Uchaguzi 2020 Jiji la Mwanza lasimama usiku kwa ujio wa Tundu Lissu - Septemba 25

Tuwe wakweli hivi nyomi hili linazidi kweli enzi za lowasa Mimi naamini Kama lowasa hakupita kwa nyomi ile sidhani Kama TL atapita sasa

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
Point of correction alishinda uchaguzi lakini hakutangazwa mshindi, na yeye kwa kuwa hakuwa mtata akaamua kupotezea na kutokana na makandokando yake mengi mwishowe akarudi alikolelewa.
Safari hii Chadema tuna chuma cha pua, taarifa kwa wezi wote wa kura kaeni mkijua ama zetu ama zenu.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Mzee yule anapoketi kuangalia nyomi La lissu YouTube nahisi kila muda wanamuokota kazima chini kwa kupaniki.
Wana mwambia za mwaka juzi utadhani mwaka juzi kulikuwa na uchaguzi😂
 
Mimi pia ni chadema mkuu lakini naona majamaa yatapiga ukanjanja wao kwenye kutangaza mshindi na sipendi Vita itokee kwenye hii nchi

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 

Polepole yuko wapi maana hii kitu haivumiliki kabisa. Serikali ni ya ccm, polisi ni wa ccm, mkuu wa mkoa ni wa ccm, sasa inakuwaje hawa wapinzani wanapeta hivi. Sabaya yuko wapi? Maana kule haialiwaandaa vibaka kufanya vurugu, je na hawa wameandaliwa pia?

Hili ni somo tosha kwamba wananchi wanalao moyoni, wamechoka kunyanyaswa na serikali ya ccm. Sanduku la kura linaweza toa matokeo ambayo yatawashangaza wengi. Tuwe tayari kulinda kura na ushindi wetu.
 
Hali kama hii inaonyesha dhahiri sera za Jiwe na chama chake zimefeli,flyover,ndege,reli,Stiegler dam,bado havijalipa havipo kwenye mioyo ya watu Mwl.Nyerere alishawahi kusema wananchi tujihadhali sana na maraisi wanaopenda maendeleo ya vitu na sio watu.Acha akaangwe kwa mafuta yake option yao iliyobaki ni kuiba kura tuu shime tulinde kura zetu wajameni pote mlipo wapigakura.
 
Amiiiini!
 
Labda kwa wizi.
Nyie hamuwajui Watanzania mnadanganywa na mihemko ya kisiasa ya kikundi cha watu,sasa ngojeeni October 28 ndio mtajua hamjui Watanzania walivyo.

Watanzania wanaimani kubwa na CCM na hii haitafutika hivi karibuni.
 
A European not an European

Be not fooled by letter "E" at the beginning of that word.

Hahaha! Umenikumbusha mbali sana.

Article "an" inatumika mwanzoni mwa maneno na majina yanayoanza na au kutamkwa mwanzoni na herufi za vowels yaani a e i o u.

Neno "European" linaanza na herufi "e" na linatamkwa "uropian'.

Yaani neno "European" siyo tu linaanza na herufi "e" bali pia linatamkwa kwa kuanza na herufi "u" ambazo zote ni vowels na lazima utamkapo uanze na article "an".

Kuna maneno mengine mfano "hour" linatakwa [our] "heir"[ea] nk japo yanaanza na herufi "h" matamshi yake herufi "h" haifanyi kazi na badala yake vowels "o" na "e" ndizo husimama mwanzoni kwa hiyo ni lazima article "an" iwepo mwanzoni.

Kwa hiyo, ni sahihi ukisema "an hour" eg half an hour before

"An heir" eg he is an heir of the deceased.

"An European" eg It is an European Union.
 

Psychologically, umetumia lugha kali Kwanza kuonyesha mapenzi yako kwa CCM, chuki kwa CHADEMA lakini pia lugha na maneno makali uneyatumia ili kuficha ukweli kwamba watu walikesha.

Ingekuwa ni uongo hawakukesha usingetumia lugha ya Matusi. Simply ungesema unachokijua.

Ila kwa kuwa nafsi yako inashindana na ukweli, ndiyo maana jasho na Lugha kali zinakutoka ili kufanya psychological balance nafsini kwako.
 
Neno European sauti unayotamka sio U mkuu....

Unanza na Y....hahaha...fanya kama unaufanya mdomo wako mrefu embu....ndiyo utamke hilo neneo.

Sijui mnazunguzia nini. Ila kama nu mtu a European...ila kama ni muungano kwangu haisikiki vizuri kuutaja muungano wa Ulaya kama a European...bali the.

Hiyo y isikushangaze saana katika fonimu ni sauti ya kipekee saana. Kwanza inatamkiwa kwenye kaakaa gumu...lakini pia ukiingia ndani y ni irabu lakini pia konsonanti.

Samahani nimeeleza ambavyo sikuulizwa.
 
Umeanza kukata pumzi TL si LOWASSA hivi Kuna chochote alichokua akikisema Lowassa majukwaani Zaid ya ELIMU ELIMU ELIMU huyu anawavua nguo na anawapa wananchi ELIMU YA URAIA na kutambua haki ZAO wameamkaa sasa
 
Umeanza kukata pumzi TL si LOWASSA hivi Kuna chochote alichokua akikisema Lowassa majukwaani Zaid ya ELIMU ELIMU ELIMU huyu anawavua nguo na anawapa wananchi ELIMU YA URAIA na kutambua haki ZAO wameamkaa sasa
Msingi wa hoja yangu ni kuwataka wapinzani kutobweteka kwa kuangalia tu ukubwa wa mikutano ya majukwaani, naelewa fika tofauti iliyopo kati ya Lowassa na Lissu ila wanapaswa kutorudia makosa ya 2015

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…