JIKUMBUSHE (VIDEO): Tundu Lissu akisambaratisha hoja za watetezi wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar usio na ridhaa ya wananchi

JIKUMBUSHE (VIDEO): Tundu Lissu akisambaratisha hoja za watetezi wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar usio na ridhaa ya wananchi

Ndiyo maana wale waoga wa kukosolewa waliamini risasi ndiyo njia sahihi ya kumnyamazisha
Wangejifunza wenye akili hizo kwamba hoja huzimishwa kwa hoja na wala sio kwa mabavu wala kwa matusi. !!
 
Nilishauri na nashauri tena, tusilinganishe vitu visivyo fanana!. Tusimcopee TL na ZZK, compare like people and like things, TL ni level ya JPM not ZZK!.

Nilishauri na nashauri tena, tusilinganishe vitu visivyo fanana!. Tusimcopee TL na ZZK, compare like people and like things, TL ni level ya JPM not ZZK!.
P
HAPANA..

Mimi sijui unaweza kumlinganisha Tundu Lissu na JPM kwa lipi hasa..

Wote ni binadamu, Yes...

Lakini kiuongozi specifically wanatofautiana kwa kiwango kikubwa saana..

Unaweza kuhoji, wewe Ndugu The Palm Beach unamlinganishaje TL na JPM wakati TL hajawahi kuwa Rais wa nchi kama alivyokuwa JPM..?

Ni kweli TL hajawahi kuwa Rais wa nchi lakini TL was (by then) and still recognized as a public figure nationally & internationally...

Na JPM amekuwa Rais na hicho pekee mtu anaweza kumhukumu nacho kwa urahisi zaidi...

Sasa tunawezaje kumtambua mtu hata KABLA YA KUPEWA JUKUMU LA KIUONGOZI...?

Wewe unadhani ni kwanini CCM nyakati za chaguzi huogopa midahalo na interviews mbalimbali..?

Jibu ni rahisi sana. Hushitakiwa na dhamiri zao ovu (guilty conscious) ambazo kupitia njia ya midahalo zingeweza kufichuliwa kwa urahisi..!!

Na wakati wa u - Rais wa John P. Maguli, tatizo la udhaifu wake huu ulijidhihirisha several times..

SASA, kwa maoni yangu ktk msingi wa uelewa, tunaweza kumjua kiongozi bora hata kabla ya kupewa jukumu hilo kwa kuangalia baadhi ya vigezo vikuu vifuatavyo:

1. Uwezo wake wa kujieleza juu ya mambo mbalimbali..

= Hapa Tundu Lissu nampa 98% na JPM 25%..
= Kwenye eneo hili, JPM was very poor and all intelligent people know it..

2. Ndani ya kujieleza ndipo tunaweza kujua kiwango cha uelewa, ufahamu na maarifa ya mtu huyo:

= Hapa Tena kwa ufahamu wangu, TL ni msomi wa kiwango cha degree mbili (Master degree) na JPM inasemekana alikuwa msomi wa kiwango cha Phylosophy Doctorate [PhD]
= Lakini in actual sense, huyu PhD holder ndugu John P. Magufuli, uelewa na ufahamu wake ulikuwa below standard na ulithibitishwa maamuzi yake mengi ya hovyo, woga, hasira, kukosa uvumilivu, chuki, ubinafsi nk..
= Lakini hebu mtazamo huyu mwenye mater degrees. He is so smart, mvumilivu, anapima kila jambo kabla ya kulisema na kulitenda, akikosea ni apologetic, jasiri na haogopi kumwambia yeyote kuwa, THIS IS WRONG...

3. Kiwango chake cha uvumilivu na kuchukulia na watu hata anapokumbana na criticism..

= Unless uwe hujamfuatilia TL kwenye matukio na mijadala mbalimbali. Jamaa ni mvumilivu sana. Haogopi kukosolewa na ikitokea, frequency za hisia zake hubakia kuwa intact and calm..
= Kwa upande JPM, hana sifa hii. Ni complete the opposite. Havumilii mtu. Alikuwa katili sana toka enzi akiwa mbunge na waziri tu. JPM kwa kutumia nafasi yake ya utawala, alikuwa muuaji...!!

