The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 1,967
- 4,267
Anaanza kwa kukaribishwa na "Hangaya" kwa sauti nyororo ya Kizanzibari...
Lakini all in all, nasema..;
Huyu jamaa ni mtukutu sana. Anapiga nyundo sadistically kiasi cha kukera sana...!
Lakini ndo hivyo tena. Ukweli uliofichwa kwa nia ovu, ukifichuliwa na kuwekwa wazi, huwaudhi waliokuwa wameuficha...
Lakini on the other hand huyu jamaa ni jasiri sana vile vile...
Anaweza kufanya jambo ambalo wengine wote mnaweza kugwaya kulifanya. Lakini kwake hupita hapohapo bila kuogopa lolote...
Huyu jamaa ni msomi kwelikweli na ni mzalendo kwelikweli. Ufahamu na uelewa wake unampa kutawala fikra za watu. Kumbe ni kweli kabisa, KNOWLEDGE IS POWER..
Huyu jamaa hana longo longo, haogopi kumchana chana yeyote kwa hoja mpaka utainamisha kichwa chini kwa aibu...
Kwenye picha ya video hii nawaona wana CCM nyundo zikiingia sawasawa kiasi cha kuona aibu wenyewe hata kuinamisha vichwa vyao chini..
Lakini wafanyeje sasa? Ni bora mkono uende kinywani. Mambo mengine yatajiju.. haa haa haa...!!
We miss you Tundu Lissu...!!