KERO Jimbo la Lupa-Chunya limetawaliwa na CCM tangu uhuru, halina barabara ya lami hata nusu kilometer

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Na wewe mleta mada acha uongo, kwamba hakuna hata nusu kilomita ya lami.
Jimbo la Lupa linaanzia Chalangwa mpaka Kambikatoto (mpakani na Rungwa). Kilomita za lami kutoka Mbeya Mjini ni 114 mpaka Makongolosi. Labda kama unamaanisha kutoka Makongolosi mpaka Rungwa (kilomita zaidi ya 300).
 
Mimi huwa nasikitishwa sana na ubora wa hizi barabara. Kwanini tunajenga basi kama hatuna hela ya kutosha, watu wasomi tunao lakini maamuzi yao ni hovyo kabisa. Kwa mkoa wa Mbeya imekua kawaida sasa kujenga barabara zenye ubora hafifu, kila siku ni kuziba mashimo tuu.
 
CCM ni adui mkubwa wa maendeleo ya nchi hii
 
Hizo wanaita sijui periodic maintenance ndiko wanakopiga pesa ndefu mkuu
 
Nina maamishamakongorosi Hadi Rungwa kms 300. Na kutoka Rungwa kwenda Itigi mkoa wa singida kms 175
 
Majimbo yaliyo wazi kabisaa na ccm huko wanajua na walioko huko ni hewa, ni Jimbo la Lupa, Chunya, mkoa wa mbeya na Jimbo la Sioknge mkoa wa Tabora.

Ila mkoa wa Tabora,na singida ni mikoa inayohitajika kutawaliwa na wakoloni. CCM imeshindwa kabisa.
Hali ya umaskini mikoa hiyo ni mkubwa sana sana.
 
Una maana jimbo la Ilala liendelee kukaliwa na CCM kwa kuwa lina Maendeleo makubwa na linaongoza kwa Mapato!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…