cha juu cha matumizi ya majengo yaliyopo, pamoja na upungufu mkubwa wa nafasi za biashara, hali inayobadilisha kwa kiasi kikubwa mazingira ya uwekezaji wa sekta ya majengo katika Afrika Mashariki.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Utulivu wa Mfumo wa Fedha ya Desemba 2025 ya Bank of Tanzania, wastani wa kodi ya ofisi jijini Dodoma umefikia kati ya Sh30,000 na Sh35,000 kwa mita ya mraba.

Kiwango hiki kinaifanya Dodoma kuwa soko la gharama kubwa zaidi la ofisi nchini, ikiiweka mbele ya Dar es Salaam, kitovu cha jadi cha biashara, ambako kodi ya ofisi za hadhi ya juu ni kati ya Sh25,000 na Sh30,000 kwa mita ya mraba.

Miji mingine ya kibiashara kama Arusha na Mwanza ina viwango vya kodi kati ya Sh20,000 na Sh25,000 kwa mita ya mraba, huku Mbeya ikiwa na wastani wa Sh10,000 kwa mita ya mraba.

View: https://youtu.be/t7Ox-qgLeOg?si=nhRprVPt2-yJAw9u

My Take
Dom imesanufiwa kuwa Jiji la Biashara na makao Makuu ya Nchi kama Nairobi,Lilongwe au Johannesburg.

Ndani ya miaka 25 kutoka Sasa yaani 2050 Dar itakuwa kama Mombasa na Dodoma kuwa kama Addis Ababa.

Serikali ilipo ndipo Kuna pesa.Tumeona Nguvu ya Serikali Sasa ni wakati wa kujenga Miji mikuu Kila Kanda Ili kuwa vitovu vya Uchumi kwenye Kanda husika na Hilo Serikali inaweza ikiamua.

Mwanza -Kanda ya Ziwa
Kigoma- Kanda ya Magharibi
Mbeya-Kanda ya Nyanda za Juu Kusini
-Mtwara -Kanda ya Kusini
-Dar & Pwani -Kanda ya Mashariki
-Arusha-Kanda ya Kaskazini
-Dom-Kanda ya Kati na Mji Mkuu.

Hujui unachoongea wewe kilaza, kama Dodoma kunajengwa zaidi kuliko Dar bei za kupangisha haziwezi kuongezeka na kuwa kubwa badala yake zitashuka chini.
 
Mkuu ukiwa na akili ndogo jiweke pembeni wengine wafikirie kwa ajili yako.
Dodoma kuna uhaba wa nyumba hilo halina ubishi maana wafanyakazi wengi wa serikali wanahamia huko.
Mind you WAFANYAKAZI!
Hata Katibu Mkuu wa wizara ni mfanya kazi.
Purchasing power yao ikoje?
Purchasing power ya mfanyakazi inajulikana na ina limit.
Na mzunguko wa pesa ukoje
Business centres Dodoma zenye high turnover ziko wapi
Dodoma kuna viwanda venye ajira nyingi?

Hebu jiulize hayo maswali kwa kuanzia halafu jijibu mwenyewe.
Nyie washika mabango mna matatizo sana.
Nakazia kwa nguvu

Zingatia sentensi "nyie washika mabango mna matatizo sana" 🔥🔥
 
Kwa mara ya kwanza katika Historia Jiji la Dodoma limepindua meza na kuwa Kimbilio la Biashara ya makazi yaani real estates.

Dom ndio Jiji linajengwa Kwa kasi makazi ya kuishi na biashara kiasi kwamba bei ya kupanga chumba Cha duka Dom ni kubwa kuliko Dar.
=============
Dodoma, mji mkuu wa kiutawala wa Tanzania, inaendelea kubadilika kwa kasi na kuwa kitovu kikubwa zaidi cha uwekezaji wa majengo ya biashara nchini.

Takwimu mpya za uchumi zinaonyesha kuwa soko la majengo ya biashara jijini Dodoma linaongozwa na ongezeko kubwa la kodi za upangishaji, kiwango cha juu cha matumizi ya majengo yaliyopo, pamoja na upungufu mkubwa wa nafasi za biashara, hali inayobadilisha kwa kiasi kikubwa mazingira ya uwekezaji wa sekta ya majengo katika Afrika Mashariki.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Utulivu wa Mfumo wa Fedha ya Desemba 2025 ya Bank of Tanzania, wastani wa kodi ya ofisi jijini Dodoma umefikia kati ya Sh30,000 na Sh35,000 kwa mita ya mraba.

Kiwango hiki kinaifanya Dodoma kuwa soko la gharama kubwa zaidi la ofisi nchini, ikiiweka mbele ya Dar es Salaam, kitovu cha jadi cha biashara, ambako kodi ya ofisi za hadhi ya juu ni kati ya Sh25,000 na Sh30,000 kwa mita ya mraba.

Miji mingine ya kibiashara kama Arusha na Mwanza ina viwango vya kodi kati ya Sh20,000 na Sh25,000 kwa mita ya mraba, huku Mbeya ikiwa na wastani wa Sh10,000 kwa mita ya mraba.

View: https://youtu.be/t7Ox-qgLeOg?si=nhRprVPt2-yJAw9u

My Take
Dom imesanufiwa kuwa Jiji la Biashara na makao Makuu ya Nchi kama Nairobi,Lilongwe au Johannesburg.

Ndani ya miaka 25 kutoka Sasa yaani 2050 Dar itakuwa kama Mombasa na Dodoma kuwa kama Addis Ababa.

Serikali ilipo ndipo Kuna pesa.Tumeona Nguvu ya Serikali Sasa ni wakati wa kujenga Miji mikuu Kila Kanda Ili kuwa vitovu vya Uchumi kwenye Kanda husika na Hilo Serikali inaweza ikiamua.

Mwanza -Kanda ya Ziwa
Kigoma- Kanda ya Magharibi
Mbeya-Kanda ya Nyanda za Juu Kusini
-Mtwara -Kanda ya Kusini
-Dar & Pwani -Kanda ya Mashariki
-Arusha-Kanda ya Kaskazini
-Dom-Kanda ya Kati na Mji Mkuu.


Tatizo dodoma hakuna majengo ya office ya kutosha, HIVYO KINACHOPANDISHA BEI NI UCHACHE WA BIDHAA
Ikitokea muwekezaji akaweka majengo matano tu ya floor 20 utashangaa bei imeshuka hadi 1500 kwa mita.
Dar maofisi ni mengi pengine mara tano ya dodoma lakini majengo yana reflect wingi wa maofisi
 
Ila wanachonifurahisha madalali wa dodoma. Bei za viwanja sijui wanakokotoa kwa njia ipi kosa lisiwe kuna majiran wamejenga jenga vijumba viwil vitatu utalisikia good neighbourhood uliza bei sasa sqm 450 anakwambia mil 18. Dodoma kukiwa na majiran na nyumba mbil tatu kosa
 
Ni mchumi pori huyu, nyuzi zake karibia zote za biashara na uchumi ni maboko matupu na AI slops. Mtu anaamini kabisa Dodoma ambayo GDP ya mkoa mzima haifikii hata Wilaya moja ya Dar inaweza kuipita Dar kiuchumi!
Sometimes wanazingua sana hawa machawa. Kama Dar private sector sasahivi inajenga vitu kama hivi, utaanzaje kufananisha na Dodoma ambayo majengo mengi ni ya serikali.

Private sector Dodoma ndio imeanza kukua hivi karibuni wakati Dar imeshafika mbali sana kwenye sekta binafsi
Muda si mrefu tumeona hapa EACLC imejengwa Ubungo. Maeneo kama Masaki kila siku zinajengwa apartment mpya
Mleta mata huenda anafananisha Dodoma na Mbagala kwa hiyo anaona Dodoma inajengeka kwa kasi
 
Back
Top Bottom