Jikoni leo na Zero IQ

da! wanaume wa dar mnaendekeza papuchi kuliko kula hako ndio kaugali mnakula na wenzako,huo msosi ni wa njemba moja ya mkoa tena anaweza asishibe
ngoja nikazie hapo
watu wa mikoa ya kanda ya ziwa huo n mlo wa mtoto
 
Zero IQ nimevutiwa na mapishi yako, naomba nikuunge wajihi hatua kwa hatua za mapishi na Kasie Makorokocho.



Viungo vunakaangwa tayari kwa kupondwa kupata ungainly wa pilau.



Vitunguu swaumu vichanga napenda kutumia hivi maana si vikali sana.



Vitunguu maji na viazi hapo bado kukatwa na kuwekwa kwenye sefuria.



Mchele ushachambuliwa.... Tayari kupikwa, huwa sioshi mchele kama nakula pilau Ila nikipika wali kwenye rice cooker huwa nauosha.



Njegere hapo ntatumia mkono mmoja tuu na karoti ntaikata size ya nusu kidole vyembamba virefu. Shurti pilau liwe na rangi.



Nyama inachemka na maji mengii ili ikiiva supu ndo maji ya kupikia pialu. Huwa sichemshi maji pembeni labda kama napika pilau ya mboga mboga au ya mayai.



Pilau imeiva, tayari kupakuliwa.



Kachumbari iko tayari...






Maji ya chungwa na mbegu zake... DIY...hand made.

K' Chief Matata.

Mengine sikuingine
 
Nashukuru sana mkuu mama la mama Kasie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…