Uchaguzi 2020 Jimbo la Kyela linahitaji Mbunge Mwanamke, wanaume wameshindwa kuleta maendeleo

Nilisoma sehemu unajinadi wewe ni tajiri !huoni Ccm imekupa utajiri ?
Utajiri wangu hauhusiani na ccm hata chembe , walijaribu hata kunifirisi kyela lakini wakaangukia pua
 
Hata Jimbo la sauli naona hakuna kinachofanyika..kifupi ccm na viongozi wake wamejichokea wanahitaji kupumzika tu
 
Kumbukumbu zangu zinaanzia kwa Mh Kasyupa Alipipi , huyu alimshinda Mwakipesile , enzi za Chama Kimoja , nilihudhuria kampeni zilizofanyika Ipande , kijiji cha Bukinga , kwenye eneo la wazi lililojulikana kama MPIKI KIMBWALA , nadhani ilikuwa mwaka 1980 ( niko tayari kusahihishwa ) wakati huo nikiwa bado mdogo sana , angalau Kasyupa unaweza kumsamehe kutokana na changamoto za wakati ule.

Baada ya Kasyupa Alipipi akaja Mwakipesile ( siyo yule aliyeshindwa na Kasyupa ) , huyu alitokea Dar es Salaam kuja kuchukua ubunge wa Kyela , na kwa vile alikuwa mkazi wa DSM hakuwa na tija yoyote kwa maendeleo ya Kyela , baada kushiba akaangushwa na Mwakyembe ambaye ndio mbunge wa Kyela hadi leo.

Kwa mujibu wa Wananchi wa Kyela mpaka sasa hakuna ahadi yoyote ya Mwakyembe iliyotimizwa katika alizowaahidi wananchi wa Kyela , ikiwemo ya kutafuta soko la Mchele wa Kyela nchini Marekani , bali kikubwa alichokifanya ni kuchangia kukausha maji ya DANIDA na kuua Taasisi ya MANGO TREE iliyokuwa msaada mkubwa wa kusaidia watoto yatima na wale wanaoishi na virusi vya Ukimwi , Ikumbukwe kwamba Kyela ni miongoni mwa maeneo yenye kiwango cha juu kabisa cha maambukizi ya Ukimwi , kutokana na mila za kizamani za kurithi wake wa Marehemu , maarufu kama " KILINGO " , sina hakika kama mpaka leo hivi vilingo bado vipo , lakini makovu yake bado yanaiteketeza Kyela kwa ukimwi , hivyo basi bado taasisi za kimataifa za kusaidia watoto yatima bado zilihitajika , Mwakyembe pia anatuhumiwa kushiriki kupora soko la Wilaya ya Kyela ambalo ndio chanzo kikuu cha mapato ya halmashauri na kulikabidhi kwa ccm kinyume kabisa cha sheria na taratibu za nchi

Mwakyembe ameshindwa kuboresha barabara zote mbadala zilizokuwepo awali na ambazo zilikuwa tegemeo , kwa mfano barabara ya kutoka daraja la Ipyana , inayopita vijiji vya Muungano , Lupembe , Ibungu , kilasilo , Mbako , Lubele hadi boda ya Kasumulu iliyokuwa tegemeo la usafiri ni kama imekufa , barabara nyingine iliyotelekezwa ni ile ya kutoka shule ya Msingi Mbako , inayopita vijiji vya Njisi , Isaki , Kabanga hadi katumbasongwe na kuunganisha hadi Ngonga na Ikolo , hii barabara ya Nkuyu hadi Matema iliyowekwa lami hivi karibuni ni mradi uliofadhiliwa na taasisi za kimataifa , hakuna juhudi zozote za Mwakyembe .

Kwa leo lengo langu halikuwa kujadili sana haya mambo bali nililenga kuonyesha jinsi wabunge wanaume wa jimbo la Kyela walivyoshindwa kuleta tija kwa maendeleo ya kyela na kushindwa kuwakomboa wananchi .

Kuna haja ya jimbo la Kyela sasa kuongozwa na Mbunge mwanamke , hii ni kutokana na hulka ya asili ya akina mama kujaa huruma na Upendo .

Hapo hoja yako ni nini kumponda mwakyembe au na demarcation ya juhudi binafsi na isiyo juhudi binafsi ni nini? huyo mbunge mwanamke ili alete nini? Tatizo Kyela kawilaya kadogo kenye wajuaji wengi, watoto wenu wamejazana dsm na mavyeo kibao mkianzisha utamaduni wa watoto wenu kujenga kwenu na kuja likizo mtajikomboa sana, nashauri ainisha nini ambacho mnadhani Kama wanakyela mnakikosa na mnadhani nguvu ya mbunge pekee ndio jibu, mna madiwani na baraza lake, na huo ujivuni bado mnachagua madiwani vilaza wakati mna form6 na degree na diploma kibao tumieni vizuri elimu yenu Kyela haipaswi kulalama mnabahati kila mahali tiss, police, jwz , elimu, vyeo na etc. Chagueni andunje awamu hii kwenye kampeni awe anasimama kwenye meza
 
Ushauri wako utachambuliwa ila mengine tutayatupa
 
Hivi ukishakuwa ofisini unapokea hela huku wapambe wako wakizipanga kwa mafungu unaweza kushindwa kukaa jf ? usiige dogo utaumia .

The district full of kujiona, inamtosha sasa afaidi na mwingine hii kasumba mwaka huu mtajamba, Harrison anachukua tena Jimbo.
 
Kumbukumbu zangu zinaanzia kwa Mh Kasyupa Alipipi , huyu alimshinda Mwakipesile , enzi za Chama Kimoja , nilihudhuria kampeni zilizofanyika Ipande , kijiji cha Bukinga , kwenye eneo la wazi lililojulikana kama MPIKI KIMBWALA , nadhani ilikuwa mwaka 1980 ( niko tayari kusahihishwa ) wakati huo nikiwa bado mdogo sana , angalau Kasyupa unaweza kumsamehe kutokana na changamoto za wakati ule.

Baada ya Kasyupa Alipipi akaja Mwakipesile ( siyo yule aliyeshindwa na Kasyupa ) , huyu alitokea Dar es Salaam kuja kuchukua ubunge wa Kyela , na kwa vile alikuwa mkazi wa DSM hakuwa na tija yoyote kwa maendeleo ya Kyela , baada kushiba akaangushwa na Mwakyembe ambaye ndio mbunge wa Kyela hadi leo.

Kwa mujibu wa Wananchi wa Kyela mpaka sasa hakuna ahadi yoyote ya Mwakyembe iliyotimizwa katika alizowaahidi wananchi wa Kyela , ikiwemo ya kutafuta soko la Mchele wa Kyela nchini Marekani , bali kikubwa alichokifanya ni kuchangia kukausha maji ya DANIDA na kuua Taasisi ya MANGO TREE iliyokuwa msaada mkubwa wa kusaidia watoto yatima na wale wanaoishi na virusi vya Ukimwi , Ikumbukwe kwamba Kyela ni miongoni mwa maeneo yenye kiwango cha juu kabisa cha maambukizi ya Ukimwi , kutokana na mila za kizamani za kurithi wake wa Marehemu , maarufu kama " KILINGO " , sina hakika kama mpaka leo hivi vilingo bado vipo , lakini makovu yake bado yanaiteketeza Kyela kwa ukimwi , hivyo basi bado taasisi za kimataifa za kusaidia watoto yatima bado zilihitajika , Mwakyembe pia anatuhumiwa kushiriki kupora soko la Wilaya ya Kyela ambalo ndio chanzo kikuu cha mapato ya halmashauri na kulikabidhi kwa ccm kinyume kabisa cha sheria na taratibu za nchi

Mwakyembe ameshindwa kuboresha barabara zote mbadala zilizokuwepo awali na ambazo zilikuwa tegemeo , kwa mfano barabara ya kutoka daraja la Ipyana , inayopita vijiji vya Muungano , Lupembe , Ibungu , kilasilo , Mbako , Lubele hadi boda ya Kasumulu iliyokuwa tegemeo la usafiri ni kama imekufa , barabara nyingine iliyotelekezwa ni ile ya kutoka shule ya Msingi Mbako , inayopita vijiji vya Njisi , Isaki , Kabanga hadi katumbasongwe na kuunganisha hadi Ngonga na Ikolo , hii barabara ya Nkuyu hadi Matema iliyowekwa lami hivi karibuni ni mradi uliofadhiliwa na taasisi za kimataifa , hakuna juhudi zozote za Mwakyembe .

Kwa leo lengo langu halikuwa kujadili sana haya mambo bali nililenga kuonyesha jinsi wabunge wanaume wa jimbo la Kyela walivyoshindwa kuleta tija kwa maendeleo ya kyela na kushindwa kuwakomboa wananchi .

Kuna haja ya jimbo la Kyela sasa kuongozwa na Mbunge mwanamke , hii ni kutokana na hulka ya asili ya akina mama kujaa huruma na Upendo .
Mkuu tuwalaumu Chadema kwa udhaifu wao kwani Mwakyembe hana mpinzani Kyela na safari hii pia atapita ,mtu anayeweza kumzuia Mwakyembe ni Mwenyekiti wa CCM wa Taifa tu,kwa Chadema nilidhani wangempitisha Mwakalinga aliyetoka CCM na kujiunga na Chadema nadhani Mwakalinga alikuwa na uwezo wa kupambana na Mwakyembe,hivi sasa Mwakalinga yuko Uingereza na haya mambo ya siasa kisha achana nayo sababu si CCM wala Chadema ambao wako makini kuteua watu ambao wanafaa na mwisho Chadema mumekuwa mabingwa wa mitandaoni na kugombania kuzika maiti hapo mtavaa migwanda myeusi na miwani kujionyesha ukamanda,ndugu yangu kwenye mazishi hakuna kura,Chadema tunaiona tu misibani hapa Kyela,Chadema ishajifia hapa Kyela,tatizo nililoliona kwa Chadema mumefanya Chadema ni Mbowe yey na wapambe zake ukiwemo na wewe,akina Yericko ndio Alfa na Omega na Chadema sasa ni Ufipa tu huku kwingine hamna la maana.Utake usitake Chadema mna safari ndefu saana,na kingine mko vocal tu kwenye vicentre/vijiwe vya biashara barabarani huko ndani vijijini hakuna na wengi wenu kazi ni kupiga kelele tu barabarani lakini kwenye kura wengi utakuta hamuendi kupiga kura ,wake zenu utakuta wapo barabarani wanauza maembe badala ya kwenda kupiga kura,au utakuta wengi wao wanapiga debe kwenye vituo vya mabasi na wengine wapo njiani kuhangaikia maisha wakati wenzao wako kupiga kura,ukiwaona vituo vya kupigia kura utakuta tayari wameshalewa.Sioni mtu wa kumg'oa Mwakyembe kwa sasa pamoja na mapungufu kibao aliyonayo,kwa taarifa yako kuanzia Matema,Mwaya ,Ipinda ,Tenende yote kaiteka ana mtaji wa kusema ameleta barabara yenye kiwango cha Highway lakini ipo vijijini.
 
Nani asiyekujua wewe mbeba begi wa Mwakyembe !
 
duh, sikuiona mapema hii. kwa mtazamo wangu, mwakalinga alikosea kujinasibisha kisiasa na lowasa. lowasa ni kama bundi kwenye siasa za tanzania.
 
si kila aliyeingia chadema 2015 alijinasibisha na lowassa , angalia Bulaya kama mfano
 
Back
Top Bottom