4. Kiwango chake cha uelewa wa mambo ya kitaifa na kimataifa..

= Hapa sasa ni kulinganisha mlima Kilimanjaro na Sekenke
= TL anaijua dunia. JPM alikuwa ni zero brain kwenye eneo hili. Na ukitaka kujifunza mambo ya dunia na ya nchi hii, TL anaweza kuwa mwalimu wako mzuri sana..

5. Kiwango chake cha ubinafsi au upendo kwa wengine..

= JPM was so selfish kwa kiwango cha kupita kawaida kinyume kabisa na alivyo TL..
= Sifa za mtu mbinafsi ni: kukosa uvumilivu, mwoga na mwenye hofu ya kupoteza, mwenye hasira na hujitetea kwa kutumia propaganda na uongo, is not apologetic, he is always defensive...
= Morever, a selfish person is always ready to kill anyone who criticizes him/her for his/her own selfish ambitions. Huyu ndiye alikuwa Pombe Magufuli..!!

6. Kiwango chake cha uthubutu wa kufanya mambo/kuchukua maamuzi magumu yanayoogopeka kwa watu lakini yenye manufaa kwa jamii/watu wake..

= Hapa twaweza kuwaweka kapu moja both TL na JPM, kwamba wote wana uthubutu..
= Lakini kwenye hili wanatofautiana kitu kimoja tu. Uthubutu wa JPM ktk mambo mengi aliyoyafanya kwa "kuthubutu" ni wa kijinga na uliosababisha maumivu na hasara kubwa kwa watu na jamii..
= I agree, kwamba kiongozi hapaswi kuogopa kufanya maamuzi. Lakini ni sharti maamuzi hayo yawe ingalau yamefanyiwa utafiti wa kutosha. Hii haikuwa hivyo kwa mzee Magufuli. Alifanya makosa mengi sana tokana na maamuzi yake ya "kukurupuka" kama tunavyosema..

Hawa ndiyo watu wawili unaosema wanafanana. Lakini ukweli ni kubwa hawafanani..

Karibu..
 
4. Kiwango chake cha uelewa wa mambo ya kitaifa na kimataifa..

= Hapa sasa ni kulinganisha mlima Kilimanjaro na Sekenke
= TL anaijua dunia. JPM alikuwa ni zero brain kwenye eneo hili. Na ukitaka kujifunza mambo ya dunia na ya nchi hii, TL anaweza kuwa mwalimu wako mzuri sana..
Nimecheka hadi nimeharibu hali ya hewa na vioo vya Suzuki havifunguki na kuna mvua inanyesha 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Lisu Alimpa dadaye Ubunge

Aliwachaji Chadema mamilioni ya shilingi kwenye Kesi

Sasa analamba asali
Unajua ndugu kuna maoni na kusema vitu halisi ukiwa na justifications mkononi..

Kwa hapa, mfano, uongo huu wewe unakusaidia nini..?

Laini yangekuwa ni maoni tu, tungesema ni maoni yake..

Lakini umeandika with authority kana kwamba ni kweli...

Tundu Lissu awezaje kutoa maamuzi ya taasisi kumpendelea mtu mmoja nduguye..? Hebu eleza unishawishi na mimi ili nikuamini..

Unaweza kuthibitisha huyo dada yake kwamba hakuwa na sifa na hakupitia mchakato wa kawaida kama wengine kupata nafasi ya ubunge wa VM..?
 
Naunga mkono hoja na hili hata mimi nalitambua na niliisha m profile humu
  1. Mifano ni hii Vurugu za Bungeni: Mhe.Tundu Lissu, Anastahili Adhabu Kali?!. Ni Mtundu Toka Shule!.
  2. Mhe. Tundu Lissu, Please Acha Kumsulubu Spika Wetu!, Unammaliza Kabisa Hadi Ameshindwa Kazi!.
  3. Hoja ya Udikteta wa Magufuli: Tundu Lissu isn't Right. Haupingwi kwa kupaza sauti kupiga tu Kelele!
  4. Unamjua aliyemshauri Lissu agombee urais?. Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!
  5. Je ulijua Tundu Lissu alisita kurejea nchini hadi ahakikishiwe usalama wake?, unajua kina nani walimshauri arejee hivyo hivyo hata bila kuhakikishiwa usalama wake? Kamanda Lissu, Usisubiri Jibu la IGP Kuhusu Usalama Wako, Aliyekulinda na Shambulio Lile Yupo, Yeye Aweza, na Ataendelea Kukulinda, Welcome Back Home!
  6. Lissu is very good kwa kujenga hoja ila pia ni binadamu na sio malaika, anaweza kukosea, mfano kwenye hili Lissu aliwaingiza chaka Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!
  7. Hakuna mtu anayefanikiwa peke yake, ukiona mtu kafanikiwa kwenye jambo fulani ujue kuna watu wamemsaidia alipaswa kuwashukuru Nyaraka za Muungano: Tundu Lissu kutoishukuru JF na Pasco maana yake nini?
Ukilinganisha vitu, linganisha vitu vinavyofanana, watu wanaofanana, usilinganisha mbingu na nchi au jua na mwezi!.
P
Leo tunapo adhimisha miaka 60 ya huu muungano wetu adhimu, nafanya tafakuri, niliwahi kuandika nini humu kuhusu muungano wetu.
Nawatakia maadhimisho mema ya miaka 60 ya muungano wetu adhimu.
Ujumbe wangu ni muungano wetu adhimu udumu milele, na sasa ni muda muafaka tuachane na huu muungano wa kimaghumashi, wa union na federation, sasa twende kwenye muungano wa kweli wa union wa nchi moja, serikali moja, na rais mmoja!.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Tusaidie

downloadfile.png

Nisaidie hapa Uncle Pascal Mayalla ufafanuzi kuhusu hii document
 
..Magu alikuwa tapeli wa kisiasa.

..uliwahi kumsikia akitetea wanyonge au madini kabla hajawa raisi?

..miaka yote hiyo alikuwa mlamba asali ktk awamu ya Mkapa alipouza nyumba za serikali, na ktk awamu ya Kikwete aliponunua kivuko kibovu Mv Bagamoyo.
Hivi kile Kivuko Kiko wapi Sasa!?
 
View attachment 2404531
Anaanza kwa kukaribishwa na "Hangaya" kwa sauti nyororo ya Kizanzibari...

Lakini all in all, nasema..;

Huyu jamaa ni mtukutu sana. Anapiga nyundo sadistically kiasi cha kukera sana...!

Lakini ndo hivyo tena. Ukweli uliofichwa kwa nia ovu, ukifichuliwa na kuwekwa wazi, huwaudhi waliokuwa wameuficha...

Lakini on the other hand huyu jamaa ni jasiri sana vile vile...

Anaweza kufanya jambo ambalo wengine wote mnaweza kugwaya kulifanya. Lakini kwake hupita hapohapo bila kuogopa lolote...

Huyu jamaa ni msomi kwelikweli na ni mzalendo kwelikweli. Ufahamu na uelewa wake unampa kutawala fikra za watu. Kumbe ni kweli kabisa, KNOWLEDGE IS POWER..

Huyu jamaa hana longo longo, haogopi kumchana chana yeyote kwa hoja mpaka utainamisha kichwa chini kwa aibu...

Kwenye picha ya video hii nawaona wana CCM nyundo zikiingia sawasawa kiasi cha kuona aibu wenyewe hata kuinamisha vichwa vyao chini..

Lakini wafanyeje sasa? Ni bora mkono uende kinywani. Mambo mengine yatajiju.. haa haa haa...!!

We miss you Tundu Lissu...!!
Hotuba hii itaishi hadi itakapopatikana katiba ya wananchi.
 
Leo tunapo adhimisha miaka 60 ya huu muungano wetu adhimu, nafanya tafakuri, niliwahi kuandika nini humu kuhusu muungano wetu.
Nawatakia maadhimisho mema ya miaka 60 ya muungano wetu adhimu.
Ujumbe wangu ni muungano wetu adhimu udumu milele, na sasa ni muda muafaka tuachane na huu muungano wa kimaghumashi, wa union na federation, sasa twende kwenye muungano wa kweli wa union wa nchi moja, serikali moja, na rais mmoja!.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Tusaidie
P
Wahafidhina wa Zanzibar watakubali!? Au ndio wataona wamemezwa Rasmi kwenye ukoloni wa Bara!?
 
View attachment 2404531
Anaanza kwa kukaribishwa na "Hangaya" kwa sauti nyororo ya Kizanzibari...

Lakini all in all, nasema..;

Huyu jamaa ni mtukutu sana. Anapiga nyundo sadistically kiasi cha kukera sana...!

Lakini ndo hivyo tena. Ukweli uliofichwa kwa nia ovu, ukifichuliwa na kuwekwa wazi, huwaudhi waliokuwa wameuficha...

Lakini on the other hand huyu jamaa ni jasiri sana vile vile...

Anaweza kufanya jambo ambalo wengine wote mnaweza kugwaya kulifanya. Lakini kwake hupita hapohapo bila kuogopa lolote...

Huyu jamaa ni msomi kwelikweli na ni mzalendo kwelikweli. Ufahamu na uelewa wake unampa kutawala fikra za watu. Kumbe ni kweli kabisa, KNOWLEDGE IS POWER..

Huyu jamaa hana longo longo, haogopi kumchana chana yeyote kwa hoja mpaka utainamisha kichwa chini kwa aibu...

Kwenye picha ya video hii nawaona wana CCM nyundo zikiingia sawasawa kiasi cha kuona aibu wenyewe hata kuinamisha vichwa vyao chini..

Lakini wafanyeje sasa? Ni bora mkono uende kinywani. Mambo mengine yatajiju.. haa haa haa...!!

We miss you Tundu Lissu...!!
Kwa kweli !
 
Kwenye siasa wengine huwa hawapendi au hawampendagi MTU anayeongea ukweli ulio dhahir !! Sijui tabia hii ni yetu huku dunia ya tatu au hii chuki huwa ipo duniani kote !! Tabia hii ya kuongea ukweli ulio dhahir imeshawaponza watu wengi kuingia kwenye matatizo na wale wasiopenda kuusikia ukweli !! Hatar sn !!!
Hata Yesu Kristo kwa kuwa mkweli ilimgharimu kifo lakini chake kifo kilikuwa cha faida kubwa kwa ulimwengu wote na kwa kila binadamu.

Ndivyo ilivyo kwa CCM. Hawa watu wa CCM wanaweza kukuua na ofcoz hawana hofu ya kumwaga damu ya yeyote msema ukweli, damu yenye faida kwao pekee.!!
 
Kuna ukweli tunatotakiwa kuufafanua na kama ni kero irekebishwe kama kweli tunafikiri muungano huu ni wa muhimu.

1. Wazanzibar wengi sana wanamiliki ardhi na majengo bara, kama raia. ila Wabara wanachukiwa wakienda kule, wanaitwa chogo, na katiba yao inazuia watu wa bara kumiliki ardhi. Juzi nilikuwa Dodoma, kwenda benjamin Mkapa kwenye kona ya Udom, kuna migorofa fulani hivi imejengwa, wanasema karibu na vile vijengo vya majaji, wengine wanamtaja mzanzibari fulani anamiliki hiyo migorofa. tukisema wazanzibar leo hii muungano umevunjika waondoke, wengi wataanza kuuza nyumba nyingi na ardhi kubwa wanayoimiliki. KWANINI BARA HATURUHUSIWI KUMILIKI KULE? faida yao ni nini?

2. kwenye ajira, hii ni kero, wazanzibar maelfu na maelfu wameajiriwa bara, hata kwenye mambo yasiyo ya muungano, wameajiriwa bara ambayo kiukweli ipo bara kwasababu zanzibar kuna utawala wao, lakini wabara hawaruhusiwi kabisa kuajiriwa zanzibaar, hii ni kero, inatakiwa iondolewe, ama la kila mtu abaki kwake.

3. wazanzibar wanakuwa wabunge kule kwao, na huku. akiwa mbunge kule kwao, atakula masurufu ya kule na atakuja kula masurufu ya bara kwa kodi za watu wa bara. tuambieni, yale mipesa wanaku wabunge 50 wa zanzibar wanakiula, zanzibar huwa imechangia bei gani? ni pesa za walipa kodi wa bara. na hao hao wakifika huku wakishiba, wanasenma twende kule kwa passport, kwa msiojua, kile ameongea yule mbunge wa zanzibar kwamba wabara twende kwa passport kwao ndicho kilichopo kwenye mioyo ya wazanzibari wote hata wenye mamlaka huku na hata walioajiriwa huku na hata wanaomiliki ardhi huku, amesema kilichopo kwenye mioyo ya wengi. wala hatakiwi kulaumiwa. kwa waliofika zanzibar wanajua kuwa hicho ndio huwa matamanio yao.

