Jiji la Mwanza lifanyiwe mabadikliko

Inasikitisha sana halafu, anakuja kiongozi anataka tumchekee tu bila kujali mahitaji yetu ya msingi kama hayo, barabara ya kenyatta imekuwa kama ulimi wa mbwa au mkia wa kondoo, jiji kubwa limejengeka lakini serikali imetususa sijui kwanini? Wabunge wanalia kila mwaka lakini hakuna wakuwasikiliza.
 
Siwezi kupinga mkuu, upo sahihi kabisaa.
 
Hao tanroad na tarura ndio wanaotuangusha pia viongoi wetu wengi hawajali kabisaa, chochote kwao ni sawa tu.
 
Mwanza ukiacha barabara mbovu is the most dark city nchini [emoji1][emoji1] barabara kuu zote taa hazifanyi kazi

Sent from my SM-N950U using JamiiForums mobile app
Ukiwa shinyanga usiku na ukija mwanza usiku utasema, shy ndio town na mwanza naenda kijijini kwasababu ya taa za barabarani, Mwanza kupewa taa au marekebisho ya taa za barabarani imekuwa kama hanasa.
 
Mimi nishauri ili jam ipungue jijini Mwanza wangetengeneza ile barabara ya mkuyuni kutokea Mwatex au kwa jina la Nilepirch road inge saidia sana maana mtu anaenda kuanzia mitaa ya neshno,mwatex,Igoma na kuendelea nilazima aingie mjini ndipo atoke kwenda hayo maeneo sasa inakuwa jam sana wakati angeingilia mkuyuni angetokea huko huko tu.
 
Sasa what is the use of kuweka taa Kenyatta wakati wana mpango wa kuipanua

Watazing'oa? Au itakuaje [emoji1]

Sent from my SM-N950U using JamiiForums mobile app
Ukiona hivyo hakuna barabara itakayojengwa hapo, serikali hii ya hovyo sana, Mwanza imekuwa kama kijijini, ukiuliza wanakuambia wapo kwenye feasibility study.
 
Well,, 90% ya barabara ulizotaja ziko manispaa ya Ilemela,,

Tizama aibu ya Nyamagana

Igoma-Kishili
Bango-Buhongwa
Kishili-Fumagila
Mwatex-Mahina
Mahina-Nyegezi
Sahwa-Buhongwa
Huku kote barabara hazipitiki hasa wakati wa mvua hii ni aibu,,
 
Nimezaliwa na kukua na kuishi Mwanza, we jamaa unaijua Mwanza nje ndani, mtoa mada angetulia akapata A,B,C kwanza maana ana argue na mtu anaujua mji kindaki ndaki, kuna mitaa na barabara umezitaja hapo ni mitaa ya home kabisa 😀
 
Katika majiji yote nadhani mbeya ndio jiji la kwanza kuwa jiji la mchongo
 
Acha makasiriko chief
Mwanza ni jiji zuri sana ukiondoa jiji la Dar kwa mtazamo wangu ndilo linafuatia
Ila linahitaji maboresho tu kama ilivyo kwa miji mingine
 
Nimezaliwa na kukua na kuishi Mwanza, we jamaa unaijua Mwanza nje ndani, mtoa mada angetulia akapata A,B,C kwanza maana ana argue na mtu anaujua mji kindaki ndaki, kuna mitaa na barabara umezitaja hapo ni mitaa ya home kabisa [emoji3]
Niko mwanza toka 2002. 21 yrs. Sema ume simuliwa uongo na uka amini uongo. Luchelele aliyo taja hakuna lami.
Bugando lami yake ime jengwa kwa ufadhili, tena Romani C. Na lami yenyewe imeishia hapo Hosp ya Bugando tu

Muulize kuna mtaa wa Nyamagana kataja hapo[emoji3][emoji3]
 
Nyie watu wa nyamagana mnapenda kuiexclude ilemela kwenye jiji la Mwanza... ilemela ni mwanza ko usianze kutafuta Chaka eti barabara ni za ilemela sio nyamagana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyie watu wa nyamagana mnapenda kuiexclude ilemela kwenye jiji la Mwanza... ilemela ni mwanza ko usianze kutafuta Chaka eti barabara ni za ilemela sio nyamagana

Sent using Jamii Forums mobile app
Ilemela unayo sifia ina barabara ngapi za lami? Igombe tu ni vumbi tupu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…