Uchaguzi 2020 Jiji la Mbeya, Hata kama mnampenda Mbilinyi (Sugu) msimchague. Ili mpate maendeleo chagueni CCM

Uchaguzi 2020 Jiji la Mbeya, Hata kama mnampenda Mbilinyi (Sugu) msimchague. Ili mpate maendeleo chagueni CCM

Ndo shida kubwa ya wapinzani uchwara.wanatangaza demokrasia ila kwa matendo hawaipendi.ukipingana nao kimawazo wanakutukana.badala kupishana kwa mawazo.

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO CHADEMA
Moja ya msingi wa Demokrasia ni uhuru wa kutoa maoni. Sasa nashangaa mimi nimetoa maoni wewe unitukania ukoo wangu mzima. Wengi hatuipendi CCM ila kwa akili kama zako ukiwa kama mpinzani basi tunakosa mbadala wa CCM. Lazima itawale tu
 
Nachoongea ni uhalisia na wala sio ushabiki kama wenu.
JE UNAJUA CCM inaungwa mkono na kundi lipi la watu.?

Kundi la watu wa vyombo vya dola na wale walio katika ulaji.
 
mto post n mwehu sana,kawadanganye wehu wenzio sasa kama ccm inaleta maendeleo majimbo haya toka nchi ipate Uhuru yapo chin ya ccm lkn hakuna maendeleo,nakutajia machache:Songea,peramiho,Mbinga,tunduru,Dodoma na wilaya Zeke Lind kwa wazir Mkuu,jimbo la Nape nauye,tabora,rukwa,kilolo,jimbo la lukuvi hili toka hata mbunge hajawahi badilishiwa lkn mpaka Leo hii halina maji safi,mafinga,iringa vjjn singida,na vitongoji vyake tanga na vitongoji vyake hayo n majimbo machache tu ambayo yako chini ya ccm na ni majimbovmabov haija wahi tokea sasa utasemaje ccm inaleta maendeleo umesha ona wote n mambugila wa kutudanganya? Nanyi wabunge wa upinzan mnapoenda majimbon kwenu ongeen kwa mifano ktk majimbo yote ambayo yako chin ya ccm kwa idadi kuliko kuongea kwa nadharia! Hawa ccm mkiongea kwa nadharia mtapigwa nao n wajanja sana namna ya kucheza na akili za watanzania. Wabunge wa upinzan nawashaur tena mkiongea kwa nadharia ktk kipind hch bila takwimu mtapigwa na ccm na kubaki kulalamika,ccm wanatumia uelewa mdo wa wananchi huko vjijin kuwachakaza
 
Mimi naongea haya kwa moyo safi. Nimetoka Mbeya jana. Mara nyingine kabla ya jana nilienda Mbeya mwaka 2018.

Leo hii baada ya ziara ya Mh.Rais Jijini Mbeya na kusuluhisha mambo yake na Wanamkoa huo ndo mambo yameanza kubadilika.angalau sasa barabara zinajengwa na maendeleo mengine.

Jiji la Mbeya lilisuswa toka 2015 na ni kutokana na misimamo yao ha hovyo dhidi ya CCM na Mh.Rais. kitu ambacho kilimkwaza sana Mh.Rais na yeye akaamua kulisusa jiji hilo ili kuwakomoa wananchi wanaojifanya wao wana Dunia yao.

Ushauri wangu:
Ili Jiji la Mbeya liendelee msimchague Joseph Mbilinyi. Mtasababisha matatizo mengine kwa jiji hilo.kwa saza wekeni maendeleo mbele.Sugu mnaweza mpatia kazi nyingine lakini si ubunge.

Kama mnampenda sana hata mumpatie cheo cha kaka wa Mwanjelwa but si ubunge. Chagueni mtu ambaye anakubalika na CCM.Ili sasa matakwa yenu yafike mbele ya Rais kwa urahisi na kufanyiwa kazi.

Mwaka 2020 bado Rais ni John P. Magufuli hilo linaeleweka. Sasa tumieni nafasi hii kwa mambo ya maendeleo.

Raisi amechaguliwa kuongoza nchi au. Yanni Mbeya leo chakula wanacholima nacho kilishe Chadema tu. Mbeya chagueni mtu wenu bila kujali chama hakuna ambaye alikuwa anawajali miaka yote ya CCM kama ni maendeleo yalikuwa yanasubiri upinzani wachukuwe jimbo! miaka yote kabla ya Sugu kwanini hakukuwa na maendeleo hayo. Magu anaondoka baaada ya miaka mitano atakuja mwingine na yake yeye anaweza akawa hajali chama ni mkanda, au mkabila. Mtu yeyote ambaye ni mchama zaidi ya maendeleo utakuta ni mkabila au mkanda. Magu ataondoka tu muda unaenda haraka hata weza kufanya kitu cha maana kwa miaka 4 tu. Kama ni kilimo huwezi kukwepa mkoa wa Mbeya ! Je hizo sehemu za CCM mbeya zinaendelea? sasa na huko tatizo ni Chadema?
 
Mbona Moshi wamechagua Chadema zaidi ya miaka 20 wana maendeleo?
 
Hata kwenye ranking ya kipato, Mbeya ipo juu sana kushinda Mwanza, Geita na Dodoma. Sasa sijui kama unaelewa maana ya maendeleo.

Mikoa inayoongoza kwa maendeleo ya kipato:

1) Dar
2) Kilimanjaro
3) Njombe

Hakuna hata mkoa mmoja ambao ni ngome ya CCM ambao una maendeleo ya watu.

Mikoa inayochukiwa ndiyo inayopiga hatua zaidi kwenda mbele. Wanaofikiria watawala watawaletea maendeleo, watasubiri sana.
 
"Maendeleo hayana vyama". Hii kauli naisikia sikia sana kutoka kwa watawala.
 
Ni lini Watanzania tutakuwa na timamu. Maendeleo yoyote ya nchi huletwa na wananchi wenyewe kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo mfano wa wadau ni serikali ya hao wananchi hiki chombo hukusanya hela za wananchi pamoja kwa naiaba ya hao wananchi kisha kuzipeleka tena kwa hao wananchi kulingana na umuhimu eneo husika ambao hao wananchi wanaishi. Wadau wengine ni mashirika ya fedha ya ndani na ya kimataifa, na mashirika mengine kama ya dini. Serikali haina uwezo wa kutuletea maendeleo maendeleo tunaleta sisi wananchi kupitia kodi na michango mabalimbali ambazo serikali ni wakala wetu sisi wananchi tumeipa dhamana ya kuzikusanya pamoja kwaajili ya maendeleo yetu.
Kwa wale vilaza ambao huamini serikali ndio huleta maendeleo basi kupitia mchango huu ninaoutoa wawe wapewa akili mudao utakapomaliza kuusoma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom