KERO Jimbo la Lupa-Chunya limetawaliwa na CCM tangu uhuru, halina barabara ya lami hata nusu kilometer

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Na wewe mleta mada acha uongo, kwamba hakuna hata nusu kilomita ya lami.
Jimbo la Lupa linaanzia Chalangwa mpaka Kambikatoto (mpakani na Rungwa). Kilomita za lami kutoka Mbeya Mjini ni 114 mpaka Makongolosi. Labda kama unamaanisha kutoka Makongolosi mpaka Rungwa (kilomita zaidi ya 300).
 
Tena ni sehemu strategic kwenye maendeleo, kuna madini ya dhahabu, kuna kilimo cha zao la tumbaku, kuna ufugaji wa ng'ombe na kule mbele kama unaelekea Tabora kuna hifadhi zenye wanyama pori.

Ni aibu kwamba ile barabara kuu kabisa inayounganisha Mbeya na mikoa ya Tabora na Singida ni ya vumbi.

Kichekesho zaidi ni kile kipande 'kipya' cha lami kinachotokea mbeya mjini mpaka Chunya mjini, barabara haina hata muda mrefu imejaa mashimo ya kutisha. Mchina ametupiga pale, nchi shamba la bibi hili.
Mimi huwa nasikitishwa sana na ubora wa hizi barabara. Kwanini tunajenga basi kama hatuna hela ya kutosha, watu wasomi tunao lakini maamuzi yao ni hovyo kabisa. Kwa mkoa wa Mbeya imekua kawaida sasa kujenga barabara zenye ubora hafifu, kila siku ni kuziba mashimo tuu.
 
CCM ni adui mkubwa wa maendeleo ya nchi hii
 
Mimi huwa nasikitishwa sana na ubora wa hizi barabara. Kwanini tunajenga basi kama hatuna hela ya kutosha, watu wasomi tunao lakini maamuzi yao ni hovyo kabisa. Kwa mkoa wa Mbeya imekua kawaida sasa kujenga barabara zenye ubora hafifu, kila siku ni kuziba mashimo tuu.
Hizo wanaita sijui periodic maintenance ndiko wanakopiga pesa ndefu mkuu
 
Na wewe mleta mada acha uongo kwamba hakuna hata nusu kilomita ya lami.
Jimbo la Lupa linaanzia Chalangwa mpaka Kambikatoto (mpakani na Rungwa). Kilomita za lami kutoka Mbeya Mjini ni 114 mpaka Makongolosi. Labda kama unamaanisha kutoka Makongolosi mpaka Rungwa (kilomita zaidi ya 300).
Nina maamishamakongorosi Hadi Rungwa kms 300. Na kutoka Rungwa kwenda Itigi mkoa wa singida kms 175
 
Majimbo yaliyo wazi kabisaa na ccm huko wanajua na walioko huko ni hewa, ni Jimbo la Lupa, Chunya, mkoa wa mbeya na Jimbo la Sioknge mkoa wa Tabora.

Ila mkoa wa Tabora,na singida ni mikoa inayohitajika kutawaliwa na wakoloni. CCM imeshindwa kabisa.
Hali ya umaskini mikoa hiyo ni mkubwa sana sana.
 
Ukweli Tanganyika ni nchi ngumu.
Jimbo la lupa lililopo chunya, halina hata nusu Kilomita ya Barbara ya Lami.

Na Cha kufurahisha mbunge wake Yuko bungeni na anatarajia kurudi kuomba kura tena, ili aendelee kuwa mbunge wa Lupa.

Ninashauri CCM itusaidie kumuondoa mbunge wa sasa, itupatie mtu anayeelewa wananchi wanachokitaka.

Cha kufurahisha zaidi hata maji safi na salama hayapo, Jimbo nzima
Una maana jimbo la Ilala liendelee kukaliwa na CCM kwa kuwa lina Maendeleo makubwa na linaongoza kwa Mapato!
 
Back
Top Bottom