Uchaguzi 2020 Jimbo la Kyela linahitaji Mbunge Mwanamke, wanaume wameshindwa kuleta maendeleo

Nilisoma sehemu unajinadi wewe ni tajiri !huoni Ccm imekupa utajiri ?
Utajiri wangu hauhusiani na ccm hata chembe , walijaribu hata kunifirisi kyela lakini wakaangukia pua
 
Hata Jimbo la sauli naona hakuna kinachofanyika..kifupi ccm na viongozi wake wamejichokea wanahitaji kupumzika tu
 

Hapo hoja yako ni nini kumponda mwakyembe au na demarcation ya juhudi binafsi na isiyo juhudi binafsi ni nini? huyo mbunge mwanamke ili alete nini? Tatizo Kyela kawilaya kadogo kenye wajuaji wengi, watoto wenu wamejazana dsm na mavyeo kibao mkianzisha utamaduni wa watoto wenu kujenga kwenu na kuja likizo mtajikomboa sana, nashauri ainisha nini ambacho mnadhani Kama wanakyela mnakikosa na mnadhani nguvu ya mbunge pekee ndio jibu, mna madiwani na baraza lake, na huo ujivuni bado mnachagua madiwani vilaza wakati mna form6 na degree na diploma kibao tumieni vizuri elimu yenu Kyela haipaswi kulalama mnabahati kila mahali tiss, police, jwz , elimu, vyeo na etc. Chagueni andunje awamu hii kwenye kampeni awe anasimama kwenye meza
 
Ushauri wako utachambuliwa ila mengine tutayatupa
 
Hivi ukishakuwa ofisini unapokea hela huku wapambe wako wakizipanga kwa mafungu unaweza kushindwa kukaa jf ? usiige dogo utaumia .

The district full of kujiona, inamtosha sasa afaidi na mwingine hii kasumba mwaka huu mtajamba, Harrison anachukua tena Jimbo.
 
Mkuu tuwalaumu Chadema kwa udhaifu wao kwani Mwakyembe hana mpinzani Kyela na safari hii pia atapita ,mtu anayeweza kumzuia Mwakyembe ni Mwenyekiti wa CCM wa Taifa tu,kwa Chadema nilidhani wangempitisha Mwakalinga aliyetoka CCM na kujiunga na Chadema nadhani Mwakalinga alikuwa na uwezo wa kupambana na Mwakyembe,hivi sasa Mwakalinga yuko Uingereza na haya mambo ya siasa kisha achana nayo sababu si CCM wala Chadema ambao wako makini kuteua watu ambao wanafaa na mwisho Chadema mumekuwa mabingwa wa mitandaoni na kugombania kuzika maiti hapo mtavaa migwanda myeusi na miwani kujionyesha ukamanda,ndugu yangu kwenye mazishi hakuna kura,Chadema tunaiona tu misibani hapa Kyela,Chadema ishajifia hapa Kyela,tatizo nililoliona kwa Chadema mumefanya Chadema ni Mbowe yey na wapambe zake ukiwemo na wewe,akina Yericko ndio Alfa na Omega na Chadema sasa ni Ufipa tu huku kwingine hamna la maana.Utake usitake Chadema mna safari ndefu saana,na kingine mko vocal tu kwenye vicentre/vijiwe vya biashara barabarani huko ndani vijijini hakuna na wengi wenu kazi ni kupiga kelele tu barabarani lakini kwenye kura wengi utakuta hamuendi kupiga kura ,wake zenu utakuta wapo barabarani wanauza maembe badala ya kwenda kupiga kura,au utakuta wengi wao wanapiga debe kwenye vituo vya mabasi na wengine wapo njiani kuhangaikia maisha wakati wenzao wako kupiga kura,ukiwaona vituo vya kupigia kura utakuta tayari wameshalewa.Sioni mtu wa kumg'oa Mwakyembe kwa sasa pamoja na mapungufu kibao aliyonayo,kwa taarifa yako kuanzia Matema,Mwaya ,Ipinda ,Tenende yote kaiteka ana mtaji wa kusema ameleta barabara yenye kiwango cha Highway lakini ipo vijijini.
 
Nani asiyekujua wewe mbeba begi wa Mwakyembe !
 
duh, sikuiona mapema hii. kwa mtazamo wangu, mwakalinga alikosea kujinasibisha kisiasa na lowasa. lowasa ni kama bundi kwenye siasa za tanzania.
 
duh, sikuiona mapema hii. kwa mtazamo wangu, mwakalinga alikosea kujinasibisha kisiasa na lowasa. lowasa ni kama bundi kwenye siasa za tanzania.
si kila aliyeingia chadema 2015 alijinasibisha na lowassa , angalia Bulaya kama mfano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…