JIKUMBUSHE (VIDEO): Tundu Lissu akisambaratisha hoja za watetezi wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar usio na ridhaa ya wananchi


Safi sana .
Tunga kitabu kinachohusu TAL..

Tundu Lisu Pia anafuata sheria na kuwa hafuati Majungu na chuki bali sheria na katiba.
Kama mtu amekosea hakurupuki bali anaangalia sheria inasemaje?

Alipingana na JPM kuzuia makinikia kwa sababu hakufuata sheria walizokuwa wamejiwekea ambazo zingeisababishia nchi hasara kubwa . Leo hii ni kweli nchi inalipa mabilioni ya fidia kwa maamuzi ya kukurupuka ya JPM japo alikua mzalendo kama Lisu ila hakuijua sheria wala mikataba ya kimataifa na waliomzunguka jawakumbia ukweli wa kisheria .

Kumfananisha JPM na Lisu ni vitu viwili tofauti sana. Japo wote ni wazalendo na wanapinga rushwa ila mmoja anataka vifanyike kisheria na sio matamko .
 
'anafaa sana kuwa kiongozi wa upinzani, kwa ajili ya checks and balance, ila hafai kuwa Rais wa nchi. namsapoti kwa ajili ya hilo tu. sihitaji kufafanua sana, ila kwa aliyenielewa amenielewa na atakubaliana na mimi.

kuhusu mbowe, ni msaliti asiyehitajika kabisa kwenye chama chochote cha upinzani, nikimsikia anaongea na kujifanya anatoa hotuba huwa nakereka sana sitamani hata kumsikiliza. kuna watu wanajua unafiki utafikiri walisomea.

tunamhitaji lisu awe mwenyekiti kwenye chama hicho, kwa maslahi ya checks and balances za nchi hii. huyo pekee ndiye anaweza hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…