Jiji la Dodoma ni chafu!

Jiji la Dodoma ni chafu!

Ungechukua koleo, fagio, chepe upige usafi uwaoneshe usafi unavyotakiwa fanywa

Ova
 
Dodoma ingetakiwa iwe safi na kpangiliwa vizuri sana kulinganisha na Dar ambapo palikosewa mifano ka majiji mengine yaliyohsmishwa kama Abuja, Yamasoukro, Pretoria
Dodoma ilianza vizuri kwa mpangilio na ilikopi mji wa Lilongwe Malawi ambako enzi hizo CDA walikuwa wakienda kuangalia mpangilio wa maeneo na ujenzi wa nyumba, kwenye ujenzi vifaa vya ujenzi vilikuwa havitozwi ushuru hivyo vilikuwa vikitoka ulaya vinapelekwa Dodoma bila ushuru na bei ilikuwa ya chini sana, lakini viongozi wa CDA wakaanza kuviiba na kuvipeleka Dar kuviuza kwa bei kubwa, serkali ilipowakamata ikaondoa mpango huo na kuivunja CDA. Ilipoivunja CDA ramani yote ya mpangilio ikasambaratishwa watu wakaanza kupimiwa viwanja ndani ya maeneo yaliyojengwa mfano kituo cha mafuta Shabibby na Area C na D ndiyo ukawa mwisho wa ustaarabu na bustani ya CDA kwa ajiri ya kupanda miti na maua ya kulipendezesha jiji ikafa.
 
Jiji lina harufu ya Nnya balaaaaaaaaaa
Nenda mitaa ya kati utaziba pua mwenyewe kmmqe,ukija mitaa ya chako ni chako ndio utakimbia,yaani full Inyeeeee gwedegwedeee
 
Majiji yote yanasafisha kisehemu ambacho mkubwa anaweza kupitia ila pembezoni ni uswazi. Dar ni safi asubuhi Hadi saa tisa. Saa kumi Hadi asubuhi mh.Makala akienda kulala Machinga na mama ntilie wanaingia na zana zao kuchafua.
 
Acha tu. Mifumo ya majitaka sijui imeharibika?
 
Majiji yote yanasafisha kisehemu ambacho mkubwa anaweza kupitia ila pembezoni ni uswazi. Dar ni safi asubuhi Hadi saa tisa. Saa kumi Hadi asubuhi mh.Makala akienda kulala Machinga na mama ntilie wanaingia na zana zao kuchafua.
Kama nchi tunatakiwa tuweke mifumo madhubuti. Usafi sio kutoka tu na mifagio eti tunafagia lakini baadae uchafu unarudi palepale.
 
Jiji la Dodoma ni lichafu. Barabara zimejaa udongo na matope utafikiri hazijawekwa lami. Tope kama tuko shambani jamani. Mvua imenyesha kidogo maji yamekwama kwenye barabara hamna proper drainage system. Pembezoni mwa barabara hapajasakafiwa vizuri au kuoteshwa majani ili kuzitunza barabara hizi.Kingo zake zinameguka kila kukicha.

Taka hazijazolewa muda mrefu. Niliona zikizolewa mara moja tu kwa kutumia yale magari ambayo yako wazi(Suma jkt) yakipita mji mzima unanuka.

Sokoni ndio usiseme. Masoko yote Dodoma ni mabaya. Watu wapo ofisini hawawajibiki. Wanasubiri nini?

Maeneo ya Uwanja wa Jamhuri kumejazwa mbao kila mahali ule msikiti wa Gaddafi umezibwa hauonekani. Mbao zinafanyanini barabarani? Hivi nyie viongozi mnaakili kweli? Mji mchafu
sana.Maafisa mazingira kazi yenu imewashinda.

Ccm wana mirunda ina bendera zao jiji zima utafikiri kichaa ndio amesimika. Kiufupi ni uchafu. Mnashindwa kuweka kitu chenye mvuto?

Mkurugenzi, jiji limekushinda. Wewe na mkuu wa mkoa kazi yenu kuropoka tu hamna mikakati. Jiji gani hili?
Pachafu mno.
Wiki chache nyuma nilipita pale sabasaba stand ya daladala aisee panatia kinyaa.
Hata sehemu ya kukanyaga haipo
 
Huko Sabasaba ndio mwisho wa maelezo. Ni kubaya sana watu wanapanga bidhaa karibia na tairi za basi. Tope ndio usiseme. Utafikiri wanaotumia stendi ni vichaa.
 
Mwaka jana nilishuka Dodoma saa sita usiku ... Kwa kweli Dodoma bado sana, inafaa kuitwa kijiji kikubwa kichafu... kufanya usafi tu ni mgogoro!. Ndio maana Hangaya kutwa kucha kiguu na njia kuelekea Pwani. Usiku huo huo niliamua kuendelea na safari kwa magari ya IT... Itaichukua Dodoma miaka zaidi ya 20 kuwa angalau sawa na Dar es salaam ya sasa.
 
Si lazma majiji yote Tz yafanane na Dar. Dar inamakosa mengi yaliyofanyika na Dodoma haina hayo makosa. Pamoja na shida zote bado Dodoma inakuwa kwa kasi lakini viongozi wanataka kukwamisha hatua zisiendelee kupigwa. Tatizo kuu kwa sasa likiwa uchafu.
 
Jiji la Dodoma ni lichafu. Barabara zimejaa udongo na matope utafikiri hazijawekwa lami. Tope kama tuko shambani jamani. Mvua imenyesha kidogo maji yamekwama kwenye barabara hamna proper drainage system. Pembezoni mwa barabara hapajasakafiwa vizuri au kuoteshwa majani ili kuzitunza barabara hizi.Kingo zake zinameguka kila kukicha.

Taka hazijazolewa muda mrefu. Niliona zikizolewa mara moja tu kwa kutumia yale magari ambayo yako wazi(Suma jkt) yakipita mji mzima unanuka.

Sokoni ndio usiseme. Masoko yote Dodoma ni mabaya. Watu wapo ofisini hawawajibiki. Wanasubiri nini?

Maeneo ya Uwanja wa Jamhuri kumejazwa mbao kila mahali ule msikiti wa Gaddafi umezibwa hauonekani. Mbao zinafanyanini barabarani? Hivi nyie viongozi mnaakili kweli? Mji mchafu
sana.Maafisa mazingira kazi yenu imewashinda.

Ccm wana mirunda ina bendera zao jiji zima utafikiri kichaa ndio amesimika. Kiufupi ni uchafu. Mnashindwa kuweka kitu chenye mvuto?

Mkurugenzi, jiji limekushinda. Wewe na mkuu wa mkoa kazi yenu kuropoka tu hamna mikakati. Jiji gani hili?
Uongo....unawasingizia watani zangu. Kwanza sasa hivi mvua zimesimama hayo matope yanatoka wapi.
 
Hatupingani nae mkuu.. tatizo ni kweli lipo lkn sio kwa ukubwa wa namna hiyo.. hebu nitajie miji ambayo haina changamoto ya uchafu tz hii.. then niambie kuna mji unaongoza kwa uchafu na harufu mbaya kuzidi Dsm?? Kama kigezo ni hicho unachosema wewe basi na dsm hastahili kabisa kuwa Jiji..
Mtoa mada hajatoa ulinganifu wowote ispokuwa ametoa kero yake. Shughulikieni
 
Back
Top Bottom