4. mzanzibar anaweza kuwa Mkuu wa wilaya, mkoa, na waziri bara, ila sisi kule marufuku. kwanini?

nimeongea hayo kwa uchache tu, lakini ukweli mwingi hata wanaopinga wanaujua, kama tunataka muungano uwepo, ondoeni kero hizi kwa watu wa bara, ama la, kila mtu achukue hamsini zake kwasababu hakuna kitu wabara wanafaidika nacho as of now. na hawajawahi kufaidika. watu wasioelewa watasema huu ni uchochezi, ila jibuni kwa hoja kama mnazo.
 
Naunga mkono hoja na hili hata mimi nalitambua na niliisha m profile humu
  1. Mifano ni hii Vurugu za Bungeni: Mhe.Tundu Lissu, Anastahili Adhabu Kali?!. Ni Mtundu Toka Shule!.
  2. Mhe. Tundu Lissu, Please Acha Kumsulubu Spika Wetu!, Unammaliza Kabisa Hadi Ameshindwa Kazi!.
  3. Hoja ya Udikteta wa Magufuli: Tundu Lissu isn't Right. Haupingwi kwa kupaza sauti kupiga tu Kelele!
  4. Unamjua aliyemshauri Lissu agombee urais?. Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!
  5. Je ulijua Tundu Lissu alisita kurejea nchini hadi ahakikishiwe usalama wake?, unajua kina nani walimshauri arejee hivyo hivyo hata bila kuhakikishiwa usalama wake? Kamanda Lissu, Usisubiri Jibu la IGP Kuhusu Usalama Wako, Aliyekulinda na Shambulio Lile Yupo, Yeye Aweza, na Ataendelea Kukulinda, Welcome Back Home!
  6. Lissu is very good kwa kujenga hoja ila pia ni binadamu na sio malaika, anaweza kukosea, mfano kwenye hili Lissu aliwaingiza chaka Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!
  7. Hakuna mtu anayefanikiwa peke yake, ukiona mtu kafanikiwa kwenye jambo fulani ujue kuna watu wamemsaidia alipaswa kuwashukuru Nyaraka za Muungano: Tundu Lissu kutoishukuru JF na Pasco maana yake nini?
Ukilinganisha vitu, linganisha vitu vinavyofanana, watu wanaofanana, usilinganisha mbingu na nchi au jua na mwezi!.
P
Tuungane kumu wish Tundu Lissu all the best kesho.
P
 
View attachment 2404531
Anaanza kwa kukaribishwa na "Hangaya" kwa sauti nyororo ya Kizanzibari...

Lakini all in all, nasema..;

Huyu jamaa ni mtukutu sana. Anapiga nyundo sadistically kiasi cha kukera sana...!

Lakini ndo hivyo tena. Ukweli uliofichwa kwa nia ovu, ukifichuliwa na kuwekwa wazi, huwaudhi waliokuwa wameuficha...

Lakini on the other hand huyu jamaa ni jasiri sana vile vile...

Anaweza kufanya jambo ambalo wengine wote mnaweza kugwaya kulifanya. Lakini kwake hupita hapohapo bila kuogopa lolote...

Huyu jamaa ni msomi kwelikweli na ni mzalendo kwelikweli. Ufahamu na uelewa wake unampa kutawala fikra za watu. Kumbe ni kweli kabisa, KNOWLEDGE IS POWER..

Huyu jamaa hana longo longo, haogopi kumchana chana yeyote kwa hoja mpaka utainamisha kichwa chini kwa aibu...

Kwenye picha ya video hii nawaona wana CCM nyundo zikiingia sawasawa kiasi cha kuona aibu wenyewe hata kuinamisha vichwa vyao chini..

Lakini wafanyeje sasa? Ni bora mkono uende kinywani. Mambo mengine yatajiju.. haa haa haa...!!

We miss you Tundu Lissu...!!
Time flies
Saizi mwenye kiti
 
Back
Top Bottom