Jiji la Dodoma ni chafu!

Okay iko wapi ya kuwatosha wote hao....
Mbona wa dar na Arusha hawakupewa nafasi hiyo ya kusubiri
Halmashauri ya Dodoma iliamua kujenga kwa mapato ya ndani. Arusha na Dar wangetaka wangejenga ya kwao.
 
Dar es salaam ndio jiji kongwe na kubwa katika eneo hili, Dodoma ndio inajengwa tena kwa masterplan iliyobuniwa miaka ya sabini, kwanza na sasa baada ya msukumo wa awamu ya tano tunategemea kuona usasa zaidi!, lakini bado Dodoma inapwaya. Angalau basi tungeona mabanda yaliyojaa pale njia nne yakiondolewa kupisha kitu kinachofanana na mji wa kisasa.... Hola!!. Uchafu kwa Dodoma haupaswi kuwa jambo la kujifunza kutoka Dar es salaam au kwingine kokote kuliko na vijiji vikubwa... Dodoma inatakiwa kuwa ya mfano katika nyanja zote zinazotafsiri hadhi ya kuitwa jiji.
 
Muogope Mungu ndugu yaani ufananishe China Plaza na zile mbao zilizojazana nje ya msikiti wa Gadafi kweli? Kwa idadi ya watu sikatai kkoo watu nyomiii ila haikeri km pale mpangilio mbovu sana tena sana
 
Tatizo Watanzania wengi wanalala kwenye store ndio maana sishangai watu kutetea uchafu na u hovyo hovyo. Msingi wa mleta mada ni kwamba tulifanya makosa Dar tukategemea tutarekebisha jiji la Dodoma lakini huko nako tunarudia makosa yale yale.

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Nyie watu mna akili ndogo sana. Makosa yaliyofanyika Dar hayatakiwi kujirudia Dodoma. Km tu hivi sasa Dodoma ina idadi ndogo ya watu tayari kuna dalili za kuelemewa na uchafu vp kwa miaka michache ijayo. Ni lazma serikali iweke mipango mikali ili lengo la kuhamia Dodoma liwe na maana,la sivyo kutakuwa hakuna maana yoyote!

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Sawa Akili kubwa..Nyie watu kujua ndio hovyo kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…