1000 digits
JF-Expert Member
- Oct 16, 2012
- 7,201
- 9,529
HAPANA..
Mimi sijui unaweza kumlinganisha Tundu Lissu na JPM kwa lipi hasa..
Wote ni binadamu, Yes...
Lakini kiuongozi specifically wanatofautiana kwa kiwango kikubwa saana..
Unaweza kuhoji, wewe Ndugu The Palm Beach unamlinganishaje TL na JPM wakati TL hajawahi kuwa Rais wa nchi kama alivyokuwa JPM..?
Ni kweli TL hajawahi kuwa Rais wa nchi lakini TL was (by then) and still recognized as a public figure nationally & internationally...
Na JPM amekuwa Rais na hicho pekee mtu anaweza kumhukumu nacho kwa urahisi zaidi...
Sasa tunawezaje kumtambua mtu hata KABLA YA KUPEWA JUKUMU LA KIUONGOZI...?
Wewe unadhani ni kwanini CCM nyakati za chaguzi huogopa midahalo na interviews mbalimbali..?
Jibu ni rahisi sana. Hushitakiwa na dhamiri zao ovu (guilty conscious) ambazo kupitia njia ya midahalo zingeweza kufichuliwa kwa urahisi..!!
Na wakati wa u - Rais wa John P. Maguli, tatizo la udhaifu wake huu ulijidhihirisha several times..
SASA, kwa maoni yangu ktk msingi wa uelewa, tunaweza kumjua kiongozi bora hata kabla ya kupewa jukumu hilo kwa kuangalia baadhi ya vigezo vikuu vifuatavyo:
1. Uwezo wake wa kujieleza juu ya mambo mbalimbali..
= Hapa Tundu Lissu nampa 98% na JPM 25%..
= Kwenye eneo hili, JPM was very poor and all intelligent people know it..
2. Ndani ya kujieleza ndipo tunaweza kujua kiwango cha uelewa, ufahamu na maarifa ya mtu huyo:
= Hapa Tena kwa ufahamu wangu, TL ni msomi wa kiwango cha degree mbili (Master degree) na JPM inasemekana alikuwa msomi wa kiwango cha Phylosophy Doctorate [PhD]
= Lakini in actual sense, huyu PhD holder ndugu John P. Magufuli, uelewa na ufahamu wake ulikuwa below standard na ulithibitishwa maamuzi yake mengi ya hovyo, woga, hasira, kukosa uvumilivu, chuki, ubinafsi nk..
= Lakini hebu mtazamo huyu mwenye mater degrees. He is so smart, mvumilivu, anapima kila jambo kabla ya kulisema na kulitenda, akikosea ni apologetic, jasiri na haogopi kumwambia yeyote kuwa, THIS IS WRONG...
3. Kiwango chake cha uvumilivu na kuchukulia na watu hata anapokumbana na criticism..
= Unless uwe hujamfuatilia TL kwenye matukio na mijadala mbalimbali. Jamaa ni mvumilivu sana. Haogopi kukosolewa na ikitokea, frequency za hisia zake hubakia kuwa intact and calm..
= Kwa upande JPM, hana sifa hii. Ni complete the opposite. Havumilii mtu. Alikuwa katili sana toka enzi akiwa mbunge na waziri tu. JPM kwa kutumia nafasi yake ya utawala, alikuwa muuaji...!!
4. Kiwango chake cha uelewa wa mambo ya kitaifa na kimataifa..
= Hapa sasa ni kulinganisha mlima Kilimanjaro na Sekenke
= TL anaijua dunia. JPM alikuwa ni zero brain kwenye eneo hili. Na ukitaka kujifunza mambo ya dunia na ya nchi hii, TL anaweza kuwa mwalimu wako mzuri sana..
5. Kiwango chake cha ubinafsi au upendo kwa wengine..
= JPM was so selfish kwa kiwango cha kupita kawaida kinyume kabisa na alivyo TL..
= Sifa za mtu mbinafsi ni: kukosa uvumilivu, mwoga na mwenye hofu ya kupoteza, mwenye hasira na hujitetea kwa kutumia propaganda na uongo, is not apologetic, he is always defensive...
= Morever, a selfish person is always ready to kill anyone who criticizes him/her for his/her own selfish ambitions. Huyu ndiye alikuwa Pombe Magufuli..!!
6. Kiwango chake cha uthubutu wa kufanya mambo/kuchukua maamuzi magumu yanayoogopeka kwa watu lakini yenye manufaa kwa jamii/watu wake..
= Hapa twaweza kuwaweka kapu moja both TL na JPM, kwamba wote wana uthubutu..
= Lakini kwenye hili wanatofautiana kitu kimoja tu. Uthubutu wa JPM ktk mambo mengi aliyoyafanya kwa "kuthubutu" ni wa kijinga na uliosababisha maumivu na hasara kubwa kwa watu na jamii..
= I agree, kwamba kiongozi hapaswi kuogopa kufanya maamuzi. Lakini ni sharti maamuzi hayo yawe ingalau yamefanyiwa utafiti wa kutosha. Hii haikuwa hivyo kwa mzee Magufuli. Alifanya makosa mengi sana tokana na maamuzi yake ya "kukurupuka" kama tunavyosema..
Hawa ndiyo watu wawili unaosema wanafanana. Lakini ukweli ni kubwa hawafanani..
Karibu..
Safi sana .
Tunga kitabu kinachohusu TAL..
Tundu Lisu Pia anafuata sheria na kuwa hafuati Majungu na chuki bali sheria na katiba.
Kama mtu amekosea hakurupuki bali anaangalia sheria inasemaje?
Alipingana na JPM kuzuia makinikia kwa sababu hakufuata sheria walizokuwa wamejiwekea ambazo zingeisababishia nchi hasara kubwa . Leo hii ni kweli nchi inalipa mabilioni ya fidia kwa maamuzi ya kukurupuka ya JPM japo alikua mzalendo kama Lisu ila hakuijua sheria wala mikataba ya kimataifa na waliomzunguka jawakumbia ukweli wa kisheria .
Kumfananisha JPM na Lisu ni vitu viwili tofauti sana. Japo wote ni wazalendo na wanapinga rushwa ila mmoja anataka vifanyike kisheria na sio matamko .